FULL TEXT: HOTUBA ya Kambi ya Upinzani iliyosomwa na Lissu, Katiba na Sheria, yaibua makubwa bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

FULL TEXT: HOTUBA ya Kambi ya Upinzani iliyosomwa na Lissu, Katiba na Sheria, yaibua makubwa bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tumaini Makene, May 3, 2013.

 1. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #1
  May 3, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Wakuu hii ndiyo hotuba ya Kambi ya Upinzani Bungeni, Katiba na Sheria, inayosomwa bungeni na Waziri Kivuli Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu;

  1. Soma na utaona msimamo wa CHADEMA juu ya mchakato wa Katiba Mpya

  2. Mawasiliano ya viongozi wa juu wa CCM, sekretarieti, akiwemo Dkt. Asha-Rose Migiro, Nape Nnauye, Mwigulu Nchemba, Seif Khatib na katibu wao wa sekretarieti walivyokuwa wakiwasiliana ili kuhujumu mchakato wa katiba mpya

  3. Utaona masuala ya uvunjwaji wa haki za binadamu kwa facts, ujionee namna walioko madarakani walipolifilisha taifa mahali pabaya.

  Makene

  ===============================

   
 2. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #2
  May 3, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,574
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Hii hotuba ni nzuri sana na ya kisomi.

  Msigwa alipaswa kuomba msaada kwa Tundu Lissu ili na yeye aandae hotuba ya kisomi sio ule uchafu alioleta juzi Bungeni.

  Hongera Tundu Lissu.

  Hoja za Lissu zinahitaji kujibiwa kwa hoja...
   
 3. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #3
  May 3, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,574
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Kuhusu Kujitoa Tume ya katiba Mpya:

  It is very clear sasa kwamba CHADEMA wamezoea kupiga mikwara wasiyoweza kutekeleza. WAMESHINDWA kujitoa.

  Mbaya zaidi CHADEMA wametoka kwenye hoja ya kujitoa kwenye mchakato, hotuba ya Lissu imekuja na mambo mengine mapya kuwa watahamasisha watanzania kuikataa rasimu.

  Kuhamasisha watanzania kuikataa rasimu ni tofauti na kujitoa kwenye mchakato.

  Actually hata mimi, wewe na yule tunaweza kuhamasisha watanzania kuikataa rasimu iwapo tutaona haina manufaa kwa taifa. Kwahiyo kitendo cha CHADEMA kusema watahamasisha watanzania kuikataa rasimu sio kitu cha ajabu, ila kina utoto ndani yake kwa sababu rasimu wenyewe hawajaiona. Utajiandaa vipi kupinga kitu ambacho hujakiona kama kina manufaa au hakina manufaa.

  All in all chadema MKWARA waliopiga wa kujitoa kwenye mchakato wa katiba ifikapo tarehe 30.4.13 UMESHINDWA. CHADEMA imemsikiliza Prof. Baregu ambaye amewaambia kujitoa kwenye mchakato wa katiba ni siasa za KITOTO...
   
 4. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #4
  May 3, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hotuba hii imenikumbusha maneno ya Muishiwa dhaifu aliyo yatoa wakati wa kampeni za mwaka 2010 alipokuwa akiuza sura mjini Singida "Ni kheri Dr. Slaa awe rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuliko Tundu Lissu kuwa Mbunge".
   
 5. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #5
  May 3, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,574
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Swala la wajumbe kutengwa pesa za kutibia iwapo watapata UKIMWI linahitaji maelezo toka kwa waziri husika. Itakuwa kitu cha ajabu sana kama kuna pesa za namna hiyo!!!
   
 6. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #6
  May 3, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,574
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Katika swala la Mwangosi, Lissu alipaswa pia atoe ufafanuzi wa jinsi CHADEMA inavyotumia picha na video za tukio la kifo cha Mwangosi kujiingizia pesa. Ikumbukwe kuwa Mwangosi alikufa kwa sababu CHADEMA wakiongozwa na Dr. Slaa walikataa kuheshimu amri halali ya polisi na kwamba Dr. Slaa aliwachochea vijana wadharau amri ya polisi lakini yeye mwenyewe Dr. Slaa aliheshimu amri hiyo na kujifngia hotelini Iringa mjini huku akifuatilia matukio kwa njia ya simu kuulizia mambo yanaendeleaje.

