Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Maneno yako yanaweza kuwa na mbolea kiasi, lakini kama wangekuwa wema hivyo tusingesikia watu /wafanyakazi wao wakawalalamikia. Mfano mdogo tu ni huu wa karibuni wa madreva na waajiri wao! Sikiliza wanavyohadithia kunyanyaswa kwao na matajiri wao. Tajiri anachojali yeye ni kutengeneza faida kubwa sana kwa kumyonya mtumishi wake ambaye ni maskini. Hapa ndiyo maana Mwl. Nyerere aliwaambia watanzania kuwa UBEPARI NI UNYAMA kama unakumbua!

Sometimes: Ndugu yangu ndio maanaa Sera za Chadema na Ukawa kipaumbele cha kwanza Elimu,Cha pili Elimu na cha Tatu Elimu.Hivi vitu kwa mwanadamu kulalamika avikuanza leo toke kuumbwa kwa ulimwengu mwanadamu si mtu wa kuridhika.hata umpatie nini mwanadamu aridhiki.hilo linaeleweka..turudi kwenye point.tunaposema Elimu sio tuu itolewe elimu ya Sayansi na kadhalika..ni elimu ya nyanja zote..mpaka elimu ya uelewa wa Haki zetu.usipojua haki zako za msingi hata uwe Prof..wewe utakuwa bure tuu.Sisi watanzania elimu ndio inatusumbua ..matokeo yake tunaanza kuwachukia watu wenye kipato tunawaona sio binadamu wanaoweza kutujali sisi maskini,,sio kweli maana mchango mkubwa wa kumuokoa maskini katika dunia hii unadhaminiwa na Matajiri.watu wenye pesa.,hilo lipo wazi,,unaposema unyanyasaji wa wafanyakazi .ndio Sawa hupo huo unyanyasaji .lakini tukirudi pale pale Elimu itamapokuwa nzuri watu wakajitambua wakatambua haki zao.huo unyanyaswaji utaisha,maana utawekwa mfumo mzuri kwa sisi kabla ya kupata kazi utapatiwa mkataba utausoma vizuri mkataba usiporidhika nao basi,ukiridhika utasaini kwa makubaliano na sheria na haki zako zote zitafuatwa kutokana na ajira hiyo.hilo litakapokuwepo Nchi utoona unyanyasaji Wa tajiri kwa maskini ,viwandani au kwenye sekta yoyote hile.Nafikiri ndugu yangu inaweza kuwa umewahi kutembea zaidi nchi zilizoendelea ,utakuta mtu anaweza kuwa na vitu vya thamani kuliko boss wake aliyemwajiri,,lkn kwa Tanzania aiwezekani utaambiwa tuu wewe ni mwizi boss wako anaendesha baiskeli wewe unaendesha gari..tuache fikra hizo..za matabaka .ukiwa mbinafsi ni mbinafsi tuu atojalisha wewe Maskini au Tajiri..Nyerere ni binadamu kama mimi na wewe..ana nyongo sio malaika.hivyo basi sio alichokifanya au kusema basi yupo sahihi..watu wanaamka sasa hivi..atuwezi kuinua hii Nchi kama tutamfikiria Nyerere,watu tunaenda mbele Future.hili tuweze kwenda na Dunia ya sasa nyinyi mnaturudisha miaka 50 ya ujamaa,,Mataifa yote ya sera za ujamaa sasa hivi Chali.Chagua Lowasa na Ukawa ujue haki zako na uwezi kuzihoji ukizikosa ,,Umeme unakatwa katwa hovyo,hospital hovyo unashindwa kuhoji maana haki zetu atuzijui kwa sababu elimu mbovu.Serikali ni wajibu wake kutoa huduma muhimu kwa raia wake.Maji,barabara,umeme,elimu,usalama wa raia na mali zao,huduma ya afya,na mengine.Hila pia serikali sio wajibu wake kumfanya mtu awe tajiri.,ukipata huduma hizo.hapo juu utokuwa na sababu ya kumuangalia tajiri kwa jicho baya..utajiri ni nguvu binafsi..Siku njema ndugu yangu.
 
Poleni sana mlioweka matimaini kwa Lowassa. Hata hivyo Watanzania hatuwezi kukosea kumpa nchi mtu kama lowassa, haaminiki na hatari sana kwa maisha yetu Watanzania

Kama mpaka leo hujui wanaohatarisha maisha yako pole, lakini usimsingizie EL.
 
Mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu Zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu Dr Slaa sasa...wote ni WASALITI wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha CCM madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa Chadema...kadi nilinunua Dar es Salaam makao makuu ya Chadema DSM na nilikabidhiwa na mwanangu Benson Kigaila Dodoma , mji mkuu wa Tanania , Jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Benson Kigaila ya kuwania Ubunge Doadoma Mjini... Benson Kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha Chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee Mtei na mwanagu Mbowe ambao, kama Ndg Lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia Watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha Prof Mohamed Babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....Tena Lowasa ndani ya UKAWA si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya CCM ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za Tanganyika na Zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na Friends of Slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji FRIENDS OF UKAWA NO more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na CCM ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa CCM madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya Rais wa Muungano na kuwepo Muungano wa serikali tatu...

