Maoni: Watanzania hawataki tena kuwa tu manamba na vibarua, wanataka pia kuwa sehemu ya wawekezaji kwenye Bandari

Misozwe

Member
Dec 23, 2022
21
26
Nyakati zimebadilika. Hivi sasa ni mwaka 2023; sio 1961 ambapo tulijinyakulia uhuru na kujitosa katika uendeshaji wa taifa bila ujuzi wa kutosha, tukijaribu utekelezaji wa sera mbalimbali kama vile ujamaa na kujitegemea; sio miaka ya 1980 mpaka 1990 ambapo tulimiliki mashirika mengi ya umma bila uzoefu wa kutosha katika usimamizi, hali iliyopelekea ubadhirifu na ufisadi, hivyo kuyumbisha mashirika hayo; sio enzi za mwishoni mwa miaka ya 90 ambapo tuliuza mashirika yetu kwa bei ya kutupa; na wala sio kuanzia 2006 ambapo wananchi walipofukuzwa kutoka kwenye makazi yao kwa fidia ndogo au bila fidia kabisa pale palipoonekana kuwa na dalili ya madini, na maeneo hayo kupewa wawekezaji bila serikali kuwa na ubia/hisa.

Hizi ni zama za kuanzia 2017 Watanzania tulipofumbua macho na kutambua kwamba, kwa hakika, rasilimali zetu zina thamani kuu hata zisipokuwa zimeendelezwa tayari, na zinaweza kutumika kama dhamana (collateral) na/au nguvu ya mazungumzo (bargaining power) katika majadiliano na wawekezaji wenye nia. Ni katika kipindi hiki ambapo kampuni kama Twiga Minerals, Kabanga Nickel na nyinginezo zilizaliwa, ambazo serikali ya Tanzania inamiliki sehemu ya hisa zao. Kitu cha maana zaidi ni kwamba, serikali imejumuishwa katika usimamizi wa kampuni hizi, ikiwa ni pamoja na kutoa viongozi waandamizi kwa baadhi ya mashirika hayo ili kuhakikisha maslahi ya taifa yanazingatiwa ipasavyo.

Watanzania wachache nilioweza ongea nao, wanachoomanisha ni kuwa tunao uzoefu wa zaidi ya miaka 60 wa haya mambo; miaka 60 si kidogo kwenye kujenga uzoefu, watanzania wanajitambua, wameamka, sio wale wa zama zile ambao inawezekana baadhi ya viongozi wakawaona mbumbumbu. Watanzania sio wajinga tena. Watanzania wanaweza ku reason kwa kutumia facts. Ni wakati sasa tuanze kuendeleza rasilimali zetu wenyewe kama watanzania kujenga uchumi wetu, hata kama itachukua miaka 100, hakuna tatizo. Tanzania ipo, haitaondoka. Itakuwa faida kwa vizazi na vizazi. Wakati wa sisi wenyewe kumiliki uchumi wetu kwa asilimia kubwa ni sasa, ni wakati muafaka kutokana na sababu zilizoelezwa hapa juu.

Tuje kwenye suala la bandari. Kwenye bandari hatuanzii sifuri. Bandari ipo, inafanya kazi, inapata mapato, hata kama ni kidogo, ina thamani! Sio kama Twiga Minerals au Kabanga Nickel ambazo ndio zinaanza hatua ya kwanza.

Rasilimali yetu ya Bandari ipo. Justification inayotolewa ni kuwa inakosa ufanisi kwa kukosa usimamizi pamoja na vifaa vya kisasa vya teknolojia. Hili la kukosa usimamizi ndio hasa linawatia simanzi wananchi. Inamaanisha katika watanzania wote zaidi ya milioni 60 wanakosekana watu 20 au 30 wa kusimamia bandari? Inakuwa ngumu sana kuamini. Inasemekana kuna watu wanaingilia uendeshaji wa bandari ili kujinufaisha, hii ni sababu kweli? Kweli? Yaani pamoja na Raisi kuwa na vyombo vyake vyenye nguvu vya usalama na vinginevyo, bado kuna watu wana nguvu zaidi yake? Haiingii akilini. Kinachowezekana kuwa kinatokea ni mamlaka zinazomsaidia Raisi kufanya uteuzi zinamuangusha kwa kutopendekeza watu sahihi kwa kufanya upendeleo, labda.

Kwa hili la teknolojia ndio kabisa linatia simanzi zaidi kwa sababu haiingii akilini kwanini watumike middlemen DP World kupata software na hardware za kuendesha bandari. Hivi Dubai kuna Silicon Valley ya kutengeneza port management systems? Si wao pia wananunua off the shelf au systems kuwa developed from scratch kutoka kwa kampuni tengenezaji kama watu wengine? Dubai kuna manufucturing industries za cranes kama China? Sio wao pia wananua China kama wengine? Ni sababu gani inayotufanya sisi tununue kwao huku wakiongeza cha juu, hatununui direct toka kwa manufucturer; kwani DPW wanatupa bure? Watapata nini?