  Fujo zilizoongozwa na Dr. Slaa kwa simu zilisababisha Mwangosi kufa na sasa video na picha zake zinatumiwa na CHADEMA kujiingizia fedha ndani na nje ya nchi.
   
 7. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #7
  May 3, 2013
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,796
  Likes Received: 171
  Trophy Points: 160
  Hongera Lissu!kazi nzuri!watoe ufafanuzi hawa walaji wa pesa za umma!Ufisadi usiokubalika huu kwa maslahi ya taifa!Hongera Chadema.
   
 8. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #8
  May 3, 2013
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,241
  Likes Received: 1,097
  Trophy Points: 280
  Huyu mtu mpaka uwe na akili timamu ndo unaweza kugugundua anachomaanisha
   
 9. E

  Eddie JF-Expert Member

  #9
  May 3, 2013
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani nusu ya hotuba inazungumza habari za mkoa mmoja tu Arusha tena kata ya Sombetini tu, hiki chama kina kazi kuba sana kujivua tuhuma za ukabila na ukanda
   
 10. t

  thatha JF-Expert Member

  #10
  May 3, 2013
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Wapi mahala ambapo hotuba ya lisu imeonesha kipao mbele cha kushughurikia changamoto ziliopo kwenye wizara ya katiba na sheria,zaid anlalamika kama mtoto mdogo.
   
 11. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #11
  May 3, 2013
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,453
  Likes Received: 1,351
  Trophy Points: 280
  Mtu akivunja shaeria anauawa? Tena mbele ya RPC?
  Haya ndiyo yametokea kusini,bodaboda kapiga mshkaki na kakataa kusimama askari kamuua,is it justifiable???
   
 12. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #12
  May 3, 2013
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,069
  Likes Received: 8,677
  Trophy Points: 280
  mSHAAANZA KUIKUBALI cdm JAPO KIMOYOMOYO......keep it up.
   
 13. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #13
  May 3, 2013
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,135
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Hujaona ya Asha Rose ? Anatakiwa kufungwa huyu......hujaona posho za tume ? Hujaona ya haki za binadamu? Hujaona ya Mwangosi?
   
 14. M

  MNYOO JOGOO Senior Member

  #14
  May 3, 2013
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 195
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Contentful....it hurt kuona watu wakifanya kazi backdoors!
   
 15. E

  Eddie JF-Expert Member

  #15
  May 3, 2013
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Bibie punguza munkari, rudi kasome tena post yangu msisitizo upo kwenye neno nusu kama hujaelewa uliza tena
   
 16. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #16
  May 3, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Mimi nitawashangaa watakaotumia muda wa thamani hapa, badala ya kujadili issues kwenye hotuba ya Lissu juu ya suala muhimu kabisa la mchakato wa Katiba Mpya, waanze kukimbizana na akina ZeMarcopolo na Chris Lukosi.

  Wakuu, tujikiteni kwenye hoja iliyoko mezani, badala ya kukimbizana na watu ambao wengine wameandikiwa taarifa za kina hapa hapa jukwaani kuwa ni wagonjwa wanapaswa kuwa Milembe hapa Dodoma au hospitali zingine za namna hiyo kokote duniani.

  Waje hapa wajibu hoja kama hizi;

  Mheshimiwa Spika,

  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina ushahidi unaoonyesha kwamba njama za kuhakikisha kwamba wanaCCM pekee ndio watakaochaguliwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upande wa Tanzania Bara zilipangwa katika ngazi za juu kabisa za CCM. Mnamo tarehe 3 Machi, 2013, siku mbili tu baada ya Mwongozo wa Tume kuanza kutumika, Katibu wa NEC ya CCM, Uhusiano wa Kimataifa Dr. Asha-Rose Migiro alituma barua pepe kwa wajumbe na watendaji wa Sekretarieti ya NEC ya CCM yenye kichwa cha habari: ‘MUHIMU!! MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA.’

