Manyara: 8 mbaroni kwa kushangilia kifo cha Magufuli

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Wakazi 8 wa Mererani Wilaya Simanjiro wanashikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Manyara kwa kosa la kukejeli na kushangilia kifo cha Rais John Magufuli.

Rais John Magufuli amefariki Machi 17 kwa matatizo ya moyo na atazikwa Machi 26, Chato, Mkoani Geita. Taifa lipo katika maombolezo ya siku 21, huku bendera zikipepea nusu mlingoti.
 
Polisi wa Tanzania ni janga la Taifa.

Hivi kama wangewaacha washangilie mpaka wachoke dunia ingejua kuwa wananchi wa Tanzania wana sherekea kifo cha rais wao?
Je wanataka kila mtu ahuzunike/alie?

Tumefuga KENGE wanaoishi kwa kodi zetu aisee.
 
Kilimanjaro Inahusika Vipi Na Manyara Sasa?
Taarifa Nyingine Mnafanya Tuzione Chumvi.
 
Sasa Kilimanjaro ndio Uko Manyara? Ni zaid ya makanjanja wale wakosa akili wao wamemiliki Tekno za kutupa pale Manzese washakua waandish..uandishi ni kaz kama kaz nyngne au nasema uongo ndugu zanguuuh
 
Yaani mzee ameondoka, lakini bado nguvu yake imeendelea tukutamalaki!! Angemaliza hii miaka mitano mingine, hakika tusingekuwa na tofauti na wale raia wa Korea ya Kaskazini walio chini ya utawala wa yule dogolasi Kim Jong Un! 😇

Mama ana kazi nzito sana ya kuwabadili hawa wanafiki na wazee wa kujipendekeza! Mambo ya watu kushangilia upuuzi wao huko yanawahusu nini polisi? Wamefanya jinai yoyote ya kuvunja mali za watu?
 
Back
Top Bottom