Mtu wa namna hii aachwe kuwa kiongozi kwakuwa alipata kura nyingi?

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,012
71,171
Huenda Maneno haya Machache yakaeleweka na watu wachache tu Kwa wengi ndio hao wanaoshabikia Ujinga.

Ipo hivi, ukikaa Kwa kutulia ukaitazama Dunia vizuri, utagundua Raia wengi wa Nchi zote Duniani, wamepitiwa na Ushetani hivi wa kupenda masuala ya kijinga jinga yaani masuala ya ovyo ovyoo.

Ni Rahisi sana Kwa Mgombea Uongozi anayeongea Pumba hata kama hazisaidii Taifa husika( Mf Kibajaji), kuweza Kushinda uchaguzi Kwa kishindo sana kuliko Mgombea anayeongea Facts( Mf.Mpina ) kwanini?? Kwa sababu watu wengi Duniani wamezolewa na Ushetani wa Kupenda mambo ya kijinga.

Namaanisha hivi, Mgombea X anaweza tumia jukwaa Zima kusifia Wanawake na kusifia wanaume ,kuongelea Mkongo , unywaji pombe baada ya kazi , kupeleka moto na Bado Akashinda Uchaguzi Kwa kishindo ... Kwa nn? Kwa sababu wapiga Kura wengi Dunian wamekua Brainwashed na masuala ya Ujinga ujinga.

Nini kinatokea Sasa? Dunia inaenda kua na Viongozi mbumbumbu ,majuha ,waliojaza vichwa vyao ujinga mtupu na Kwa namna hiyo, Itakua ngumu Taifa kupiga hatua.

Kwann Mabeberu wao hawaathiriki na hili?. Kwasababu wao Nchi zao zilijengwa zaman sana na hivo wakajiwekea Misingi yao imara linapokuja suala la Uongozi , ndio maana unaona wao Ni rahisi Kiongozi kuachia Madaraka pale anapohisi kapwaya, au anaondoshwa lakini Bado na wao Kuna wakati Wananchi wao Wajinga Kwa wingi wao huingia barabaran kutafuta mabadiliko yanayowafurahisha, na hapo ndipo Wenye Hekima huamua kutumia Nguvu , ndiooo wanatumia Nguvu kulinda Masilahi ya Nchi .

Mpumbavu hatakiwi kuongoza Nchi, Nchi haipaswi kuongozwa na mpumbavu Et kisa Upumbavu wake unapendwa na Raia wengi ambao wamekua Brainwashed na Sasa wanafurahia Upumbavu na wanaunga mkono Upumbavu.

Kwa mfano..... Chukulia watu wanaofurahia Ushoga, Hawa ikitokea Mgombea anatetea ushogaz wako tayari kumpigia kura na Akashinda Kwa kishindo kikubwa ( ingawa Ushoga ni Laana ya Nchi) ila atashinda..... Je mtu wa namna hii aachwe kuwa Kiongozi kwakuwa Alipata Kura nyingi?."

Hapa tunapata sababu ya kihakika kwamba, Sio Kura tu za makaratasi zinaweza kutuletea Viongozi Bora, Smart, wabunifu, wenye Maono , wanaojiamin, wazalendo, wanaweza kutuvusha kama Taifa, Viongozi Hawa wanaweza wasipendwe na watu wengi wajinga lakini wakapendwa na wachache wenye Akili na Hekima .


Sasa Tuje hapa kwetu ....... Je Kuna uwezekano wa kupata Viongozi Diwan, Mbunge, Rais asiyefaa ila kwakua kapigiwa kura na watu wengi wajinga basi awe Kiongozi??. ... Jibu ni ndio , na nyie wote ni mashaidi.

Kuna Siku nimekaa nikatafakari, Et Akina Nape, January ,Mwigulu , ndio ambao watatuchagulia Rais kupitia CCM?. .......

Bwana DOLA, embu tuweni serious kidogo basi Kuna Sheria na Kanuni ni LAZIMA VIVUNJWE KWA MSILAHI MAPANA YA NCHI "

Tuchukulie , Waziri Mkuu KASIM MAJAALIWA , kachukua Fomu ya Urais , na January naye kachukua Fomu ya Urais ........ Ni wazi Nape na Mwigulu, Kura zao zitakwenda Kwa January, Na pengine kwakua Wana mkono mrefu huenda wakahakikisha anapita kugombea Urais, na Hatimaye Kasim anapigwa chini...... SASA DOLA, hivi Kwa haraka haraka, January anaweza kutuvusha kama ambavyo angetuvusha KASIM ? Et sababu tu ya Kura za makaratasi?.. HAPANA ,HAIPASWI KUA HIVO, SHERIA NI LAZIMA IVUNJWE, NDIO SHERIA LAZIMA IVUNJWE NA IWASHANGAZE WENGI ,NDIO MAANA UNAONA UCHINA LEO HII WAMEMUONGEZEA XI JINPING MUHULA WA TATU WA KUONGOZA !!.


