Maoni ya Mnyika dhidi ya hotuba ya rais ya mwezi Juni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maoni ya Mnyika dhidi ya hotuba ya rais ya mwezi Juni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, Jul 2, 2012.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,652
  Trophy Points: 280
  MAONI YA MBUNGE WA UBUNGO KUHUSU HOTUBA YA MH. DKT. JAKAYA KIKWETE RAIS WA TANZANIA KWA WANANCHI TAREHE 30 JUNI 2012

  Leo tarehe 1 Julai 2012 kumesambazwa katika mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari hotuba ya Mh. Dkt. Jakaya Kikwete Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi inayotajwa kutolewa tarehe 30 Juni 2012.

  Kufuatia hotuba hiyo na kufuatia mwito kutoka wachangiaji wa mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kutaka maoni yangu kuhusu hotuba husika, naomba nichukue fursa hii kutoa maoni kwa nafasi yangu ya ubunge kuhusu hotuba tajwa kama ifuatavyo:

  Hotuba hiyo ya Rais imeibua mjadala na masuala ambayo yanahitaji kujadiliwa bungeni katika mkutano wa nane wa Bunge unaoendelea hivyo, serikali isiendelee tena kutumia kisingizio cha mahakama kulizua bunge kujadili masuala husika wakati yenyewe inayajadili na kuyatolea maelezo na maelekezo pamoja na kuchukua hatua hususani kuhusu suala la mgomo wa madaktari.

  Hotuba hiyo ya Rais ukindoa suala la usafirishaji haramu wa watu nchini inaelekea kuwa ndiyo kauli ya Serikali ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliahidi kwamba ingetolewa bungeni lakini baadaye serikali ikasema haitatoa kauli. Uamuzi wa Serikali kuitoa kauli hiyo kupitia hotuba ya Rais una mwelekeo wa kukwepa wabunge wasijadili hotuba husika na pia wasitimize wajibu wa kikatiba wa ibara 63 (2) wa kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi.

  Hivyo, Ofisi ya Rais na Ikulu wanapaswa kutoa maelezo kwa umma sababu za Rais kutolihutubia taifa tarehe 30 Juni 2012 kama ilivyotangazwa katika baadhi ya vyombo vya habari vya kielectroniki na badala yake hotuba ya Rais kusambazwa tarehe 1 Julai 2012 kupitia mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari na iwapo masuala ya hotuba hiyo kuhusu mgomo wa madaktari ndiyo yale ambayo Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikusudia kuyaeleza bungeni.

  Aidha, kwa kuwa bunge litajadili mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya Ofisi ya Rais kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2012/2013 kuanzia kesho tarehe 2 Julai 2012 na kuendelea ni muhimu wabunge wakajadili pia masuala ambayo Rais ameyaeleza kwa taifa na kutimiza wajibu wa kikatiba kwa mujibu wa ibara ya 63 (2) wa kuishauri na kuisimamia serikali.

  Kuhusu Usafirishaji Haramu wa Binadamu Nchini
  Ni vizuri hotuba ya Rais imeeleza wazi kwamba tukio la Chitego, Dodoma la wahamiaji haramu kukamatwa na wengine kukutwa wamekufa si la kwanza kutokea hapa Tanzania kwa kuwa kwa kipindi cha miaka kumi kumekuwa na ongezeko la usafirishaji haramu wa binadamu katika taifa letu kupitia mipaka ya mikoa mbalimbali hapa nchini. Kwa mbinu yoyote ile ambayo imetumika, matukio haya yanaashiria kwamba mipaka yetu haipo salama kwa kuwa kama malori na vyombo vingine vya usafiri vyenye watu wasio na hati za kuingilia nchini wanaweza kuingia kwa wingi kwa nyakati mbalimbali tafsiri yake ni kwamba nchi iko kwenye hatari ya kuingiziwa pia vitu vingine haramu ikiwemo madawa ya kulevya na silaha hali ambayo ni tishio kwa usalama wa nchi na maisha ya wananchi. Ni vizuri Rais amekutana tarehe 27 Juni 2012 na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama kuzungumzia tukio hilo; hata hivyo, zaidi ya kuwapongeza vyombo vya dola kwa kazi nzuri ya kudhibiti shughuli za biashara haramu, nilitarajia kwamba Rais kwa mujibu wa mamlaka yake ya ibara ya 33 (2) ya mkuu wa nchi, kiongozi wa serikali na amiri jeshi mkuu angeagiza uchunguzi ufanyike kuhusu udhaifu uliojitokeza na kuagiza hatua kuchukuliwa kwa walishindwa kudhibiti hali hiyo katika mipaka ambayo biashara haramu ya usafirishaji wa watu inapitia. Izingatiwe kwamba mianya hii katika mipaka yetu ina athari pana sio katika suala hili tu bali pia katika usalama wa maisha ya wananchi kama ilivyo katika mikoa ya Kigoma, Kagera na kwingineko ambapo uhai wa wananchi na mali zao uko mashakani kutokana na uvamizi toka kwa wahamiaji haramu. Aidha, athari za hali hiyo zimejitokeza katika usambazaji wa chakula toka kwenye hifadhi ya taifa ambapo pamoja na Serikali kutumia zaidi ya bilioni 27 kusambaza mahindi na nafaka nyinginezo bei za bidhaa hizo katika Soko la Dar es salaam ikiwemo katika Jimbo la Ubungo hazikushuka kutokana na vyakula hivyo kutoroshwa na kuuzwa nje ya nchi kutokana na udhaifu katika ulinzi kwenye mipaka.

