Uchaguzi 2020 Maoni huru: Awamu hii Urais wakipata hata kura Milioni 3 wana bahati sana

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Nakitazama hali ilivyo ngumu mtaani, uchumi umekua mgumu kuna mama wanashinda barabarani na nyanya zao na mchicha kutwa nzima hawauzi wanarudisha nyumbani jioni, frame kibao za biashara zimefungwa maeneo mengi, Wafanya kazi wa umma wanalia maslahi duni, mikopo elimu ya juu kizungumkuti mitupu kuna vijana wanalia hawana ada.

Lawama zote ni kwa serikali ya CCM ambayo iliahidi maisha bora kwa watanzania wote na matokeo yake watu wamejikuta katika hali ngumu ya maisha. Wananchi hawa wapo tayari kwa mabadiliko ya kiutawala, sasa kumbe shida siyo Magufuli ni CCM yake.

Aliyofanya JPM tunamshukuru sana anaweza kupumzika akamwachia mwingine kijiti aendelee. Aliyofanya ni makubwa sana na ni fahari kwa nchi historia yake itakumbukwa. Ni mwanzo mzuri kwa mrithi wake.

Wapinzani wakiungana wote wenye nguvu CCM ipo pekee yake hata kura milion 3 hakiwezi kupata. Watu wamechoka wanataka kuona changes za kweli zenye kuleta neema kwa nchi yetu. Wakiungana wapinzani na wanajiandaa bila uoga kusimamia ushindi wao wa haki basi CCM chalii. Tuliona KANU ya Kenya ilivyodondoshwa collaboration ya vyama vya siasa chini ya Mwai Kibaki
 
"... Wapinzani wakiungana wote wenye nguvu CCM ipo pekee yake hata kura milion 3 hakiwezi kupata. Watu wamechoka wanataka kuona changes za kweli zenye kuleta neema kwa nchi yetu.

Wakiungana wapinzani na wanajiandaa bila uoga kusimamia ushindi wao wa haki basi CCM chalii. Tuliona KANU ya Kenya ilivyodondoshwa collaboration ya vyama vya siasa chini ya Mwai Kibaki.

KWA TAMAA MLIZONAZO KUUNGANA HAITAWEZEKANA. KILA UCHAGUZI MNAISHIA KUSEMA KUUNGANA, VITENDO HAKUNA.
 
Kama serikali huwa inashauriwa na watu kama wewe basi ndiyo maana nchi iko kwenye shida ilipo.

Magufuli atapigwa kura nyingi sana, na huenda mkalazimika kutumia siku nyingi sana kutafuta njia ya kubadili matokeo.

Katika jitihada hizo, safari hii mmewahiwa ki tech. Uchaguzi uliopita mlikuwa na China tu. Uchaguzi huu hata China wamejipanga kuwaingiza mkenge ili mkamatike. Magharibi ndiyo kabisa inataka mjifunze maana ya utu na haki za binadamu.

Iandaeni nchi kupambana na wananchi wake barabarani kama mtalazimisha kama huko nyuma.
Hizi pre-emptive propaganda zenu safari hii hazifiki popote. Isaidieni nchi ijiandae inavyotakiwa. Genge hili la wezi CCM halitazuwia kilichoandaliwa dhidi ya dhuluma zenu. Kiko juu mno ya uwezo wenu.

Accepting the possibility of loss at war is one of the best defensive strategies.
 
Tuna utawala wa kipumbavu sana, enzi za Nyerere watawala wa namna hii aliwaita WASHENZI NA WENDAWAZIMU. Kushindwa kuwajibika kwa serikali hii katika matukio ya kifedhuli yanayoendelea nchini, inamaana TANZANIA HATUNA SERIKALI. Bali kuna GENGE TU linalotawala kihuni na kihalifu, utawala wa namna hii SASA BASI.

MITANO YA MKONO WA CHUMA, INATOSHA.
 

Attachments

  • Makonda ajitangaza mla raha namba moja duniani..mp4
    857.8 KB
Uchumi umepiga mweleka hakuna mwananchi wa kawaida atakayeipigia kura CCM zaidi ya MATAGA/Wachumia tumbo.
 
Utafiti wako huu kuwa Watu wameichoka CCM uliufanya wapi na lini Mkuu? Na je, hao hao Watu wako wamekuhakikishia wanawapenda Upinzani?
Wewe wa elfu saba saba kila siku kutoka Lumumba kwa kazi ya propaganda tu, huwezi kuyaona hayo anayozungumzia mleta mada.
 

Attachments

  • Makonda ajitangaza mla raha namba moja duniani..mp4
    857.8 KB
Huwa nacheka sana nikiona mada za namna hiii but tujipe muda muda ni hakim mzuri sana

Hapa leo hata kampen bado haijaanza watu mnasema hayo
 
Back
Top Bottom