Uchaguzi 2020 Maoni huru: Awamu hii Urais wakipata hata kura Milioni 3 wana bahati sana

Ndivyo ilivyopaswa kuwa lakini tatizo ni wapinzani wa Tanzania. Tuna wapinzani wa ajabu sana.

Upinzani ndani ya CCM ndio upinzani halisi nje ya CCM ni Vikampi vya watu binafsi. CCM ya Kikwete ilishindwa na CCM ya iliyokuwa imebeba hasira za Lowasa kukatwa.

Halikadhalika 2025 CCM itakayoshinda ni ile itakayotoka kwa Mtu atakayekuja na hoja za kufanya tofauti na CCM ya Magfl .
Upinzani upo ndani ya CCM.

Leo hii wapinzani kama Chadema wangeruhusu Mageuzi ya ndani na chaguzi huru ndani ya Chama Bila shaka Mwenyekiti angekua ni ama Zito Kabwe au Komu au Heche au Halima. Chama kingekua na mtizamo mpya na nguvu mpya. Leo hii Chadema inaongozwa na MTU aliyeipoteza njia mwaka 2010,2015, 2020 sasa.

Wapiga kura wakimuona Mbowe jukwaani wanapoteza imani ya kushinda. Miaka mitano Mbowe amekua ni MTU wa kulilia Uenyekiti tu huku Chaguzi zikiwa zinavurugwa bila tamko lolote. Sasa kamanda anabaki kwenye kiti na ujasiri wa kujificha nyuma ya shujaa Tundu Lisu.

Kama Kikwete aliwapa watanzania maziwa na nyama na samaki lakini walimkataa kwa kumwita dhaifu asiye na maamuzi na walitamani aondoke madarakani kwa ushawishi wa Mbowe na Dr.Slaa huku wakiamini kuwa nchi inapaswa kuendeshwa kidikteta basi watanzania Chini ya Upinzani wa Mbowe hawawezi kamwe kuiondoa CCM madarakani.

Kwanza Sheria za Uchaguzi zinafanana sana na zile za CCM. Yani Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi wana nguvu kuliko wananchi wote milioni 28+ wanaopiga kura.

CCM wajumbe wa wale wanaopitisha majina Dodoma wapo wachache lakini wana nguvu kubwa kuliko wapiga kura wote ndani na nje ya Chama.

Wapinzani hawana Sera zinazowavutia wananchi zaidi ya kumshambulia Magufuli binafsi. Wakati huo huo wananchi kwa uelewa wao ama mdogo au mkubwa wanazungumza Lugha moja kuhusu Magufuli kuwa ameleta maendeleo makubwa.

Yani hata mtu ambaye kijijini kwake hakuna maji ,barabara na dawa hospitalini huku biashara zikiwa zimedoda lakini ana matumaini kuwa Magufuli anabana kwa Muda tu lakini akikamilisha Kujenga miundo Mbinu hali ya maisha itapaa na kuwa nzuri kuliko Ulaya na Uarabuni na tutatoa misaada kwa Wazungu badala ya kuomba misaada.

mani hiyo ipo mpaka kwa wasomi, Wachungaji na mashekhe na wasanii wa Muziki mpaka watoto wadogo ,wazee na wafanyakazi pia wanamatumaini kuwa Hali ni ngumu kwa muda tu. Mpaka kule kusini kwenye wakulima wa Korosho, wote wana matumaini na JPM na wapo tayari kwenda naye kwa matumaini kuwa naye pia ni maskini mwenzao kwa sababu hasafiri kwenda kwa mabeberu kuomba misaada.

Wapinzani wengi hawajui maisha ya vijijini yalivyo kwa uhalisia matokeo yake wanaongelea mambo yasiyo na tija kwa mamilioni ya watanzania huku wakijikita kwenye Hotuba za kumkejeli Magufuli muda wote.
 
Jobless people katika ubora wao wa wakuilaumu serikali.

Mkuu wewe Endelea kulialia wakati huo Sisi tunaendelea kupiga hatua moja mbele na kutengeneza future ya Watoto wetu.

Life is about choice.
 
Hakuna wenye akili zao timamu wakapigia kura CCM ya Magufuli. Hata awe CCM, huo ndio ukweli MCHUNGU.

Miaka 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala ajira mpya kwa vijana wetu waliomaliza vyuo.

Utawala wa hovyo sana huu.

