Uchaguzi 2020 Maoni huru: Awamu hii Urais wakipata hata kura Milioni 3 wana bahati sana

Jiwe anakipelekesha ccm anavyo taka maana hakuna mtu wa kusema ekosea. Kila mtu anamuogopa kwa kuhofia kibarua chake kuota nyasi.

Ccm imekuwa ya mtu mmoja hata kama wanachama hawataki lkn hawana njia ya kuwasilisha maoni yao.
Mali ya mtu moja ndiyo sasa ngoja tunamuondoe Magu na ccm yake ili iwefundisho kwa chama chochote cha sisasa wajifunze kutofautisha nyazifa Rais asiwe mwenyekiti
 
Nakubaliana na hoja , wapinzani wakiungana wanaitoa ccm . ila wasipo ungana ni ngumu na wasahau . Watu wamepigika kweli kweli . Mimi nipo mkoa fulani nyumba watu wanauza kwa ajili ya kutaka hata kujipanga , Bei inayouzwa nyumba ni kichekesho . Nyumba ya milioni 80 , inauzwa hata millioni 30.

Watu wapo hoi maendeleo ya vitu na maendeleo ya mtu vinasigana . tuwaendeleze watu na vitu vyao , si upande mmoja tu.

Yule anayesifia chama tawala , anasifia kwa sababu watu wansema na kufuata huo upepo . Ndiyo maana leo hii , ametokea mtu akiongea tu hoja moja . Upande wa pili unatikisika. Kwani walikuwa katika kifungo cha muda mrefu cha kutosikia hoja kinzani kwa muda mrefu .

Nawashauri ccm , siku wakimuacha tundu lisu ajidavuvue vizuri . Apate airtime katika vyombo vyote vya habari . Watanzania wataelekea kwake . wengi wa wa tanzania wanataka kusikia.
 
Hakuna wenye akili zao timamu wakapigia kura CCM ya Magufuli. Hata awe CCM, huo ndio ukweli MCHUNGU.
Miaka 5 hakuna nyongeza ya mishahara wala ajira mpya kwa vijana wetu waliomaliza vyuo..
Utawala wa hovyo sana huu.
Wafanyakazi jumla hawazidi million mmoja,Idadi ya wapiga kura nchi nzima million 29.Ukiondoa wafanyakazi wote wanabaki 28 million.Ni wazi wafanyakazi hawana ubavu mkubwa kama zamani kupinduwa matokeo.

Wananchi walio wengi ni wakulima au wafugaji,au wavuvi,au self employed.
 
Andiko lako zuri saaana kwa watu wenye stress litawasaidia, rudi shule ukasome siasa na focus yako iwe kwenye siasa za Tanzania na hasa mfumo wa ccm. Unaanzia wapi kuitoa ccm yenye mtandao kuanzia kwa balozi wa nyumba kumi, mabalozi ndiyo watafuta kura, kwa upande mwingine upinzani unategemea mafuriko. Poor analysis as u trying to compare unlikes.

Nikusaidie tu kimahesabu; tanzania bara ina jumla vijiji 12000;
Kila kijiji kina kinaweza kuwa na wastani wa idadi ya KAYA 1500 hivyo kuwa na wastani wa chini kabisa wa mabalozi 150.

Ukifanya hesabu za chini kabisa kwamba vijiji 12,000 vina mabalozi 12,000*150 = mabalozi 1,800,000. Kwa hiyo balozi akipewa jukumu la kutafuta wapiga kura wachache sana kwenye ubalozi wake mfano 10.

Kwa mahesabu ya makadirio utaona ccm ikipata kura 18,000,000

Kumbuka pia kuwa idadi ya wanaccm kwa hesabu za karibuni kulingana na ripoti ya PolePole wako 16,800,000

CCM ITASHINDA KWA 95% HUU NDIYO UKWELI MCHUNGU
 
Hizi tathmini nyingine ni sawa na mchambua soka alie bet. Ukweli anaweza kuwa ana ujua ila mkeka ukambana
 
Nakitazama hali ilivyo ngumu mtaani, uchumi umekua mgumu kuna mama wanashinda barabarani na nyanya zao na mchicha kutwa nzima hawauzi wanarudisha nyumbani jioni, frame kibao za biashara zimefungwa maeneo mengi, Wafanya kazi wa umma wanalia maslahi duni, mikopo elimu ya juu kizungumkuti mitupu kuna vijana wanalia hawana ada...
Delete ccm Oct 28
 
soma utafiti wa yule jamaa aliyepokonywa pasipoti na kusingiziwa sio raia utaupata

Sina muda huo Mchafu ila nina muda tu wa Kumpigia Kampeni Rais na Mwenyekiti wangu wa CCM Dkt. Magufuli ashinde na aweze Kuongoza tena.
 
26 Reactions
Reply
Back
Top Bottom