Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Maoni ya Dr. Lwaitama Kuhusu Hotuba ya Dr. Slaa...

Mbaya zaidi, analeta cheap politics.

Hajajibu hata hoja moja ya Dk. Slaa.

Hoja za Dk. Slaa huwezi kuzijibu kwa kutumia cheap politics.

Eti anasema Dk. Slaa ni msaliti. Hivi anafahamu maana ya neno usaliti katika mantiki ya Lowassa, CHADEMA na Dk. Slaa?

Chadema ina upungufu mmoja unaokizuia kuwa chama chenye nguvu kuliko vyote Afrika.
Hawakubali kukosolewa, na sera yao ya utawala wa ndani ni 'demokrasia ya mabavu'
 
Kila siku Raisi wenu kiguu na njia akitafuta msaada, kwani huwa anakwenda nchi masikini?
Safari hii wananchi tupo mnadani, hatuna pa kujishikilia.

Wasomi wametuuza, waandishi na wachambuzi ndio kama hivyo wapo kutumikia.

Tunasubiri kudra za Mwenyezi Mungu kusikika mawazo yetu.
 
Mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu Zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu Dr Slaa sasa...wote ni WASALITI wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha CCM madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa Chadema...kadi nilinunua Dar es Salaam makao makuu ya Chadema DSM na nilikabidhiwa na mwanangu Benson Kigaila Dodoma , mji mkuu wa Tanania , Jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Benson Kigaila ya kuwania Ubunge Doadoma Mjini... Benson Kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha Chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee Mtei na mwanagu Mbowe ambao, kama Ndg Lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia Watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha Prof Mohamed Babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....Tena Lowasa ndani ya UKAWA si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya CCM ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za Tanganyika na Zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na Friends of Slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji FRIENDS OF UKAWA NO more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na CCM ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa CCM madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya Rais wa Muungano na kuwepo Muungano wa serikali tatu...

Dr Slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu Zito na Prof Mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha CCM another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama

Mwalimu Lwaitama hajajibu hoja hata moja ya Dr. Silaa.

Silaa amesema wazi kuwa Mbowe na Lowassa sio wazalendo na wamewahadaa Watanzania.

Dr. Silaa ametoa ushahidi na vielelezo vinayoweka misingi ya hoja zake. Kaanza kwa kuupinga utetezi wa Lowassa dhidi ya richmond, kisha mchakato wa Lowassa kuhamia Chadema na Tatu..kaonyesha kuwa viongozi wa Chadema ni walaghai na wamewadanganya wanachama wao mara kadhaa kwenye mambo yenye umuhimu mkubwa.
Likiwemo kusema uongo kuhusu vikao, kuhadaa umma kuwa Silaa bado ni kiongozi wao etc.

Mwl Lwaitama hajajibu tuhuma hizi hata moja, na hajaweka msingi wowote wa dhana anayosimamia. Silaa kaweka dhana na ushahidi wake. Ilikuwa ni wakati wa kumuumbua Silaa kuwa kapotoka na kasema uongo.

Lwaitama kajuinga na lile kundi ambalo ukiikosoa Chadema hata katika ukweli, na kwa nia njema utajibiwa majibu matatu 1. Wewe ni Msaliti, 2. Wewe ni Gamba 3. Unatumiwa na Magamba. Hapo ndo mwisho wake. Rudia usomi wako fuata mfano wa wasomi wenzio Shivji, Ngugi na Soyinka
 
Inasikitisha kuona jinsi Watanzania wachache walivyo athirika kwa ushabiki na mahaba yaliyopitiliza kwa mtu kiasi cha kutokuona hata kama wanaangalia au kuto kusikia japo wanasikiliza!! Kwao sasa hivi anayesema ukweli ni yule anayeongea lugha ambayo Masikio yao yanataka kusikia kinyume na hapo watatukanwa na kuvutwa majina yote machafu na kwamba wametumwa na CCM. Leo ati Slaa kusimamia anayoyaamini ambayo ndiyo anayahubiri siku zote katumwa na CCM ...... It is a shame. Mungu aturehemu
 
Chadema ina upungufu mmoja unaokizuia kuwa chama chenye nguvu kuliko vyote Afrika.
Hawakubali kukosolewa, na sera yao ya utawala wa ndani ni 'demokrasia ya mabavu'

Kwa jinsi ambavyo utawala huu ulivyochanganyikiwa baada ya wapinzani kuungana sidhani kama Chadema kingalikuwako,kwa haya uliyoyasema ambayo ni kinyume na katiba ya nchi na ni kinyume na katiba ya Chadema basi msajili wa vyama nchini angalikuwa ameshaifutilia mbali Chadema..
 