  Hivyo, ni muhimu wabunge wakati wa mjadala wa bajeti ya ofisi ya Rais wataka kuongezeka kwa uwajibikaji na usimamizi wa utawala wa sheria ili kudumisha amani nchini.

  Hatua ambazo zinapaswa kuchukuliwa ni pamoja na bunge kuisimamia serikali kuhakikisha idara ya usalama wa taifa inafanya kazi kwa ufanisi zaidi katika kuvisaidia vyombo vingine vya dola kulinda mipaka ya nchi na pia matatizo ya maslahi katika vyombo vya ulinzi na usalama yanatatuliwa ili vyombo husika viweze kufanya kazi bila baadhi ya maofisa wake kujihusisha na vitendo vya ufisadi na kuruhusu biashara haramu za aina mbalimbali.

  Kuhusu Mgomo wa Madaktari

  Kuhusu mgomo wa Madaktari unaoendelea nchini hivi sasa; hotuba ya Rais imeendeleza kauli za upande mmoja ambazo zimekuwa zikitolewa na serikali kuhusu mgogoro huo bila taifa kupewa fursa ya kupata maelezo na vielezo vya upande wa pili; hivyo kuwa serikali imetoa kauli yake hadharani badala ya bungeni au mahakamani, ni muhimu pia taarifa ya kamati ya bunge ya huduma za jamii iliyoshughulia suala hilo na kukutana na pande zote mbili itoe taarifa yake bungeni na kwa umma.

  Katika hotuba yake Rais amewaeleza kwa kiwango kikubwa wananchi namna ambavyo madaktari wanasababisha mahangaiko kwa wagonjwa wengi na kusababisha vifo kwa wengine lakini hakueleza kabisa mchango wa serikali katika kusababisha hali hiyo. Hivyo, kwa kuwa pande zote mbili zinachangia katika athari zinazoikumba nchi na wananchi kutokana na mgomo; ni muhimu chombo cha tatu kikaingilia kati kuwezesha ufumbuzi kupatikana na chombo hicho ni bunge ambalo ndilo lenye wajibu wa kuisimamia serikali. Jitihada za kuwalazimisha madaktari kurejea kazini bila majadiliano ya pande mbili mbele ya chombo cha kuisimamia serikali kushughulikia chanzo cha mgogoro huo zinaweza kuleta ufumbuzi wa muda mfupi na athari za muda mrefu.

  Ieleweke kwamba hata madaktari wakisitisha mgomo wa wazi kutokana na amri ya mahakama na agizo la Rais, migogoro katika ya serikali na watumishi wa umma wenye kusababisha migomo baridi ya chinichini ina madhara ya muda mrefu kwa taifa.

  Mathalani, kutokana na migomo baridi na huduma mbovu katika sekta ya afya wananchi wa kawaida wamekuwa wakifa kutokana na magonjwa yanayotibika.

  Migomo ya chini kwa chini ya walimu na mazingira mabovu yamekuwa yakisababisha kudidimia kwa elimu katika shule za umma; mwanafunzi aliyehitimu masomo yake bila kujua kusoma na kuandika hana tofauti na mgonjwa anayekufa kwa kukosa huduma.