Kwakua Upinzani wamepoteza Dila na mwelekeo na hawajui nini Sasa wanasimamia na falsafa zao hazieleweki, wamelevywa Kwa kileo Cha AsAli ya Ikulu na wamesahau wajibu wao na Sasa Mwananchi anatakiwa kujisemea mwenyeweee , Na kwakua Dola ni CCM na Kwamba CCM inaitwgemea DOLA kuliko Dola inavyotegemea CCM basii

RAI YANGU kwako Dola Mwaka 2025 ,tuleteeni watu Si ambao watatokana na Kura tu, Bali tuleteeni watu ambao mmekaa mkatafakari na kuona kwambaz Hawa wataipigania Nchi, kiuchumi, KIJAMII, kitamaduni, kisiasa na Nchi itasonga mbele Kwa Amani, Maendeleo kama Taifa Kwa Ujumla.
 
Sukuma Gang msitegemee kurudi ikulu hata kwa dawa maana nchi masikini Kama TANZANIA ukiendekeza ngono Basi Mafanikio utaendelea kuyasikia
Ngono salama ni Afya, ndio maana tunahimiza Vijana waoe !!

Na nitashangaa kama Kuna Kijana Kwa umri wake wa kutosha, Et anaisusa ngono, wakati Wanawake tumeumbiwa sisi watupe Raha kupitia Ngono.
 
Hao uliyowataja ndio wanaongea na kufanya vitu vya kipumbavu?

Kukubali kuishi katika jamii yenye utofauti wa mitazamo ni kazi ngumu sana.

Kwanini unataka kila mmoja atumie Tafsiri yako ya upumbavu kufanya maamuzi ya kitaifa?

Na huo ndio upekee wa CCM kuna makundi yote mawili wahafidhina kama wewe na waliberali. Hivyo heshimu mtazamo kinzani kwasababu kwa pamoja mnaendeleza mapambano ya kushika uongozi ndani ya chama hatimae kushika dola.


Tanbihi:Siku CCM ikibakiwa na kundi moja la kimtazamo wananchi watachoka na kuamua kuchukuwa hatua zao wenyewe kwasababu usitegemee miongo ya hivi karibuni wapinzani kushika dola.
 
Watu wanaposhusha nondo zao acheni kujibu majibu mepesi. SUKUMA GANG Hilo neno limeletwa na kujazwa kwenye vichwa vya watu ili kuhakikisha hawafikiri nje ya box, Kila atakayejaribu kuona tofauti ataitwa SUKUMA GANG.

CHAWA WA MAMA, hii status wamepewa watu makini kabisa na tegemezi ila ukiidadavua kiundani ni maana mbaya kabisa na kutokuipokea ukiielewa, ili kuhakikisha hakuna upinzani ukiwa na wazo tofauti CHAWA watakuattack. Poor people
 
Watu wanaposhusha nondo zao acheni kujibu majibu mepesi. SUKUMA GANG Hilo neno limeletwa na kujazwa kwenye vichwa vya watu ili kuhakikisha hawafikiri nje ya box, Kila atakayejaribu kuona tofauti ataitwa SUKUMA GANG.

CHAWA WA MAMA, hii status wamepewa watu makini kabisa na tegemezi ila ukiidadavua kiundani ni maana mbaya kabisa na kutokuipokea ukiielewa, ili kuhakikisha hakuna upinzani ukiwa na wazo tofauti CHAWA watakuattack. Poor people
Huyo Jamaa Ni mjinga Mmoja anaamini katika falsafa za Magufuli za kuua watu na kuiba hela huku akiita watu wanyonge na kuwaaminisha watu kuwa bodaboda na Mama ntilie ni Ajira.
 
Ngono salama ni Afya, ndio maana tunahimiza Vijana waoe !!

Na nitashangaa kama Kuna Kijana Kwa umri wake wa kutosha, Et anaisusa ngono, wakati Wanawake tumeumbiwa sisi watupe Raha kupitia Ngono.
Hahaha hili unalipenda mzee mwenzangu.
Sema nn? Kwenye huu uzi umetema Madini Sana mwanangu
 
Back
Top Bottom