Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu dr slaa sasa...wote ni wasaliti wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha ccm madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa chadema...kadi nilinunua dar es salaam makao makuu ya chadema dsm na nilikabidhiwa na mwanangu benson kigaila dodoma , mji mkuu wa tanania , jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya benson kigaila ya kuwania ubunge doadoma mjini... Benson kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee mtei na mwanagu mbowe ambao, kama ndg lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha prof mohamed babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....tena lowasa ndani ya ukawa si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya ccm ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za tanganyika na zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na friends of slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji friends of ukawa no more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na ccm ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa ccm madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya rais wa muungano na kuwepo muungano wa serikali tatu...

Dr slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu zito na prof mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha ccm another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama
you my true hero...god bless you sir.
 
Mtu imara bila taasisi imara ni ujinga pia ,kaungane na Mh Wasira katika utabiri maana inaonekana bado unayo ilimu ya mkoloni kichwani mwako.Unafikiri unavyofikiri ndio mwisho wa upeo wa watu wote.

Siwezi kuendelea na mtu ambae hana reasoning capacity for transcendent ideas. Take care.
 
An intellectual message...we don hv any other options than taking n digest them not only in our powerful minds but again in our hearts flawlesly...TUTAMPIGIA KURA EDWARD LOWASSA.
 
Ameegemea upande gani kwa mtazamo wako ?

Hivi huoni kuwa kitendo cha yeye kujitambulisha kuwa ni mwanachadema tayari ameegemea mawazo ya uchadema tu?

Falsafa inapingana na itikadi ambayo ni moja ya nguzo ya chama chochote cha siasa, ukiishajiunga na chama cha siasa unakuwa umeuza uhuru wa kufikiri, sasa mwanafalsafa gani ambaye yupo tayari kuwekewa mipaka ya kusema anachokiamini?
 
Utajiri ama tuseme ustawi kwa jamii nzima hautokani wa wananchi kugawiwa pesa (rejea milioni 50 kwa kila kijiji zinazo ahidiwa na Makufuli au mabilioni ya Kikwete ya sikumbuki mwaka gani lakini ni kati ya 2005-2015), bali jinsi ya ku-manage na ku-organize rasilimali zilizomo nchini ikiwa ni pamoja na raslimali watu kama wewe ziweze kunufaisha jamii nzima. Hapa hatuzungumzii ubilionea au umilionea, bali kupata huduma na mahitaji yote ya msingi kwa binadamu yaliyo bora. Kama ni elimu kwa wote, iwe elimu bora, kama ni maji safi yawe maji safi na salama na upatikanaji bora kwa wote, kama ni .. kila kitu kipatikane kwa wote na kiwe bora. Huo ndio utajiri wa jamii. Mwanafalsafa Lwaitama yuko sahihi kabisa. CHAGUA MABADILIKO, CHAGUA UKAWA, CHAGUA LOWASSA.

Eti mwanafalsafa lwaitama! watu mna vichwa vitupu kabisa. Kama wanafalsafa wetu ndio hawa wakina lwaitama basi tuhesabu tu kuwa hatuna wanafalsafa.

Hayo maneno mengine nimeshindwa kukujibu maana najua hutanielewa.
 
Dr Slaa pole sn,lkn tambua kuwa shetani anauwezo wa kupinga jambo jema kupitia vinywa vya wanadamu lkn shauri la Bwana husimama palepale!!!!
 
Naunga mkono hoja.Toka lini tajiri akawa na urafiki na maskini? Ni kama paka kuvaa tasbihi/rozali ya dagaa.

Sometimes: ukisema hivyo unakosea,,Ukiangalia tuu kwa haraka haraka,hao matajiri mnaosema awatoweza kumsaidia maskini,Ndio watu wanaomiliki viwanda,na ni wafanyabiashara wakubwa sana duniani,,Mfano mdogo tuu .Mtu tajiri atakuwa na kiwanda cha saruji.,katika kile kiwanda watajiriwa watu.katika nyadhifa tofauti tofauti.,hata vibarua pia..Hapo katika watu waliowaajiriwa zitakuja jitihada binafsi za kila mmoja wao,kuna watakaofanya kazi na wakipata mshahara na kuwekeza katika biashara..,kilimo.nk.je hao wafanyakazi wakifanikiwa.na wao mbeleni kuwa matajiri baada ya kuajiriwa na tajiri wakatumia jitihada zao pia .wakafika hapo walipo.Mimi nafikiri tunaweza kusema Tajiri nafasi yake kubwa sana ya kumsaidia maskini afanikiwe kimaisha kuliko Maskini kumsaidia maskini mwenzake. Maskini kwa maskini yataishia majungu tuu ,yaa kuanza kugombania hata chakula,,Ni vizuri sana kwa Nchi kama za kwetu likaangalia hilo..najua wengi maskini wanatumia gear hiyo ya Kutaka mtu wa kipato cha chini hili walete Ujamaa na kiushikaji kupeana madaraka,
 