Watanzania wengi tumeshaamua kuwa tutamchagua lowassa kuwa rais na amiri jeshi mkuu wa jmt.
 
Inasikitisha kuona jinsi Watanzania wachache walivyo athirika kwa ushabiki na mahaba yaliyopitiliza kwa mtu kiasi cha kutokuona hata kama wanaangalia au kuto kusikia japo wanasikiliza!! Kwao sasa hivi anayesema ukweli ni yule anayeongea lugha ambayo Masikio yao yanataka kusikia kinyume na hapo watatukanwa na kuvutwa majina yote machafu na kwamba wametumwa na CCM. Leo ati Slaa kusimamia anayoyaamini ambayo ndiyo anayahubiri siku zote katumwa na CCM ...... It is a shame. Mungu aturehemu

Katika mambo yaliomshushia hadhi Dkt Slaa ni kauli yake kuwa Chadema walisomba watu na malori jangwani kama ilivyo tabia ya ccm...Hii ni kauli mbovu sana na inaacha mashaka kwa kile anachokisimamia.

Pia matukio yaliofuatia bàda ya hapo pia yalituachia shaka kama wananchi tunaopima mambo sio kusikiliza jambo tu kama kasuku.Prf Lipumba alipojiuzulu hatukuona nguvu kubwa ikitumika ktk kupata taarifa ile.Nilistuka sana TBC kurudia hotuba ya Dkt Slaa wakati ya Lipumba hata live yenyewe haikuwapo....Tunajua Slaa alikuwa silaha kubwa ya mwisho kutumika na utawala huu...

Tunawangoja kwa hamu hapo Oct 25 tutafahamiana tu kama sie ni malofa au wapumbavu.
 
Poleni Wahanga wa Mahaba... Mmepofushwa hata uwezo wa katafakari haupo tena......!!!

Wewe unaendeleza tu matusi ambayo ccm wanatutukana wananchi,wakati umeshafika mtaondoka tu na matusi yenu..
 
Hawa ndio wasomi wanaojielewa sio sawa na Dr. Bana.
Juzi alihojiwa na EATV anajiuma uma haeleweki.
 
Mimi nimesikitishwa na kuhuzunishwa mno na hotuba ya dr. Slaa jana...kama nilivyosema kuhusu mwanangu Zito hapo nyuma na sema hivyo hivyo kwa rafiki yangu Dr Slaa sasa...wote ni WASALITI wa vuguvugu la uma la kukiondoa chama dola cha CCM madarakani...

Mimi kuanzia wiki iliyopita ni mwana chama wa Chadema...kadi nilinunua Dar es Salaam makao makuu ya Chadema DSM na nilikabidhiwa na mwanangu Benson Kigaila Dodoma , mji mkuu wa Tanania , Jumapili iliyopita wakati wa ufunguzi wa kampeni ya Benson Kigaila ya kuwania Ubunge Doadoma Mjini... Benson Kigaila ni kati ya wajamaa wengi tu ndani ya chama cha kibepari cha mrengo wa kati cha Chadema kilichoanzishwa na matajiri kama mzee Mtei na mwanagu Mbowe ambao, kama Ndg Lowasa , ni wazalendo matajiri wanaochukia umasikini na wangetamani kuwasaidia Watanzania wengi iwezekanavyo kuwa matajiri...

Inanikumbusha Prof Mohamed Babu mwaka 1995 alipotoa kauli mbiu ya let people be rich....Tena Lowasa ndani ya UKAWA si rahisi awe dikteita kama ambavyo angekuwa ndani ya CCM ..walau tutapata muungano wa serikali tatu na tuanzisha mchakato katiba upya ikiwa ni pamoja na kuanzisha mchakato wa katiba za nchi washirika za Tanganyika na Zanzibar....