#LISSURAIS2020
 
1000 digits,
Mbulula wa Lumumba mna kazi mwaka huu!!
Hamkutarajia kumuona Lisu mliyempiga marisasi, sasa amerudi tena anagombea uraisi.
Hata mkipakaza vipi Watanzania sio wajinga wanaona unyama wenu live kwa macho!!
Huko vijijini maisha magumu sukari 1kg ni Tshs 3000/=+ haitegemewi kushuka!!
Mazao hayana bei mmefukuza wafanya biashara!!
Uchumi umevurugwa upside down, watu hawana ajira, viwanda hadi vijijini vimefungwa kwa kodi zisizo rafiki!!
We ni mgumu kuelewa maana uko Lumumba kwenye kiyoyozi!!
 
Kila chama kimeshachagua mgombea wake sasa sijui wataunganaje. Tanzania bado sana. Magufuli anashinda kwa kishindo sana
 
Dah...hapo umenena mkuu. Kweli tumemchoka JPM ... atupishe tu na aje mwingine.

Tunamtaka Rais mwenye huruma kwa mafisadi kwani hata wao ni binadamu pia.

...yaani dizaini fulani hivi..mpolempole...siyo Kila kitu anakomaa tu watu tunashindwa kufanya yetu
 
waTanzania wa ss sio wajinga maendeleo wanayaonaa barabara,ma flyover ,huduma za afya zilizo boreshwa,elimu mzee kagusa kila sekta ndani ya miaka mitatu tu.
Je akipewa mitano tena tarajia watoto wenu mashuleni kura chipsi kuku asubuhi, wali nazi mchana,wali kuku usiku.
 
Tatizo huwa hatuna Tume huru ya uchaguzi. CCM ilishajifia zamani, hapa tatizo letu ni tume tu. Vitendo alivyofanya Jiwe kama vile watanzania wenzetu kutekwa, kuuawa, kupotezwa, maiti lukuki kuokotwa kwenye fukwe na mengineyo mengi were the last nail in the coffin.
 
Wake up! Naona unasinzia wakati kumekucha😃😃, well, hao wapinzani hata wakiungana nothing changes, JPM is there for 5 years once again.Got it
 
Tatizo huwa hatuna Tume huru ya uchaguzi. CCM ilishajifia zamani, hapa tatizo letu ni tume tu. Vitendo alivyofanya Jiwe kama vile watanzania wenzetu kutekwa, kuuawa, kupotezwa, maiti lukuki kuokotwa kwenye fukwe na mengineyo mengi were the last nail in the coffin.
Hata Kama kukiwa na tume huru hamuwezi.
 
Inawezekena ccm isiwe bora kwa kiwango fulani lakini ni mara elfu moja ccm ikaendelea kutawala hii nchi miaka mingi ijayo maana wanajua kujireform kuliko kuwapa nchi wapinzani ambao muda wote wanahubiri chuki na kukosoa maendeleo yaliyofanyika nchini bila wao kusema wakipewa nchi watafanya nini.

Wapinzani wa nchi hii wamekuwa ni watu walama na visingizio kila wakati. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 walishinda wabunge na madiwani wengi lakini hakuna cha ajabu walichowafinyia wananchi kwenye majimbo ya tofauti na wabunge na madiwani wa ccm badala yake wamejikita kulaumu na kusingizia.
 
Inawezekena ccm isiwe bora kwa kiwango fulani lakini ni mara elfu moja ccm ikaendelea kutawala hii nchi miaka mingi ijayo maana wanajua kujireform kuliko kuwapa nchi wapinzani ambao muda wote wanahubiri chuki na kukosoa maendeleo yaliyofanyika nchini bila wao kusema wakipewa nchi watafanya nini.

Wapinzani wa nchi hii wamekuwa ni watu walama na visingizio kila wakati. Uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 walishinda wabunge na madiwani wengi lakini hakuna cha ajabu walichowafinyia wananchi kwenye majimbo ya tofauti na wabunge na madiwani wa ccm badala yake wamejikita kulaumu na kusingizia.
Wanaogopa ccm kuondolewa madalakini ni wapiga dili.
 
Na safari hii ndiyo itakuwa aibu kubwa kwa ccm maana ndiyo itakuwa mara ya kwanza kwa mgombea wao kuiondoa madarakani baada ya miaka 60 ya uhuru.
 
Back
Top Bottom