urithiwetu
Senior Member
- Mar 5, 2009
- 103
- 3
Hawawezi kumpeleka Slaa mahakamani au kumdai fidia ,ndugu napenda uelewe kuwa kinachotokea hapa ni mapambano ya kambi ndani ya CCM na si kingine chochote kile ,na wala si kwamba wanaupigania ufisadi ,hio ni tiketi tu ya kugandamizana ndani ya chama chao ,au kwa zaidi ni amjungu ya wao kwa wao ,hivi unataka kutuambia Mengi alikuwa hawafahamu hao mafisadi tokea walipokuwa hawajatajwa na walipotajwa na akina Slaa ? Na kwa nini alikuwa Bubu mida yote hiyo mpaka juzi na jana jambo ambalo limeshapigiwa makelele zaidi ya mwaka sasa na kesi za rangi za kinyonga na miondoko yakobe zipo mahakamni.
Kitu kimoja ambacho inabidi mukielewe ikiwa mpo WaTz mnaofuatilia siasa za Tanzania ,Hamasi ni chama kilichoasisiwa na Wayahudi(Kama mnaifuatilia) ili kujipenyeza ndani ya kambi za wapelestina kwa kasi na kujua mambo ya ndani ya Wapalestina lakini baada ya kupenyeshwa kikageuka na kugeuza kibao ingawa bado kuna majasusi wanatumika wakiwemo ndani ya Hamasi lakini sehemu kubwa imebadilika na kuwa na itikadi za Kipalestina na hivyo kuwapa tabu wayahudi.
Sasa Hapa petu moja ya ujasusi uliopenyezwa ni hiki CHADEMA ,hiki kinasemekana ni pandikizi la CCM katika vyama vya Upinzani ,hapo awali yake lakini katika kutamukiwa kumetokea mapinduzi na kuibadili nia iliyokusudiwa na Chama Tawala kusoma harakati za vyama vya upinzani lakini ndani yake humo Chadema kuna waliowatiifu na kwa za CCM kwa maana wamebaki na nia ile ile japo huwezi kuwaelewa kwa kuwa dili limebadilika inabidi wajifiche na kuonekaana ni CHadema damdamu .
Sasa kumetokea mpasuko ndani ya CCM (Kambi za ndani ya CCM) ,hapa wale majasusi inabidi waonyeshe ni upande gani walioko ambao kusaidia kwao kambi hiyo ndiko kunakojitokeza hivi sasa ,hivyo angalieni sana mtaona kuwa maficho na rangi ya CHADEMA huwa inajitokeza tokeza na kufifia kwa maana WACHADEMA wamechanganyikiwa hawajui wapi pa kushika ila inaonekana kuwa CHADEMA wapo upande wa mafisadi kila awapo Kikwete na Chadema unaikuta kuwepo huko ,Zitto alikubali mitambo inunuliwe ,hapa palitokea kutofahamiana na Slaa ,Mengi nae anawapinga mafisadi na kumuunga mkono Kikwete Slaa anaonekana kumuunga mkono Mengi ,hivyo utaona migongano hii inatokana na kuwepo majasusi ndani ya Chadema ambao wanatoa sapoti kwa kiasi fulani pale mambo yanapoonekna yanataka kuingia doa ,tutaona makubwa tu maana ,kuna watu wamekaa pembeni wanaangalia miondoko ya Chadema na kumsifia pamoja na kumkingia kifua Mengi CCM nambari one.
Acha spinning & trying to confuse some people man with your Party-politics conspiracy theories.
Inahitaji courage fulani kukusanya vyombo mbalimbali vya habari (havikuwa vya IPPMedia kama walivyodanganya wakuu fulani) na kumtaja mtu kama RA, kwani influence yake inafahamika. Ni kama King-maker vile.
Watu wamekuwa wakimtaja kwenye mazungumzo. Mengi amekuwa wa kwanza kupata courage ya kumtaja hadharani. Ingawa unajaribu kudai angesema mapema zaidi, nani mwingine ametamka kabla ya Mzee Mengi?
Much respect Mengi. Tunasubiri kesi ya Manji ili uanike uozo wote!