  Barua pepe ya Dr. Asha-Rose Migiro inasema: “Naandika kuhimiza kazi ya kuwatia hamasa Makatibu wa Mikoa wasimamie kikamilifu mchakato wa kuundwa kwa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba. Kama mnavyofahamu Tume ya Katiba imeshatoa taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari ... kuhusu zoezi hili muhimu. Sambamba na hatua za awali tulizochukua baada ya kupata rasimu ya mwanzo ya Mwongozo wa Tume, hivi sasa tunatakiwa tuongeze juhudi za ushiriki wetu na kutayarisha makundi husika kama tulivyokwishaongea.”

  Baada ya kuagiza ‘mawasiliano kati ya SUKI na Makatibu wa Mikoa’ kuhusu mambo ya kufanya, Dr. Asha-Rose Migiro alimalizia barua yake kwa maneno yafuatayo: “Tafadhali wanakaliwa msisite kutoa maoni, ushauri na mbinu bora zaidi za kutimiza azma yetu katika suala hili muhimu.” ‘Wanakiliwa’ wa barua pepe ya Dr. Asha-Rose Migiro ni pamoja na Mh. Mwigulu Nchemba, Mh. Zakhia Meghji, Mh. Muhamed Seif Khatib na Bw. Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa NEC ya CCM.

  Siku moja baadaye, Nape Nnauye aliwaandikia ‘wanakiliwa’ wenzake kama ifuatavyo: “NASHAURI ikiwezekana kwa sababu ya unyeti wa swala hili tupate taarifa kila siku/au walau siku tatu ya HALI HALISI inavyoendelea katika kila mkoa, ni vizuri idara ikaandaa checklist ya mambo muhimu ya kupima kama mchakato unakwenda vizuri au la! Mfano ... idadi ya walioandaliwa kugombea katika kila eneo, idadi ya waliohamasishwa kuhudhuria na kupiga kura, n.k.”

  Mheshimiwa Spika,

  Njama za CCM kuteka nyara mchakato wa Katiba Mpya zinahusu pia mchakato wa uhalalishaji wa Katiba Mpya kwenye kura ya maoni. Mnamo tarehe 18 Desemba mwaka jana, Katibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Francis K. Mwonga, aliwaandikia barua Makatibu wote wa CCM wa Mikoa kuwapa ‘Maelekezo ya Kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Makatibu wa CCM wa Mikoa Kilichofanyika Dar es Salaam Tarehe 10/12/2012.’

  Sehemu ya Maelekezo hayo inasema: “Wakati wa kupiga kura ya maoni kuhusu Katiba Mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mawasiliano yafanywe na wahusika ili vituo vya kupigia kura visiwe mbali sana na wananchi.” Maneno haya yameandikwa hata kabla Tume haijamaliza zoezi la kukusanya maoni ya wananchi na tayari Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya CCM inawaelekeza makada wake mikoani kufanya mawasiliano na ‘wahusika’ juu ya namna ya kupanga vituo vya kupigia kura.

  Mheshimiwa Spika,

  Kwa mujibu wa kifungu cha 56(a) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi, Sura ya 343 ya Sheria za Tanzania, mamlaka inayohusika kupanga vituo vya kupigia kura ni Msimamizi wa Uchaguzi, yaani Mkurugenzi wa Jiji, Mkurugenzi wa Manispaa, Mkurugenzi wa Mji na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya. Wasimamizi hawa wa uchaguzi wamelalamikiwa kwa miaka mingi na vyama vya upinzani kwa kupendelea CCM na wagombea wake katika chaguzi mbali mbali. Hawa ndio wanaotakiwa wawasiliane na Makatibu wa CCM Mikoa ili wapange vituo vya kupigia kura ya maoni juu ya Katiba Mpya!

