Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

"Mimi kuanzia wiki jana nimekuwa mwanachama wa Chadema"

Yaani kuanzia wiki jana ndo unajifanya unaijua Chadema wewe prof. uliyefulia? Unaijua Chadema kuliko Dr. Slaa wewe? Njaa tu inakusumbua hakuna lolote na ungekuwa bado Mlimani sidhani kama ungekuwa unahangaika hivi!
 
PhD holder anapimwa kwa uwezo wake wa kuchambua mambo siyo kwa ushabiki wa kipumbavu kama wa mwendawazimu Azaveli lwaitama. Mzee mzima anakosa busara anaongea pumba.shenzi sana.

Soma tena amejibu issues.
 
“Let me define a leader. He must have vision and passion and not be afraid of any problem. Instead, he should know how to defeat it. Most importantly, he must work with integrity.”
― A. P. J. Abdul Kalam.

Je Lowassa na washabiki wa "bora mabadiliko" wanajitathmini vipi na sifa hii ya kiongozi!
 
masahihisho: lengo ni kuwapotezea muda CHADEMA na UKAWA wasipate kujipanga vema na kampeni na uchaguzi. huyu atakuwa amekuwa 'corrupt' na CCM.

Kuna dalili zote za kitu kidogo
 
Soma tena amejibu issues.
Dr. Slaa ametoa changamoto kwa Lowassa na Sumaye wazijibu hoja zake sio wajibiwe na mtu mwingine.. Personal and Integrity Challenge!!! They have to come out clean kama kweli wanataka kupanda treni ya mabadiliko ya kweli
 
Kusaliti umma ni kumsaliti Mungu, hakika macho na maskio yake sio mabovu asinyoshe mkono kuwakomboa watu wake
 
Babu Slaa apuuzwe, amegeuka mchumia tumbo! Ghafla amegeuka kuwa kipenzi cha TBC1, na wa gazeti la Uhuru! Hapo bado hujaelewa tu anaowatumikia?
Tunavyoongea Yuko majuu akila matunda ya jasho lake alilovuja wakati wa hotuba yake na waandishi wa habari!

Ukiona shetani anakupenda, ujue umetimiza mapenzi yake
 
"Mimi kuanzia wiki jana nimekuwa mwanachama wa Chadema"

Yaani kuanzia wiki jana ndo unajifanya unaijua Chadema wewe prof. uliyefulia? Unaijua Chadema kuliko Dr. Slaa wewe? Njaa tu inakusumbua hakuna lolote na ungekuwa bado Mlimani sidhani kama ungekuwa unahangaika hivi!

Hahaha njaa tena
 
Umezungumzia kipaumbele cha Lowassa kuwa ni Elimux3! Huyu huyu Lowassa mwaka jana alisikika akisema kuwa Vijana ni bomu linalosubiri kulipuka!Leo hii hazungumzii chochote kuhusu bomu hili la vijana. Vijana wengi hivi sasa ni wale waliomaliza Vyuo mbalimbali lakini hawana kazi. Sasa akisema Elimux3 ndiyo kipaumbele chake huoni atazidi kutengeneza wasomi ambao hawana kazi kama Nigeria? Tunafahamu mataperi wakubwa wa Nigeria ni wale waliosoma sana lakini hawana ajira! El nitamuona wa maana kama atazungumzia bomu la vijana ili lisije kulipuka kama anavyodai!
 
Mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu Zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu Dr Slaa sasa...wote ni WASALITI wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha CCM madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa Chadema...kadi nilinunua Dar es Salaam makao makuu ya Chadema DSM na nilikabidhiwa na mwanangu Benson Kigaila Dodoma , mji mkuu wa Tanania , Jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Benson Kigaila ya kuwania Ubunge Doadoma Mjini... Benson Kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha Chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee Mtei na mwanagu Mbowe ambao, kama Ndg Lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia Watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha Prof Mohamed Babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....Tena Lowasa ndani ya UKAWA si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya CCM ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za Tanganyika na Zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na Friends of Slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji FRIENDS OF UKAWA NO more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na CCM ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa CCM madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya Rais wa Muungano na kuwepo Muungano wa serikali tatu...

Dr Slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu Zito na Prof Mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha CCM another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama

Hivi huwa mnaenda shule kufanya nini?? Au hvyo vichwa ni vya kufigia nywele tu?? Dr, cjui profesor, cjui hata umeandika nini,

Hvi kuwa mwanachama wa cdm ndyo hujui hata ajenda kuu ni nini??

Hoja ni je alichosema dr ni sahihi au si sahihi?? Kubali au kataa..