  Hali hii ya kugoma kusiko kwa wazi imeenza kujipenyeza mpaka kwa askari wa vyombo vya ulinzi na usalama kwa kuachia mianya ufisadi na kushindwa kusimamia utawala wa sheria kama ivyodhihirika kwa kuongezeka kwa vitendo vya biashara haramu katika taifa letu.

  Rais amewaeleza wananchi kuwa kati ya tarehe 10 Aprili, 2012 na tarehe 30 Mei, 2012, vilifanyika vikao sita vya majadiliano kati ya Serikali na Chama cha Madaktari na kwamba katika mazungumzo hayo hoja au madai 12 ya madaktari yalizungumzwa na pande zote mbili zilifikia muafaka na kukubaliana wa pamoja kwa mambo saba. Hata hivyo, katika masuala matano yaliyobaki, Rais hakueleza kwa wananchi nini ambacho serikali ilikuwa tayari kutoa kwa kila madai na kwa kiasi gani badala yake ameonyesha tu kwa ujumla kwamba madai hayo hayatekelezi.

  Aidha, kufuatia hotuba hii ya Rais Madaktari nao wana wajibu wa kuueleza umma msingi wa madai yao na kwa kiwango gani walikuwa tayari kushuka kutoka katika madai yao ya awali, kinyume na hayo itaonekana kwamba madaktari waliingia katika majadiliano wakiwa na msimamo wa kutaka madai yao pekee ndiyo yakubaliwe wakati ufumbuzi wa mgogoro wa pande mbili hupatikana kwa win win (give and take).

  Ni vizuri ikafahamika kwamba katika majadiliano, pande zote mbili huwa na mapendekezo yake; hivyo upo uwezekano kwamba yapo madai ambayo madaktari wameyatoa ambayo serikali haina uwezo wa kuyatimiza kwa kiwango walivyopendekeza na yapo ambayo serikali imeyakataa wakati ambao ina uwezo wa kuyatekeleza hata ikiwa kwa kiwango pungufu ya kile kilichopendekezwa na madaktari.

  Suluhu katika mgogoro kama huo ambao kila upande una mapendekezo yake linapaswa kufanywa na vyombo vya usuluhishi; hata hivyo kuwa suala hili linahusu mgawanyo wa rasilimali za nchi na bajeti ya serikali, chombo chenye mamlaka ya kuisimamia serikali kwa niaba ya wananchi ni bunge.

  Na kwa kuwa kamati ya bunge ya huduma za jamii ilikutana na pande mbili, ilikuwa muhimu kwa serikali kabla ya kupeleka shauri mahakamani kurejesha kwamba suala husika bungeni ambalo ndilo lenye wajibu wa kupendekeza vipaumbele vya mpango wa serikali na ndilo lenye kuidhinisha bajeti ya matumizi ya serikali.

  Uamuzi wa serikali kukimbilia mahakamani kabla ya majadiliano ya bunge umechangia katika kusababisha mgomo wa madaktari, hivyo ushauri wangu kwa Rais Kikwete ni kwa serikali kufuta kesi iliyoko mahakamani ili bunge lipewe fursa ya kujadili ripoti yake kamati yake na kupitisha maazimio ya kuwezesha suluhu kati ya serikali na madaktari.

  Mahakama iwe ni hatua ya mwisho baada ya mihimili miwili muhimu ya serikali na bunge kushindwa kuupatia ufumbuzi mgogoro unaoendelea wenye athari kwa nchi na maisha ya wananchi.

  Rais Kikwete ameeleza taifa kwamba Serikali imeongeza sana bajeti ya sekta ya afya kutoka shilingi bilioni 300 2005/2006 hadi shilingi trilioni 1.2 mwaka 2011/12; hata hivyo serikali inapaswa pia kulieleza taifa namna ambavyo kiwango hicho cha fedha kinapungua ukiweka kizio (factor) cha kushuka kwa thamani ya shilingi na mfumumo wa bei ukilinganisha mwaka 2005 na 2012.