  Mheshimiwa Spika,

  Mawasiliano haya ya viongozi wa ngazi za juu za CCM yanathibitisha kwamba mchakato wa Katiba Mpya umeiingiliwa na kuhujumiwa kwa kiasi kikubwa na CCM. Aidha, mawasiliano haya yanathibitisha kauli iliyotolewa mbele ya Bunge lako tukufu na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wakati wa mjadala wa hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba “...viongozi wa kiserikali kama vile Wakuu wa Wilaya na wa Mikoa waliwahamasisha wenyeviti wa vijiji, mitaa na madiwani kuhakikisha kwamba wagombea wote wasiokuwa wa CCM, hasa wa CHADEMA, wanaenguliwa katika chaguzi za vijiji, mitaa au kata.” Aidha, mawasiliano haya yanathibitisha kauli ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kwamba Mabaraza ya Katiba ya Wilaya yaliyochaguliwa kwa utaratibu “...ni mabaraza ya CCM na sio mabaraza ya katiba ya Watanzania wote.”

  Mheshimiwa Spika,

  Yote ambayo tumeyasema hapa yanathibitishwa pia na Tume yenyewe. Tarehe 29 Aprili, 2013 Mwenyekiti wa Tume Jaji Warioba alikiri kwenye mkutano wa waandishi habari kwamba “... sehemu kubwa ya matatizo yaliyojitokeza yalisababishwa na misukumo na misimamo ya kisiasa na kidini.” Mwenyekiti Warioba amekiri kwamba kuna wajumbe wamejazwa katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya: “‘Hao waliojazana kwenye mabaraza wanadhani wanakuja kupiga kura, hapana.... Tume inazingatia uzito wa hoja zilizotolewa na wananchi na si idadi ya watu waliotoa maoni.’” Kwingineko, Mwenyekiti Warioba amekaririwa na vyombo vya habari akikiri kwamba kulikuwa na rushwa katika mchakato wa uchaguzi wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya. Hata hivyo, licha ya kukiri kuwepo kwa matatizo makubwa kama haya katika mchakato wa kuunda Mabaraza hayo, Mwenyekiti Warioba na Tume yake wamekataa madai ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Mabaraza kwa hoja kwamba kufanya hivyo kutachelewesha kupatikana kwa Katiba Mpya!

  Mheshimiwa Spika,

  Kauli ya Mwenyekiti wa Tume ni ya kinafiki na ya kujikosha kutokana na makosa ya Tume yenyewe. Hii ni kwa sababu Tume yake ilitahadharishwa mapema juu ya uwezekano mkubwa wa matatizo hayo kujitokeza. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliitahadharisha Tume mapema mwezi Februari ya mwaka huu kwamba rasimu ya Mwongozo wa Tume itazaa mabaraza ya kiCCM na italeta manung’uniko mengi ya wadau ambao wataenguliwa kwenye ngazi ya WDC ambazo zinatawaliwa na CCM kwa kiasi kikubwa.

  CHADEMA iliishauri Tume iachane na mapendekezo ya kuziweka WDC kuwa ni kikao cha uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya na badala yake wajumbe wa Mabaraza wachaguliwe moja kwa moja na wananchi kama ilivyopendekezwa kwa upande wa Zanzibar. Jaji Warioba na Tume yake walikataa kata kata mapendekezo haya ya CHADEMA. Kama alivyosema Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni: “... (L)icha ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupatiwa maoni ya wadau kwamba utaratibu huo utaharibu mchakato wa Katiba Mpya, Tume ilikataa kata kata kuubadilisha Muundo wa Mabaraza haya. Ni wazi kwamba Tume inafahamu inachokifanya. Ni wazi vile vile kwamba Tume inafahamu matokeo ya hicho inachokifanya, yaani kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ambayo ni ya wanaCCM.”