Well said Lwaitama. MABADILIKO KWANZA, Sasa train ya MABADILIKO ipo njiani haitapisha mtu yeyote ni mwendo mdundo hadi MAGOGONI

sio ili mradi tu mabadiliko tunataka mabadiliko bora,kwa maneno yako inaonyesha kwako ni sawa tu kutoa bunduki na kuingiza rungu eti ili mradi mabadiliko
 
Kwanini wasisaidie hao maskini kwa pesa zao binafsi bila kusubiri kwenda ikulu? kama wao waliweza kuwa matajiri kwanini wengine wasiweze kuupata? hoja dhaifu kabisa kwa mtu anayejiita msomi kuwa na fikra duni kuwa kipimo cha ubora wa maisha ni utajiri! nani amewaambia kuwa watanzania wanataka kuwa matajiri? ina maana watu hao wasipotimiza ndoto zao za urais hawatawasaidia watanzania kuwa matajiri? Lwaitama atuambie, hadi sasa hao matajiri wamewasaidia maskini wangapi kuwa matajiri.



umelilitendea haki jina lako
 
MUNGU yupo PAMOJA NASI WATANZANIA KUJIKOMBOA TUJITIE MOYO TUTAFIKA

Ni Mungu yupi unae mrejea hapa? Msimuhusishe Mungu katika mambo yenu ya kifidadi na ya kishirikina. Kama unafuata mkumbo afadhali. Lakini si bure mmelogwa nyinyi.
 
Yaani tajiri amsaidie masikini awe tajiri kama yeye.?

Je kipofu aweza kumuongoza kipofu mwenzake?

Mkuu naona bado umejawa mawazo ya Kambarage aliyewaaminisha Watanganyika kuwa wao ni watu maskini na watakombolewa na maskini mwenzao...

Kauli kama hizo ndio zimesababisha mabepari na makabaila kupora mali na ardhi ya Watanzania miaka nenda miaka rudi...
 
Dr Slaa pole sn,lkn tambua kuwa shetani anauwezo wa kupinga jambo jema kupitia vinywa vya wanadamu lkn shauri la Bwana husimama palepale!!!!

Shauri la Bwana gani?
Unadhani uko kanisani hapa. Huyo Bwana wako atakuadhibu kwa kumchanganya na mipango dhalimu ya wanadamu
 
Bukanga

Dr Gani Hajui Hata Kuvaa Na Hajipendi? Huyo Lwaitama Alichobakiza Tu Ni Kuokota Makopo Kwani Ana Kila Vimelea Vya Mtu Aliyechanganyikiwa. Labda Sasa Amehamia CHADEMA + UKAWA Ataacha Kunywa Gongo Na Kuunguza Ule Mdomo Wake Ambao Muda Wote Lips Zake Ni Nyekundu Tu. Hivi Ni Kwanini CHADEMA + UKAWA Mnapenda Sana Kukumbatia Mizinga Ya Nyuki Namna Hii?

Ha ha ha.
Tulikuwa tunamwita Mwl Lwaitama "a powder keg". Ni baruti inayolipuka na ni hatari kwa mwenye baruti.
Sasa mwenye baruti ni Chadema. You have a powder keg in your hands.
 
Last edited by a moderator:
Mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu Zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu Dr Slaa sasa...wote ni WASALITI wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha CCM madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa Chadema...kadi nilinunua Dar es Salaam makao makuu ya Chadema DSM na nilikabidhiwa na mwanangu Benson Kigaila Dodoma , mji mkuu wa Tanania , Jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Benson Kigaila ya kuwania Ubunge Doadoma Mjini... Benson Kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha Chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee Mtei na mwanagu Mbowe ambao, kama Ndg Lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia Watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha Prof Mohamed Babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....Tena Lowasa ndani ya UKAWA si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya CCM ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za Tanganyika na Zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na Friends of Slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji FRIENDS OF UKAWA NO more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na CCM ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa CCM madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya Rais wa Muungano na kuwepo Muungano wa serikali tatu...

Dr Slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu Zito na Prof Mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha CCM another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama
Hapa ndio utajua kwanini siasa ni mchezo mchafu..
 
Back
Top Bottom