Kutokana na maendeleo ya kasi sana ya teknolojia duniani, ikichangiwa na AI, pengine tunaweza pata teknolojia nzuri zaidi ya hao wa DP World, inayoweza kuwezesha kutohitaji significant human inteventions kwenye operations, kuanzia meli inatia nanga mpaka kontena linapandishwa kwenye behewa au roli. AI ina uwezekano wa ku-manage kuanzia kutoa mizigo melini, ku scan, ku intepret data, kukadilia custom taxes na kodi nyingine, na logostics nyingine mpaka mzigo unamfikia mteja. Tusi limit our options.

Bandari ina thamani kubwa na biashara kubwa sana ndio maana DP World wako interested. Serikali labda tuseme haina hela za ununuzi vifaa hitajika, ingawa kiasi cha investment inayotakiwa hakijawahi kutajwa. Tujue, tuelezwe, hata kama, kwa mfano, ni shilingi trillioni 10. Sisi tunao wafanyabiashara wakubwa kama Bakhresa, Mo Dewji, Rostam, Angelina wa TPSF, wafanyabishara wa Kariakoo wana mitaji mikubwa tu, na wafanyabiashara wengi tu huku nchini, kuna mabenki ya biashara, kwanini tusiwashirikishe? Unaweza sema wafanyabiashara wanaweza kuwekeza lakini hatuna wataalamu wa kuendesha bandari kisasa; sasa, kama tunaweza kuajiri makocha wa timu za taifa kutoka popote duniani na kuwatimua pale wasipofikisha malengo, kwanini ishindikane kuajiri wataalamu wa bandari toka popote duniani na kuwapa malengo? Utasema trafiki bado watasumbua barabarani na kuchelewesha mizigo? Trafiki wameajiriwa na nani?

Kuna njia nyingi za kupata mitaji. Kwa mfano mmoja tu, tuko watu milioni 60 (yes, kuna watoto, wagonjwa, wazee, wasiojiweza, n.k. katika hao), lakini tukifanya kwa wastani kila mtu akachanga shilingi 100 tu kwa siku (zinaweza kuwa nyingi zaidi au kidogo kutokana na uwezo) kama hisa (au watu milioni 6 wakachanga shilingi 1000 kila siku, jambo ambalo kwa takwimu za biashara ya miamala kwa mitandao ya simu linawezekana), zinaweza patikana shilingi bilion 6, kwa siku tu; je kwa mwezi, kwa mwaka? Baada ya miaka michache si tutakuwa tumepata mtaji tayari? Hatuna haraka, bandari haiwezi kuhama. Watanzania tujaribu pia kuwaza nje ya boksi.

Wanachoshauri, ambacho naamini watanzania wengi wanawea kuunga mkono ni kuwa, ndio, bandari iendeshwe na sekta binasi, sekta binafsi ya Tanzania. Sekta binafsi popote pale duniani kwa kawaida huwa hazina ruzuku, so effieciency ndio kila kitu, usipo perfom, uko nje ya biashara, na kwa kuwa sekta iko result-oriented kama norm, hivyo tutaongeza ufanisi:

Ushauri:

1. Turudi mwanzo, hatujachelewa. Serikali iweke kwa uwazi kabisa changamoto zote za bandari ili wananchi wazijadili na kutoa mapendekezo ambayo serikali itayafanyia kazi na kutoa mrejesho utakaopelekea procurement process:
2. Zikaribishwe kampuni za sekta binafsi kuendesha bandari kwa vitengo tofauti tofauti, utawala, makontena, n.k. za watanzania zikipewa first priority
3. Serikali kwa kutumia wataalamu wake itengeneze port management systems (eGA wametengenza mifumo mingi tu, gepg, ppra, n.k) au i procure port management sytem kwa watengenezaji popote duniani.
4. Zitangazwe open tenda, hata kama ni kwa small manageable lots, watu wa procurement wanatumia sana njia hii, kwa mfano ku supply kompyuta ishirini ishirini kwa lot, au crane tatu tatu kwa lot ambazo naamini watanzania wanao uwezo kabisa wa kununua.
5. TPA ibaki kama msimamizi na mshauri na mtoa mwelekeo, mwenye maamuzi ya mwisho ya kisera na kiutendaji
6. Bandari haibinafsishwi, inaendelea kuwa mali ya umma
7. Tuone wapi kabisa tunashindwa ndio tulete wawekezaji wengine kama DP World, tena kwa kushindanishwa