Nawasiwasi na udr wako au uprofesooo..
 
Slaaaaa kapuliziwa dawa,leo akiulizwa alichokisema jana hawezi kukumbuka,amejikaanga kwa mafuta yake mwenyewe.

Ili ujue amejikaanga kweli kweli alidai kuwa alikuwa akitaabika na mchumba wake Mshumbusi wakila mihogo na maharage akisahau tunajua kuwa alikuwa akifuata mishahara yake yote chadema bila kukosa wala kuchelewa. Alikuwa bado akitumia gari la chadema na walinzi wa chadema muda wote huo. Hakuelewa kuwa inteligensia ya chadema ilikuwa inamfuatilia kila alichokuwa akikifanya yeye na mchumba wake na kugundua walifichwa hoteli ya kimataifa ngorongoro kwa muda kabla ya kupelekwa south Africa na kuwekwa hoteli yenye hadhi ya nyota tano kabla ya kurudishwa tena nchini na kufikia hoteli ya hadhi katikati ya jiji la Dar na siku mbili baadae kukodishiwa ukumbi wa mkutano na waandishi na kuonyeshwa na tv tatu na kesho yake kusafiri kuelekea Marekani. Sasa vyote hivyo vililipwa kwa hela ya kula mihogo na maharage kama anavyojaribu kutuaminisha? Hivi nae akili yake imerudi kulekule kwa wale wanaoamini hadi leo kuwa akili za Watanzania ni zile zile za miaka ya uhuru na bado ni za kipumbavu na kilofa?Ndio aliyokuwa akifundishwa na kuaminishwa hivyo alikokuwa akizungushwa na kulazwa na kuambiwa atakayoyasema kwenye mkutano? Hizo hela za kula mihogo na maharage zilimwezesha na kununua tiketi yake na Mushumbusi kwenda Marekani na wakaishi? Uchamungu wake upo wapi? Hivi siku ya mkutano hotelini pale hakujua Mwakyembe alionekana kwenye chumba na baadhi ya wanausalama wa taifa?Hivi usaliti wake kwa chadema unatoutiana vipi na aliomtwisha Zitto na wenzie?Hivi ni lini kadinali Pengo alikasimisha madaraka yake kwake kukemea mapadre wake kwa masuala ya rushwa?Hivi kuhusisha viongozi wetu wa dini na masuala ya rushwa na kesho yake kuikimbia nchi na mchumba wako unataka kutuachia uchaguzi wa namna gani? NAOMBA WANACHAMA NA WAPENZI WA UKAWA NA MAGEUZI KWA UJUMLA TUMPUUZE HUYU NA KUMUEPUKA. HIVYO HIVYO WANANCHI NA VIONGOZI WETU WA DINI ZOTE.
 
Siamini nchi hii imefika hapa, hata wasomi sasa wanajitoa ufaahamu na kupongeza wakosa maadili....

No wonder kila mtanzania ni mfujaji na mkosa maadili kwani ukiwa muadilifu hata sehemu ya kazi utabezwa na kudharauliwa, ili hali mwenzako anaheshimika.

....SHAME ON YOU....
 
Dr.Lwaitama ni miongoni mwa Wasomi wachache wa TZ wanaotumia vichwa kuwaza ....well altered Mwl wang

Ni ajabu. Haya Ma daktari yanayotufundisha kwenye vyuo yanatakiwa kupimwa akili. Sasa watu wanamshabikia hivi kaandika nini? Mbona haja address hoja hata moja ya Slaa?. Tutawapa taabu sana wajukuu zetu ya kuchimbua makaburi yetu ili wapime bongo zetu kama zilikuwa sawa au zilikuwa kwenda Evolution Process. This msomi is another failure
 
Ni Mungu yupi unae mrejea hapa? Msimuhusishe Mungu katika mambo yenu ya kifidadi na ya kishirikina. Kama unafuata mkumbo afadhali. Lakini si bure mmelogwa nyinyi.

MPEPA
Kunamiungu wangapi unao wafahamu binafsi namtaja mungu wa ELIA NA YAKOBO ww ulidhani mungu yupi??
n
Ni weke wazi kwenye hii sentensi yako UFISADI NA USHIRIKINA ,epia unaniambia kama nafuata mkumbo afadhali maana yake nni ww ninani unifanye nisitoe maoni yangu?? ww ni nani hata kubisha imani yangu??
Kama ww ni mtakatifu kwamfano UNAZUNGUMZIAGE KURWAGWA pasi na shaka humwamini mungu aliye juu mbinguni.
 
Back
Top Bottom