Kuna wakati nilikuwa humu JF kwa ID nyingine, ilikuwa ninadhani 2009, kuna bwana alileta uzi mzuri sana hapa, si mkumbuki jina. Alisema Tanzania ya leo si ile ya Nyerere ya ujamaa na kujitegemea, kila mtu ni ndugu na watoto wote wanasoma pamoja, anaefaulu anakwenda secondary, hata kama mzazi wake hana pesa, atapata barua ya balozi wa nyumba kumi, na katibu kata mpaka wilayani atakapo chukua warrant ya kusafiria kwa train kwenda shule.
Tanzania ya leo tumegawanywa, watoto wa vigogo wanasoma Braenburn, IST, Fedha boys ect, watoto wetu wanasoma shule za kata. Matokeo ya shule za kata wanaopata div four wamefaulu angalao wanaondoka na cheti, yaani wenzao wana wapongeza, wakati wale wa Braenburn wanatoka na div I na II, anaepata III walimu wenyewe wanambeleza mzazi motto arudie mitihani kwa gharama yao, wakimuonea huruma pesa alizolipa.
Watoto wao wakimaliza shule wanakwenda kusoma nje ya nchi, wakirudi wanakuwa wameandaliwa nafasi za kugombea katika chama na taasisi nyingine, watoto wetu wanaishia kuwa wapiga kura kuwapigia kura watoto wao.
Watoto wao wakipata matatizo wazazi wao wanapiga simu na yanamalizwa, yakikwa magumu sana ndiyo inabidi waitwe polisi, wakifika polisi mahojiano yanfanyika katika ofisi ya mkuu wa kituo, na kama itabidi alale ndani, mkuu wa kituo mwenyewe anakwenda kumchukulia soda na mishikaki, na analazwa ofisini kwa mkuu wa kituo.
Watoto wetu sisi wakikutwa na kosa wanakaa mahabusu miezi sita, waka kesi haijasikilizwa.
Baada ya kuagana na ujamaa tumebaki na tabaka la wapiga kura na wapigiwa kura.