Mtu anatimba na wanasheria nane, na sio wanasheria tu ila ni vichwa vya wanasheria 8. Unategemea watamueka ndani ili baadae akishinda kesi washtakiwe wao? Si watamlipa mpaka pesa za kuchukua wanasheria.Sijawahi ona mtuhumiwa anapewa kiti akae na kukunja nne,Jana Manji walimpa kiti akae. Halafu badae wanakuja kutwambia wamemlaza mahabusu .
Acha move iendeleeJana baada ya mwenyekiti wa club ya Yanga na mfanyabiashara mkubwa Yusuph Manji, na mchungaji Gwajima kuwasili polisi central, tulishuhudia badae wakiondolewa kituoni kwa gari nyeupe. Leo mchana kamanda Siro ametoa taarifa kuwa bado wanashikiliwa kwa mahojiano. Binafsi sijaelewa imekuwaje hawa wakapelekwa mahabusu kimya kimya? Na wapo mahabusu ipi?
Sky upo sahihi. Hata iwe mahabusu ya "gest" unakuwa hauna uhuru wa maamuzi, tena bila mwanamke.hata kama alilala machinjioni lakini alikuwa chini ya ulinzi tena bila mke wake.
Hivi kaka wewe unaamini kabisa serikali yetu inaweza ikamueka chini ya Ulinzi mtu kama Manji mwenye pesa zake? Unadhani wakimsumbua sana Manji, baada ya kesi Manji atawaacha hivihivi? Kama Lissu tu anawasumbua na kuwachezea wanasheria wa Serikali atakavyo, unasemaje juu ya mtu kama Manji ambae jan tu kaenda na wanasheria 8. Ingekuwa ni nchi za wenzetu walau ningeamini kwamba Manji ataweza kunyooshwa ila sio nchi hii.Siyo lazima achanganywe na mahabusu wa kawaida lakini mahabusu hata kama ni Kilimanjaro kempinski ile kuwa chini ya ulinzi na kunyimwa uhuru.
Mimi nadhani wale watu walienda kuombwa msamaha.Basi hakuna haja ya kushangaa wengine kulala lupango wengine kuamua wakalale wapi. Hata jela kuna VIP wing.
Wale wasanii mapicha kila siku na kutamba wana hela hili sekeseke limeonesha kwanza hizo hela hawana na akili hawana pia.
Unasemaje ya Manji kuhojiwa na Kamanda Siro mwenyewe tofauti na hawa vijana wengine?Hawa walikuwa wawili tu na alikosekana mheshimiwa Mbowe tu pale, wale vijana wenu walikuwa wengi, waliingizwa kwenye defender tena nyuma kule mnasimama na kushika bomba.
Mkuu hakuna kinachoshindikana, sema akitoka hatakaa tena Tz ndiyo anahama.Hivi kaka wewe unaamini kabisa serikali yetu inaweza ikamueka chini ya Ulinzi mtu kama Manji mwenye pesa zake? Unadhani wakimsumbua sana Manji, baada ya kesi Manji atawaacha hivihivi? Kama Lissu tu anawasumbua na kuwachezea wanasheria wa Serikali atakavyo, unasemaje juu ya mtu kama Manji ambae jan tu kaenda na wanasheria 8. Ingekuwa ni nchi za wenzetu walau ningeamini kwamba Manji ataweza kunyooshwa ila sio nchi hii.
Sijajua Mkuu umri wako na ufatiliaji wako wa mambo ya siasa nchini.Mkuu hakuna kinachoshindikana, sema akitoka hatakaa tena Tz ndiyo anahama.
Hana mume huyoMbona umeshikilia hio bila mke wake?
wake zao hata wasipokua karibu nao wanaridhika wasipokuwepo pesa ipo karibu yao je ww labda uwe karibu na kunguniIwe mahabusu au la lakini usiku wa jana walikuwa chini ya ulinzi tena mbali na wake zao.
Bora ata hao mumewaona, je Majizo ameonekana popoteHata Mimi ninashangaaa, kuna sitofahamu.
Kumbuka, akina TID na wenzake walitolewa central police kwa defender hawa watu wawili walibebwa na Land cruiser (Shangingi) tena wakiwa na wana sheria wao.
Walilala mahabusu ipi?? Gwajima atajibu ibada ya jumapili