  Ukweli ni kwamba bajeti ya Sekta ya Afya bado ni ndogo kwa kuwa serikali haijatimiza bado azimio la kutenga asilimia 15 kwa ajili ya bajeti ya afya pia, hata kiwango hicho cha ongezeko la fedha hakijaleta matokeo ya kutosha kutokana na matumizi kuelekezwa kwenye baadhi ya maeneo yasiyokuwa ya kipaumbele na kuwa na utegemezi wa kiwango kikubwa cha fedha za wahisani ambazo kwa mwaka huo wa 2011/2012 aliourejea Rais Kikwete hakikutolewa kwa kiwango kilichoahidiwa. Hivyo, Rais Kikwete awezeshe kuongezwa kwa fedha za ndani kwenye bajeti ya afya kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Katika madai mengine Rais Kikwete ameeleza kwamba pande mbili zilifikia makubaliano nusu nusu, hali ambayo inaashiria kwamba madaktari wana hoja ambazo zinahitaji majadiliano hivyo, ni muhimu bunge likapewa nafasi ya kujadili kuweza kuwakilisha pande zote mbili za serikali na madaktari kuhusu nini kinawezekana na nini hakiwezekani ili kulinusuru taifa na mgogoro unaoendelea.

  Rais Kikwete ametumia kwa kiwango kikubwa madai ya madaktari ya ongezeko la mshahara kujaribu kuwachonganisha wananchi na madaktari kwa kuwa na madai yasiyotekelezeka. Hata hivyo, ni muhimu ikafahamika kwamba sio madaktari pekee ambao wana mgogoro na mwajiri wao yaani serikali kuhusu kiwango cha mshahara bali pia watumishi wengine wa umma ikiwemo walimu.

  Nyongeza iliyotolewa na serikali ya kati ya asilimia 15 na 20 kwenye mwaka wa fedha 2012/2013 ni tofauti na ahadi ambazo serikali imekuwa ikitoa kwa wafanyakazi za kuongeza mishahara na kupunguza kodi katika mishahara. Rais Kikwete na serikali warejee maoni na mapendekezo ya kambi rasmi ya upinzani kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na 2012/2013 kuhusu nyongeza za mishahara kwa watumishi wa umma na vyanzo mbadala vya mapato vya kuongeza kwa ajili ya kuwa na uwezo wa kutimiza mahitaji. Uwiano wa sasa wa matumizi ya mishahara kuwa asilimia 48 ya bajeti badala ya uwiano mzuri wa asilimia 35 kuwa mishahara na na asilimia 65 zitumike kugharimia huduma na shughuli nyingine za maendeleo ya wananchi na taifa; ni matokeo ya udhaifu wa serikali katika kupanua vyanzo vya mapato, kupunguza matumizi ya kawaida yasiyo ya lazima na kuongeza fedha katika miradi ya maendeleo hali ambayo Rais Kikwete kuliwezesha bunge kuisimamia serikali na kuirekebisha.


  Kuhusu Suala la Dkt. Steven Ulimboka

  Rais Kikwete ameeleza wananchi kuwa ameelekeza vyombo vyetu vya ulinzi na usalama kufanya uchunguzi wa kina ili ukweli ujulikane; hata hivyo kauli hii inaashiria kukubaliana na hatua iliyochukuliwa na jeshi la polisi kuunda jopo la kuchunguza.

  Nilitarajia Rais Kikwete kwa kutambua uwepo wa madai ya polisi kutuhumiwa kuhusika katika jaribio la mauji ya Dr Ulimboka angetangaza kuunda tume huru ya uchunguzi au walau angeongeza nguvu katika jopo la uchunguzi lililoundwa kwa kuunda timu ya maafisa waandamizi wa vyombo vya ulinzi na usalama na usalama pamoja na wadau wengine kutoka taasisi huru.

  Rais Kikwete anapaswa kutumia madaraka yake kwa mujibu wa katiba kuunda tume huru ambayo inadhihirisha kwa vitendo kwamba watuhumiwa hawajichunguzi wenyewe na kuwezesha matokeo ya uchunguzi kuaminika.

  Narudia kuwasihi madaktari kuendelea kuokoa maisha ya wananchi katika kipindi hiki kigumu lakini wakati huo huo Rais Kikwete aiongoze serikali kuepusha athari zaidi katika sekta ya afya ya kuwa na mgogoro na madaktari kwa kuliwezesha bunge kujadili suala hili na kulipatia ufumbuzi ikiwemo kupitia nyongeza ya bajeti ya Wizara ya Afya. Nimemwandikia barua Spika Anna Makinda akiwa ni mkuu bunge kama muhimili mmojawapo wa dola kuweza kuchukua hatua stahili, naomba pande zote zizingatie maoni yanayotolewa na wabunge kwa niaba ya wananchi kwa maslahi ya taifa.