  Mheshimiwa Spika,

  Jaji Warioba na Tume yake hawawezi wakasikika sasa hivi wakisema kwamba vyama vya kisiasa na taasisi za kidini ndio zenye makosa kwa kuvurugika kwa mchakato wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya! Aidha, Tume iliyotengeneza Mwongozo uliosababisha wanachama wa CCM ‘kujazana’ katika Mabaraza ya Katiba ya Wilaya haiwezi sasa ikalalama na kudai kwamba haitaangalia idadi ya waliotoa maoni bali itaangalia uzito wa hoja! Katika hili Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali iwaeleze Watanzania kama kuna uhalali wowote kutumia shilingi bilioni 4.734 kwa ajili ya kuratibu na kuendesha Mabaraza ambayo Tume imesema maoni ya wengi katika Mabaraza hayo hayatafuatwa.

  Zaidi ya hayo, kukataa kwa Tume kufuta matokeo ya uchaguzi wa Mabaraza ambayo Tume yenyewe inakiri umevurugwa ni uthibitisho tosha kwamba ndivyo Tume ilivyodhamiria tangu mwanzoni. Mabaraza haya ya kiCCM ni matunda ya moja kwa moja ya Tume kukiuka utaratibu uliowekwa na kifungu cha 18(3) cha Sheria ulioilazimu Tume kuunda Mabaraza ambayo “... yatashirikisha na kuwakutanisha wawakilishi toka makundi mbali mbali ya wananchi katika jamii.”

  Mheshimiwa Spika,

  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali itoe kauli mbele ya Bunge lako tukufu kama CCM au viongozi na makada wake wamefanya mawasiliano yoyote na vyombo vitakavyosimamia kura ya maoni juu ya Katiba Mpya kama zinavyoashiria nyaraka za CCM ambazo tumezielezea hapa. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hii ya CCM itoe kauli juu ya uhalali wa mawasiliano haya wakati mchakato wa kutengeneza Katiba Mpya haujakamilika na wala sheria husika za uchaguzi hazijafanyiwa marekebisho ili kuruhusu kura ya maoni kufanyika kihalali, hasa kwa upande wa Tanzania Bara.

  Mheshimiwa Spika,

  Kifungu cha 10 cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba kinafafanua kwamba “Tume itakuwa na mamlaka na uhuru kwa kadri itakavyokuwa muhimu kwa ajili ya utekelezaji wa majukumu na mamlaka yake chini ya Sheria hii na haitaingiliwa na mtu au mamlaka yoyote.” Nyaraka za CCM ambazo tumezielezea hapa zinaonyesha dhahiri kwamba CCM imeingilia uhuru na mamlaka ya Tume. Kwa uchache kabisa, nyaraka hizi zinaonyesha viongozi wa ngazi za juu kabisa wa Sekretarieti ya NEC ya CCM wamefanya makosa ya kula njama kutwaa mamlaka ya Tume kwa kuwatumia Makatibu wa Mikoa wa CCM ‘kusimamia kikamilifu mchakato wa kuundwa kwa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba.’ Kwa mujibu wa kifungu cha 21(2)(b) cha Sheria, “mtu yeyote ... atakayejifanya kuwa mjumbe wa Tume au Sekretarieti ... atakuwa ametenda kosa.” Kifungu cha 21(3) kinaelekeza adhabu ya faini isiyopungua shilingi milioni mbili na isiyozidi shilingi milioni tano au kifungo kwa muda usiopungua mwaka mmoja na usiozidi miaka mitatu au adhabu zote mbili, kwa mtu yeyote atakayepatikana na hatia na kosa hilo. Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inaitaka Serikali hii ya CCM itoe kauli mbele ya Bunge hili tukufu kama iko tayari sasa kuwachukulia hatua tajwa za kisheria Dr. Asha-Rose Migiro, Mh. Mwigulu Nchemba, Mh. Zakia Hamdani Meghji, Mh. Muhamed Seif Khatib, Nape Nnauye na wengine wote waliotajwa katika nyaraka za CCM kwa uhalifu walioufanya dhidi ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

  Mheshimiwa Spika,

  Baada ya ushahidi wote huu, hakuwezi kuwa na ubishi kwamba utaratibu mzima wa kuundwa kwa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya ni haramu. Hakuwezi kuwa na ubishi tena kwamba uharamu huu una lengo moja tu: kuhakikisha kwamba Katiba Mpya itakayopatikana kwa mchakato huu haramu “... itakuwa ni Katiba Mpya kwa jina tu, mambo mengine ya msingi yatabaki vile vile (yalivyo katika Katiba ya sasa). Kwa maneno mengine, itakuwa ni Katiba ile ile, ya watu wale wale, wa chama kile kile.”
   
