Tofauti kati ya mazishi ya watu siyo kigezo cha utaifa wao. Daudi Balali ni mtu wa huku Iringa sehemu moja inaitwa Malangali, lakini kazikwa Marekani. Kuna mahujaji hufia Makkah na huzikwa huko huko Makkha. Mazishi ya mtu kufanyika mahala inategemea na mapenzi ya mtu. Nenda Arusha kuna watu lukuki ambao kwa asili ni "watanzania" lakini wamezikiwa Nairobi kenya.
Kuna watu wana imani kwamba wakifa wasisafirishwe kwenda kuzikiwa kwingine, hao nao wasafirishwe kuja kuzikiwa Tanzania kwa hofu kwamba wakizikiwa huko wataonekana kuwa si watanzania!! Kuna watu hapo hapo Dar huzikiwa Makaburi ya Kisutu na wengine hata iweje ni lazima wazikiwe Makaburi ya Kinondoni.Mahali anapozikwa mtu inategemeana na utashi wake au wa familia yake baada ya kifo kutokea na wala haihusiani na utaifa wa mtu. Kuna watanzania wengi tu wamezikwa nchi za nje ingawa uwezo wa kuleta maiti zao ulikuwepo!!
Matola mimi hoja yangu ni kwamba hamuwezi kuundoa utanzania wa Manji eti kwa sababu tu ni mhindi au kama mnavyosema ni fisadi. Kuna makabila hapa tanzania wanapiga sana wake zao, wengine wanauana sana, lakini huwezi sema kwamba si watanzania kwa kuwa tu wana tabia hizo. Manji ahukumiwe kwa makosa yake lakini asishutumiwe kutokana na asili yake!!