  Maoni haya yametolewa leo tarehe 1 Julai 2012 na:

  John Mnyika (Mb)
  Bungeni-Dodoma

  COPIED FROM http://mnyika.blogspot.com/2012/07/maoni-ya-mbunge-wa-ubungo-kuhusu-hotuba.html

  MT TAKE:
  Kweli ukitaka kupiga piga panapo huma zaidi,
  Dogo amegundua dhaifu ni dhaifu, basi anaendelea kuonyesha udhaifu wa dhaifu kwa kuonyesha madhaifu ya dhaifu.
   
 2. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #2
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,782
  Likes Received: 2,391
  Trophy Points: 280
  ndugu mnyika tanzania haina rais,maoni ni kupoteza muda chukua hatua sasa.JK amewezaje kuzungumzia suala lilopo mahakam
   
 3. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #3
  Jul 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  lililoongelewa bungeni haliwezi kushtakiwa, lililopo mahakamani haliwezi kujadiliwa bungeni, kwa maneno rahisi ni kuwa MJADALA WA BUNGE HAUATHIRI MAHAKAMA, labda tumekuwa wajinga wa mahakama!
  WABUNGE JADILINI.
   
 4. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #4
  Jul 2, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Umesomeka Kamanda Mnyika!
   
 5. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #5
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Mihimili iko mi3 ni kweli.
  Lakini ikumbukwe Head of State hapatikani kutoka katika kila muhimili.
  Ni muhimili mmoja kati ya mi3 ndiyo una TOP (RAIS)
  1. RAIS
  2. SPIKA
  3. JAJI MKUU
  Aidha AMIRI JESHI MKUU
  Anayo mamlaka ya kuongea chochote atakachoona kinafaa , kwa maslahi ya Taifa.
  "State of emergency" situation requiring immediate action.
   
 6. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #6
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Ukisikia kudandia hoja ndio huko. Ulikuwa huna ubunifu wa kujuwa yote hayo mpaka umsikie Kikwete? hapo ndipo unapotudhihirishia kuwa wewe ni dhaifu wa hoja.

  Uchukuwe hoja za mtu uzigeuzegeuze halafu uje humu na uende bungeni ukajidai hoja zako? Kijana naona umeishiwa kama Lema na Slaa.
   
 7. Q

  Q600 Member

  #7
  Jul 2, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Uyu mh.dhaifu anadai wa tz ni vilaza kiivo?? Data za mishaara ya mwaka 2000,ajui salafu yake aina thaman tena?? Na kai aribu yeye! Awape mishaara mizuri ma Dr.,so k ulia lia!
   
 8. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #8
  Jul 2, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Kuwa mpinzani maana yake siyo kupinga kila kitu.
   
 9. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #9
  Jul 2, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,816
  Likes Received: 1,353
  Trophy Points: 280
  On a serious note labda hizi siasa zetu sizielewi vizuri, kwengine kokote duniani upinzani ungekaa kimya tu kwenye hili sakata la madokta na kuwa wangaliaji wa mbali kulikoni kujiingiza kati.

  Kumbuka siasa ni dhamana ya kuongoza na kugawa rasilimali zilizopo kwa faida ya jamii, sasa wewe jamii inaumia hata kama madaktari wana argument huwezi kutokea mbele na ku-side na madokta. madokta wanamadai yao kwa serikali na jamii inahitaji huduma za madokta.

  Ukikurupuka na kuchagua ku-side na madokta ni sawa na kujiwekea political suicide kwenye issue at hand. wenzako watakuamishia mpira kwa wananchi nakusema unatetea madokta na unaamini wapo sawa wao kuwanyimwa matibabu kwa mujibu ya chama fualni. In case you forget your priority ni wananchi wengi kwanza, then groups.
   
