Maoni: Ili kujenga uzalendo, Serikali ifute shule zote binafsi hapa nchini tubaki na shule za kata tu!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,852
18,261
Habari wakuu?

Naingia kwenye mada moja kwa moja bila kuwachosha. Baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) kutangaza matokeo ya mitihani ya Kidato cha Nne (CSE), nimetafakari sana na kugundua njia nzuri ya kuboresha elimu hapa nchini ni ama kufuta au kutaifisha shule zote za binafsi ili wanafunzi wote wakasome kwenye shule za umma (shule za kata).​

Mfumo huu sio mgeni hapa duniani. Nchi nyingi za Ulaya, Asia na Marekani hawa-entertain uwepo wa shule binafsi kwani waligundua zinachangia sana kudhoofisha kiwango cha elimu katika nchi zao. Ndio maana Mwalimu Nyerere aliona hili tatizo mara baada ya nchi kupata uhuru akaamua kutaifisha shule za wamisionari na kuzirudisha serikalini. Sasa wakati umefika Rais Samia afuate nyayo za Nyerere ili kulikomboa taifa hili kielimu. Kuna sababu kadhaa zilizonifanya nitafakari jambo hili kwa kina:

Mosi, ikiwa shule binafsi zitataifishwa, kutakuwa hakuna mashindano ya ubora wa shule kwa kuangalia ufaulu. Kwa hiyo, suala la ku-promote shule kwa kuzichuanisha kiubora litakuwa limekufa kifo cha mende. Na serikali haitapata tena wakati mgumu kutangaza shule bora kwani shule zote zitakuwa na viwango sawa au vinavyokaribiana.

Pili, kwa kuwa hakutakuwa na sehemu mbadala ya kuwasomesha wanafunzi zaidi ya shule za kata, itawalazimu wananchi wote kuthamini shule hizi na kuhakikisha kuwa wanaziboresha kwa udi na uvumba. Kwa sasa sio watu wote wanaopenda kuona shule za kata zinakuwa bora kwani hata zikiendelea kuwa duni, wazazi wanazo shule mbadala ambako wanaweza kuwapeleka watoto wao kupata elimu bora. Wakikosa mbadala lazima tu wataboresha shule hizi ili watoto wao wapate elimu bora.

Tatu, kwa kuwa shule hizi zitakuwa zimewashikanisha watanzania wote kwa pamoja (kama ilivyokuwa kipindi cha Ujamaa na Kujitegemea), hii itasaidia kurudisha uzalendo wa kitaifa kwa wananchi ambao umeshuka kwa kiwango cha kutisha. Kwa mfano, imefika wakati sasa wazazi wenye uwezo wa kusomesha watoto wao kwenye shule binafsi hawaoni uchungu pale elimu kwenye shule za kata inaposhuka kwani wanaona hilo haliwahusu. Lakini wazazi wakishabanwa kusomesha watoto wao kwenye shule za kata (watake wasitake) lazima tu watakuwa na uchungu na maendeleo ya shule hizi.

Kwa mantiki hii, ipo haja ya serikali sikivu ya mama yetu mpendwa Rais Samia Suluhu Hassan kufuta shule zote za binafsi hapa nchini ili kila mtanzania mzalendo akamsomeshe mwanaye kwenye shule za kata. Hakuna namna nzuri ya kukuza uzalendo zaidi ya kuchukua maamuzi haya magumu. Najua wapo watakaonuna lakini hatimaye tutaelewana tu.

Nawasilisha​
 
Hao watu walioajiriwa kwenye sekta ya elimu binafsi utawapeleka wapi, mtaani?
Njia nzuri ni kuboresha mitaala na mazingira ya elimu kwa ujumla ndipo tunaweza kuleta mabadiliko.
Na walimu pia watataifishwa na kuingizwa serikalini walipwe kulingana na salary scale ya serikali. Ikiwa wataona mshahara ni mdogo, waache kazi ya ualimu wakafanye kazi nyingine.
 