Tukianza kwa mtindo huu, inaweza kuwa very complex (tuta simplify) na chaotic hapo mwanzoni, tutaanza kwa kuchechemea , tutaenda, tutafanya makosa, tutarekebisha, kutaboreka, hata kama process itachukua miaka 30 sio tatizo kwa sababu bandari ni yetu na haiondoki, sisi wa kizazi cha sasa tutamaliza muda wetu duniani, watoto wetu na wajukuu wataendeleza, bandari ikiwa ni yao na vizazi vinavyowafuata wao. Bandari ni yetu kama watanzania, hakuna amwenye mamlaka nje ya Tanzania mwenye uwezo wa kutuhoji. Hatua hii pia itachochea creativity.

Hatua hii itatuletea maendeleo ya kiuchumi kwa kupata kodi na kutoa ajira kwa vijana wetu, kizazi cha sasa na kijacho. Pia licha ya umiliki wa bandari kuendelea kuwa chini ya watanzania wenyewe, pia nafasi zote za utawala na utendaji eventually zitaendelea kuwa chini ya watanzania, kwa sekta binafsi, kuondokana hali ya kuwa vibarua na manamba peke yake.

Maoni haya nimeyakusanya katika kipindi cha wiki mbili hizi kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Tanzania, kipindi mbacho mjadala huu umekuwa ukiendelea, yakishirikisha watu zaidi ya 100 kutoka kada mbalimbali, randomly, siwezi kusema ni representative kisayansi, lakini sifa kuu wote ni watanzania. Ni mchanganyiko wa watu wa kawaida na viongozi, na zaidi ya asilimia 95 ya watu hawaungui mkono mkataba wa DP World. Nikajaribu kutumia maelezo mengi yaliyotolewa na viongozi kufafanua faida za mkataba huu lakini bado wengi niliiongea nao hawajaafiki.

Na kwa mtazamo wangu, hakuna maelezo yoyote yatakayotolewa na mtu yoyote yule yanaweza kuwashawishi kuukubali mkataba huu.

Wananchi wana sababu zao, ikiwemo hofu ya kutokea kuondolewa kwenye ardhi zao kama ilivyokuwa Loliondo na kwingineko, walio Oysterbay au Kurasini au Ukonga na kwingineko hawajioni wako salama, mwekezaji akitaka maeneo yao kwa ajili ya upanuzi wa bandari, itakula tu kwao. Wanasema hakuna kitu kikubwa kinachoogopesha, kinacholeta dharau na kuumiza kama vile kutwaliwa ardhi yako au ya ukoo wako na wewe ukiwa huna la kufanya mbele ya wawekezaji au watawala. Kuwa na uhuru kunakosa maana.

Please share na wengi kupata maoni zaidi ya watanzania kuhusu hili. Kumbuka kutoa maoni ni haki ya kikatiba ya kila mtanzania na sio kosa kisheria. Kikubwa ni kutumia lugha ya staha na ustaarabu.
 
Mbona mmeshindwa kuiendesha kabla hiyo bandari sana sana mnafanya uwizi,uzembe tu hapo
Mradi gani mshauendesha na kuusimamia,unakwenda vizuri
Hiyo mwendokasi tu mnambwelambwela tu
Mtanzania hawezi kuendesha wala kusimamia chochote,sahv anachojua ni kukata mauno tu

Ova
 
Mbona mmeshindwa kuiendesha kabla hiyo bandari sana sana mnafanya uwizi,uzembe tu hapo
Mradi gani mshauendesha na kuusimamia,unakwenda vizuri
Hiyo mwendokasi tu mnambwelambwela tu
Mtanzania hawezi kuendesha wala kusimamia chochote,sahv anachojua ni kukata mauno tu

Ova
Umeona eehhh...Yaani hao TICTS wanafanya Nini bandarini,wizi TU na urasimu
 
Mbona mmeshindwa kuiendesha kabla hiyo bandari sana sana mnafanya uwizi,uzembe tu hapo
Mradi gani mshauendesha na kuusimamia,unakwenda vizuri
Hiyo mwendokasi tu mnambwelambwela tu
Mtanzania hawezi kuendesha wala kusimamia chochote,sahv anachojua ni kukata mauno tu

Ova
Soma kwa hatua andiko langu kwa makini. Bandari kutokuwa na ufanisi tatizo ni nani mnawapa kuongoza. Mnawateua wenyewe halafu mnashindwa kuwasimamia walete ufanisi, halafu wewe uliyewateua unalalamika? Tatizo ni nani unafikiri? Utakuwa umeshapata jibu
 
Back
Top Bottom