 10. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #10
  Jul 2, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,196
  Likes Received: 1,977
  Trophy Points: 280
  Pambaf sasa walichokuwa wanasema kisiongelewe bungeni kwamba ni kuingilia muhimili mwingine ambao ni mahakama nini? Wakati dhaifu kaingilia hapo ndio hoja ilipo Pambaf wewe
   
 11. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #11
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Wewe rudi Shule ukajifunze kuandika kwanza! Kama umtanzania na lugha yako ya Taifa inakuchanganya, je ya nje ya Tz itakua vipi ?
  > Salafu = Sarafu
  > Mishaara = Mishahara
  > Kai aribu = Kaiharibu
  Cha kushangaza wewe tena unamwita Mkuu wa nchi "dhaifu" unawaita na Member wenzako vilaza !
  Wakati wewe hata Kiswahili kukiandika mtihani .
  Viazi.
  Usiparamie mijadala ikiwa hata kuandika issue !
   
 12. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #12
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  umedhihirisha kwamba bosi wako ni nape,unaangalia spelling badala ya content.kama tu bosi wako anavyotaka real ID za members badala ya ku-attack hoja ya mtu................mmedundaaaaaaaaaaa
   
 13. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #13
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  unaweza kuwa na hoja lakini si katika kila jambo,kukaa kimya usiwatetee watu au kukitetea kitu unachokiamini kwa kuogopa eti wananchi wataona umeside na madokta ni unafiki,na hii haiwezi kufanywa na mtu makini kama mnyika au any MP from cdm except shibuda.Naamini wananchi watataka hoja na si ni nani au nani anaside au hajaside na madokta au kundi lolote.............hakielimu eti?
   
 14. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #14
  Jul 2, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hii tabia ya kuwa eti dhaifu kasema kitu usijibu au kuchambua alichokisema kwa kuogopa kudandia hoja iko huko kwenu tu kwenye cocus ya magamba,na hata kama ni kudandia hoja shida iko wapi? watu wanadandia maneno aliyotoa yesu na manabii wengine kwenye biblia na allah kwenye quran itakuwa sembuse huyu dhaifu wenu.............utakuwa una brain miscarriege kama siyo pregnancy miscarriage...
   
 15. M

  Masabaja Senior Member

  #15
  Jul 2, 2012
  Joined: Mar 4, 2012
  Messages: 139
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nadhani utakuwa unachukua kaposho karefu maana kwa kumtetea DHAIFU si kwamba unafanya bure kwa jinsi ninavyokuona
   
 16. dosama

  dosama JF-Expert Member

  #16
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 25, 2010
  Messages: 786
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nakuja
   
 17. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #17
  Jul 2, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 841
  Likes Received: 203
  Trophy Points: 60
  kuwa chama tawala sio maana yake kupinga kila kitu!
   
 18. Safari_ni_Safari

  Safari_ni_Safari JF-Expert Member

  #18
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 22,446
  Likes Received: 5,833
  Trophy Points: 280
  Hiyo uliyoitaja siyo mihimili isipokuwa hii:
  1. SERIKALI
  2. BUNGE
  3. MAHAKAMA
   
 19. Bob Lee Swagger

  Bob Lee Swagger JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Binafsi naona unajichanganya tu. Unataka kutuaminisha fikra zako kuwa ndo zinazotokea "kwingineko duniani" maana hata kama yanatokea haimaanishi kuwa ni sahihi, sababu umeielezea mwenyewe hapo pa zambarau.

  Mnyika kaongea ulipo mzizi wa tatizo, UBABE na kutaka kuwaaminisha watu kuwa serikali IMEFANYA VYA KUTOSHA bila mjadala, kitu ambacho sio sahihi. Kwa nini wasiliachie bunge lijadili badala ya kutafuta huruma ya wananchi kama anavyofanya raisi kwenye hotuba zake!? kumbuka kuna kamati ilikua inafuatilia hili baada ya mgomo uliopita na hatujaona majibu yake na ni fedha za umma zilitumika hapo?!

  Umesema hapo pa kijani, na hiyo ni wajibu wa kila mwananchi japo utekelezaji unafanywa na serikali iliyopo madarakani hivyo kuhoji utekelezaji sio ku'take sides'

  Hakuna political suicide yeyote hapo, labda kama unaongea na wazee wa daresalama waliozoea ngonjera za JK, wengine wameamka na wanaelewa!
   
 20. proisra

  proisra JF-Expert Member

  #20
  Jul 2, 2012
  Joined: Jun 14, 2012
  Messages: 213
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  ========================================

  Hili jambo linazungumzika, iwe Bungeni au hata Ikulu kama alivyofanya JK. Kisingizio cha kwamba jambo liko mahakamani hakina mshiko (not tangible). :israel:
   
Loading...