Kwanini serikali nayo isiige mikakati ya kuboresha elimu kama private?

Kuna msemo unasema first never follows hapa serikali lazima ikubali na kuiga kwa waliofanikiwa hivi ndio maendeleo huja.

Mfano ratio ya mwalimu kwa wanafunzi kimsingi haipaswi kuzidi 40 kwa ajili ya ufanisi ila utakuta serikalini huko kuna shule ina walimu wanane na wanafunzi ni 500+ hapo kuna ufanisi?
 
nchi za ulaya university kuna ranking, yaani utaifishe shule kisa kuna ushindani???kila mtu ashinde mechi zake kama mzazi unaweza kumlipia mtoto shule nzuri mpeleke, system unayopropose shule zitajibweteka mno.
Mkuuu, sio kwamba zitataifishwa kwa sababu ya ushindani bali ni katika kuboresha uzalendo na kiwango cha elimu kwa manufaa ya taifa zima kwa ujumla.
 
Kwanini serikali nayo isiige mikakati ya kuboresha elimu kama private?

Kuna msemo unasema first never follows hapa serikali lazima ikubali na kuiga kwa waliofanikiwa hivi ndio maendeleo huja.

Mfano ratio ya mwalimu kwa wanafunzi kimsingi haipaswi kuzidi 40 kwa ajili ya ufanisi ila utakuta serikalini huko kuna shule ina walimu wanane na wanafunzi ni 500+ hapo kuna ufanisi?
Mkakati wenyewe ndio huu wa kutaifisha shule zote ziwe chini ya serikali mkuu.
 
Mkuuu, sio kwamba zitataifishwa kwa sababu ya ushindani bali ni katika kuboresha uzalendo na kiwango cha elimu kwa manufaa ya taifa zima kwa ujumla.
Uzalendo utaletwa na serikali kuweka policies nzuri kutaifisha shule sio policy mojawapo,trust me kwa mazingira yetu ushindani lazima uwepo unless sijakuelewa how this will improve quality of education, quality of education na sio uzalendo nauliza...
 
Mkuu kutaifisha kutawafanya wananchi wote kuwa na collective responsibility katika kuhakikisha kiwango cha elimu kinapanda na kinaendelea kuwa juu.
 
Mkakati wenyewe ndio huu wa kutaifisha shule zote ziwe chini ya serikali mkuu.
Unadhani hiyo ni njia bora?

Shule ngapi zilitaifishwa na sasa ni dhoofu sio kimiundombinu tu bali hadi ubora wa kielimu zimepoteza pakubwa.
 
Unadhani hiyo ni njia bora?

Shule ngapi zilitaifishwa na sasa ni dhoofu sio kimiundombinu tu bali hadi ubora wa kielimu zimepoteza pakubwa.
Yes. Nadhani ni njia bora mkuu.

Ule utaifishaji aliofanya mwalimu Nyerere sio kama huu atakaofanya Rais Samia......huu utakuwa strategic zaidi.
 
Akili yako ndogo sana!

Halafu mtu kama huyu akiambiwa atoe mchango wa elimu katika Shule zake hizo za kata,povu kama lote!
Uzalendo haujengwi kwa kusomea ktk Shule za kata!

Mwigulu Nchemba analala na tai ya bendera ya Taifa lakini watoto wake nadhani wote wanasoma Feza!

Analipa karibia Milioni 40 kwa mwaka kama school fees.
 
Mkuu hapa umeenda nje ya mada. Hebu rudia kusoma hoja yangu neno kwa neno utanielewa.
 
Ikitokea hivyo, tutawapeleka watoto wetu kusoma Kenya.
Hapo utakuwa umekosa uzalendo mkuu. Na ikiwa utawapeleka watoto wako Kenya basi uhamie huko huko. Hatutakutaka kurejea hapa nchini tena.
 
Back
Top Bottom