Nature
JF-Expert Member
- Nov 5, 2014
- 758
- 2,027
Binafsi nimeshangazwa sana na uongozi wa Klabu ya Simba SC kukurupuka kumkana Kocha wa Makipa, Muharami Said Mohamed kutokana na tuhuma za Kukutwa na madawa ya kulevya kwa kusema kwamba Klabu ya Simba haikuwa na mkataba naye bali alipewa mwezi mmoja wakati Simba inatafuta Kocha Rasmi wa Makipa,
Cha ajabu zaidi ni kwamba imemtangaza kocha mpya masaa matatu baadaye.
Ni vyema Uongozi wa Klabu ya Simba na Mashabiki wa Soka kwa ujumla kukumbuka kwamba, Miaka kadhaa iloyopita Aliyekuwa Mwenyekiti na Mdhamini wa klabu ya Yanga Bwana Yusuph Manji aliwekwa mahabusu kwa Zaidi ya Miezi mitatu kwa tuhuma za Makosa tofauti tofauti ikiwemo kutumia madawa ya kulevya. Na mahakamani ukaketwa ushahidi wa Kitabibu baada ya kupimwa mkojo kuwa amethibitika kitumia madawa ya kulevya (japo ilitiliwa shaka)
Katika kipindi chote cha Kesi ya Manji uongozi wa Klabu ya Yanga haukutoa Kauli yoyote kumhusu mpaka mahakama ilipotoa maamuzi ya mwisho..pamoja na kwamba Serikali ya wakati ule ilitisha haswaa na kulikuwa na kila sababu ya Yanga kama klabu kuogopa na kumkana Manji lakini Yanga haikusema neno liwe jema au baya.
Pia ni vyema tukakumbuka Kwamba haya mambo siyo mara ya kwanza kutokea katika michezo...
Mlinzi wa Klabu ya Manjester City Benjamin Mendy Alishtakiwa kwa makosa ya ubakaji, utekaji na unyanyasaji wa kingono na mpaka sasa yuko Gerezani lakini Haikuiathiri Klabu kwa namna yoyote ile..
Pia Tumeona kwa wachezaji Kama Mason Greenwood nk wote hawa Klabu zao zilitoa kauli ya kukemea vitendo vyao lakini siyo kuwakana
Katika hili Uongozi wa Kalbu ya Simba ni lazima ukubali kuwa umekurupuka kwa maana tuhuma zinazomkabili Mharami hazijathibitishwa na mahakama ....hakukuwa na ulazima wa Klabu kutoa Statement ya haraka haraka kumkana kocha na kutoa maelezo ya kitoto kabisa Eti aliombwa afundisha kwa Muda wa Mwezi mmoja
Swali ni Je kama Tuhuma hizi zisingekuwepo, leo hii Simba wangemtangaza Kocha mpya wa makipa...?
Huo mwezi mmoja ulikuwa unisha leo?
Kwa kweli Statement ya Klabu inaonekana imeandikwa kwa Hofu na Mashaka makubwa na inaacha maswali mengi zaidi..ni afadhali wangekaa kimya na kupata muda mzuri wa kutafakari kauli ipi ya kusema.