 17. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #17
  May 3, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,044
  Likes Received: 1,521
  Trophy Points: 280
  Hakuna kitu kipya zaidi kufanya siasa za kivyama bungeni
   
 18. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #18
  May 3, 2013
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 290
  Trophy Points: 180
  Tulitahadharisha watu wa namna hii, wasome kwa makini, wachangie wakiwa na uelewa na hoja iliyoko mezani. Eddie, kaa chini usome tena.
   
 19. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #19
  May 3, 2013
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 21,406
  Likes Received: 13,904
  Trophy Points: 280
  Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ina ushahidi unaoonyesha kwamba njama za kuhakikisha kwamba wanaCCM pekee ndio watakaochaguliwa kuwa wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya kwa upande wa Tanzania Bara zilipangwa katika ngazi za juu kabisa za CCM. Mnamo tarehe 3 Machi, 2013, siku mbili tu baada ya Mwongozo wa Tume kuanza kutumika, Katibu wa NEC ya CCM, Uhusiano wa Kimataifa Dr. Asha-Rose Migiro alituma barua pepe kwa wajumbe na watendaji wa Sekretarieti ya NEC ya CCM yenye kichwa cha habari: ‘MUHIMU!! MABARAZA YA KATIBA YA WILAYA.'

  Barua pepe ya Dr. Asha-Rose Migiro inasema: "Naandika kuhimiza kazi ya kuwatia hamasa Makatibu wa Mikoa wasimamie kikamilifu mchakato wa kuundwa kwa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba. Kama mnavyofahamu Tume ya Katiba imeshatoa taarifa rasmi kwenye vyombo vya habari ... kuhusu zoezi hili muhimu. Sambamba na hatua za awali tulizochukua baada ya kupata rasimu ya mwanzo ya Mwongozo wa Tume, hivi sasa tunatakiwa tuongeze juhudi za ushiriki wetu na kutayarisha makundi husika kama tulivyokwishaongea."

  Nini maoni yako kuhusu hili ''Kamanda''
   
 20. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #20
  May 3, 2013
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,574
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Kuhusu barua pepe ya mama Asha-Rose Migiro:

  Hapa kuna mambo mawili.
  1. Hakuna kosa lolote kwa CCM kuhamasishana kushiriki katika mchakato wa katiba kama jinsi ilivyo si kosa kwa makundi mbalimbali ya kijamii kama NGO, wanaharakati etc. Kwahiyo kama kiongozi wa CM mama Migiro anayo sababu ya kuhamasisha wana CCM kutokujiweka mbali na uundwaji wa mabaraza ya katiba.

  2. CHADEMA wameibuka na mchezo mpya wa kuingilia mawasiliano binafsi ya watu na kutokuon aibu kusema hadharani kuwa wamefanya hivyo.

  CHADEMA inapaswa kutambua kuwa kuingilia mawasiliano binafsi ya watu ni kuvunja sheria za nchi. Hii ni sawa na mtu kusema kuwa "nimeingia chumbani kwa mtu fulani nikafungua kabati lake nimekuta ana shilingi laki mbili, nadhani hizi hela kaziiba". Hapa inabidi uulizwe, wewe umefikaje chumbani kwa mtu na kufungua kabati lake wakati mweyewe hayupo?

  Hii inanikumbusha maisha yetu uswahilini ya nyumba za kupanga. Wapangaji tunatumia jiko la pamoja huku uswahilini. Kuna mpangaji mwezangu chumba cha jirani aliniambia kaka mbona wali wako hujaweka chumvi. Nikashangaa jamaa kajuaje kama mimi sijaweka chumvi?!!!

  Hii ndio tabia waliyoanzisha CHADEMA hivi karibuni...
   
Loading...