Mwaka 2010 kuwepo na Friends of Slaa ilikuwa muafaka ...leo tunaitaji FRIENDS OF UKAWA NO more need to be neutral......sasa ni lazima kuunganisha nguvu zote za kisiasa toka vyama vyote pamoja na CCM ..kuunganisha wote wenye kukiri kwa sababu zao mabalimbali kuwa wanajiunga na vuguvugu la wenye kiu ya kuondoa CCM madarakani na kupata ukombozi awamu ya pili chini ya katiba ya wananchi inayo lenga kupunguza madaraka ya Rais wa Muungano na kuwepo Muungano wa serikali tatu...

Dr Slaa, kama ilivyo kuwa kwa wanangu Zito na Prof Mkumbo historia itawahukumu inavyostahiki kwa kukipa chama cha CCM another lease of life beyond its expiry date...
Mwl. Lwaitama

Poleni sana mlioweka matimaini kwa Lowassa. Hata hivyo Watanzania hatuwezi kukosea kumpa nchi mtu kama lowassa, haaminiki na hatari sana kwa maisha yetu Watanzania
 
Tatizo umekariri na haukuwa ukitaka kujifunza ,unaamini tu bila ya kufikiri na upande wa pili na ni kama vile unaamini muuaji hawezi kuwa na huruma ataendelea kuua kila siku .
Haueleweki kijana! Kiswahili nacho ni kigumu pia.
 
Sometimes: ukisema hivyo unakosea,,Ukiangalia tuu kwa haraka haraka,hao matajiri mnaosema awatoweza kumsaidia maskini,Ndio watu wanaomiliki viwanda,na ni wafanyabiashara wakubwa sana duniani,,Mfano mdogo tuu .Mtu tajiri atakuwa na kiwanda cha saruji.,katika kile kiwanda watajiriwa watu.katika nyadhifa tofauti tofauti.,hata vibarua pia..Hapo katika watu waliowaajiriwa zitakuja jitihada binafsi za kila mmoja wao,kuna watakaofanya kazi na wakipata mshahara na kuwekeza katika biashara..,kilimo.nk.je hao wafanyakazi wakifanikiwa.na wao mbeleni kuwa matajiri baada ya kuajiriwa na tajiri wakatumia jitihada zao pia .wakafika hapo walipo.Mimi nafikiri tunaweza kusema Tajiri nafasi yake kubwa sana ya kumsaidia maskini afanikiwe kimaisha kuliko Maskini kumsaidia maskini mwenzake. Maskini kwa maskini yataishia majungu tuu ,yaa kuanza kugombania hata chakula,,Ni vizuri sana kwa Nchi kama za kwetu likaangalia hilo..najua wengi maskini wanatumia gear hiyo ya Kutaka mtu wa kipato cha chini hili walete Ujamaa na kiushikaji kupeana madaraka,
Maneno yako yanaweza kuwa na mbolea kiasi, lakini kama wangekuwa wema hivyo tusingesikia watu /wafanyakazi wao wakawalalamikia. Mfano mdogo tu ni huu wa karibuni wa madreva na waajiri wao! Sikiliza wanavyohadithia kunyanyaswa kwao na matajiri wao. Tajiri anachojali yeye ni kutengeneza faida kubwa sana kwa kumyonya mtumishi wake ambaye ni maskini. Hapa ndiyo maana Mwl. Nyerere aliwaambia watanzania kuwa UBEPARI NI UNYAMA kama unakumbua!
 
watanznia kwa moyo wa dhati kabisa tuko tayari kwa mabadiliko na kuhakikisha hili tumeamua kuwa tutamchagua mh. Lowasa kuwa raisi wa tano wa jmt.
 
Chadema ina upungufu mmoja unaokizuia kuwa chama chenye nguvu kuliko vyote Afrika.
Hawakubali kukosolewa, na sera yao ya utawala wa ndani ni 'demokrasia ya mabavu'

Hiyo ni wewe na mitazamo yako mibovu! Unataka tuachie CCM waje watupangie jinsi ya kuendesha chama chetu! Ngumu ngumu mno!
 
nini chakufanya?

Babu Slaa apuuzwe, amegeuka mchumia tumbo! Ghafla amegeuka kuwa kipenzi cha TBC1, na wa gazeti la Uhuru! Hapo bado hujaelewa tu anaowatumikia?
Tunavyoongea Yuko majuu akila matunda ya jasho lake alilovuja wakati wa hotuba yake na waandishi wa habari!
 
Back
Top Bottom