Dr Slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu Zito na Prof Mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha CCM another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama

Yaani CCM iondolewe kwa gharama zozote zile!! hapana jamani...
 
Dar vile vivazi vya kijani havionekani kabisa hasa katikati ya mji, oh CCM R I P 2015
 
Sikutarajia hata kidogo kwa Lwaitama kuanza kumsifia mtu ambaye ni kielelezo cha ufisad katika nchi yetu, ni kweli tunataka kuitoa ccm madarakani lkn si kwa kumfanya mtu ambaye si mwadilifu awe RAIS wa NCH yetu.
 
Sikutarajia hata kidogo kwa Lwaitama kuanza kumsifia mtu ambaye ni kielelezo cha ufisad katika nchi yetu, ni kweli tunataka kuitoa ccm madarakani lkn si kwa kumfanya mtu ambaye si mwadilifu awe RAIS wa NCH yetu.

Kwako wewe nani mwadilifu asili mia mia kati ya wagombea wote. Jana tuu, mgombea ccm anawadanganya wana Mtwara kwamba serekali imejenga kiwanda cha Dangote. Si uongo huo.? Tunajua kwamba pana tuhuma za ufisadi wa lowassa, yaani tuhuma. Mbona wengi wapo ccm wale kumi? Ndani ya chama tawala, ndo hao wanao mtaka magufuli aendele kuwalea? Zoti hizi ni mbwembwe zakuunda mahakama ya mafisadi, hatafanya chochote. Tatizo ni mfumo, tusidanganyane hapa. Sasa nibora mfumo wote uondoke tuanze upya na wengine.
 
KUTUMIA LUGHA HASI NA UKAKASI NI SAWA NA KUTWANGA MAJI KWENYE KINU! ni reflection ya haiba yako dhaifu!! HAKUPUNGIUZII LWAITAMA CHOCHOTE Wala kumvua Phd yake; Nani kasema wewe hapa umeonyesha uwezo kabambe wa kufikiri na kuchambua lolote kama sio block minded!?



PhD holder anapimwa kwa uwezo wake wa kuchambua mambo siyo kwa ushabiki wa kipumbavu kama wa mwendawazimu Azaveli lwaitama. Mzee mzima anakosa busara anaongea pumba.shenzi sana.
 
Bukanga

Dr Gani Hajui Hata Kuvaa Na Hajipendi? Huyo Lwaitama Alichobakiza Tu Ni Kuokota Makopo Kwani Ana Kila Vimelea Vya Mtu Aliyechanganyikiwa. Labda Sasa Amehamia CHADEMA + UKAWA Ataacha Kunywa Gongo Na Kuunguza Ule Mdomo Wake Ambao Muda Wote Lips Zake Ni Nyekundu Tu. Hivi Ni Kwanini CHADEMA + UKAWA Mnapenda Sana Kukumbatia Mizinga Ya Nyuki Namna Hii?

Pole sana, hivi hoja
yako ni IPI?
 
Last edited by a moderator:
Du yaani matajiri wawasaidie watanzania kuwa matajiri!!hii kali
 
Fisadi ni fisadi tu hafai kwenda ikulu

Hata hao walioko ikulu kwa sasa mbona nao ni mafisadi tu? Au Ikulu ni ya ccm tu. Sasa mmeshikwa kisawasawa hamna jinsi na mbinu zenu chafu zitakazo sababisha machafuko.
 
Siamini Dr Lwaitama anaweza kukimbia hoja kwa kutoa maelezo mepesi yasiyojibu hoja hata moja ya Dr Slaa. Nitaendelea kumheshimu mpaka atakapothibitisha yeye mwenyewe kama kweli ameamua kuzikwepa hoja za Dr Slaa kwa kutoa maelezo mepesi kiasi hicho.

Lengo la Dr Slaa ni kukwamisha safari ya mabadiliko. Ndio maana ya kukimbia na kujiunga na team ya campaign ya wasiotaka mabadiliko kwa wananchi TZ. Kujibu hoja moja moja ya Dr Slaa ni kukubali kuingia ktk mipasho na kuhamishwa kutoka agenda kuu ya kuleta mabadiliko/maendeleo ya kweli. Amen
 
Babu Slaa apuuzwe, amegeuka mchumia tumbo! Ghafla amegeuka kuwa kipenzi cha TBC1, na wa gazeti la Uhuru! Hapo bado hujaelewa tu anaowatumikia?
Tunavyoongea Yuko majuu akila matunda ya jasho lake alilovuja wakati wa hotuba yake na waandishi wa habari!

Na clip alivyoingia serena hotel hujaiona na dada alie eleza kila kitu wakati wameingia na mwakembe serena.
 
Back
Top Bottom