Hiyo press conference ya Lema ina makosa mengi sana.Hata ukimuondoa kabisa Mange katika hoja hizi, hayo makosa anayoyasema Mange ya Lema kuomba fadhila kwa Samia kwenye suala la kumtembelea Lissu wengine tulishayaona na kuyaandika hapa kabla Mange hajayasema.
Nimeyarudia tena post #151.
Kwa hiyo hizi si hoja za Mange tu, hata wengine tulishaona hizi contradictions za Lema kabla Mange hajasema.
Kwa hiyo, hata tukiacha kumjadili Mange, makosa ya Lema bado yapo pale pale.
Kuiita wakati huu kabla ya hukumu ya Lissu. Kuwaongelea wanaharakati ambao hawezi kushindana nao, hawana cha kupoteza.
Angalau angejikita kuzungumia Lissu, Mwaipaya, Pambalu kusisitiza umoja, mshikamano na haki kutendeka.
Kuongelea mchango wake mkubwa kuwezesha Lissu na Heche kuwa pale hiyo ni kweli. Mchango wake ni mkubwa ila haikuwa wakati sahihi kuzungumzia ukaribu wake na CCM na serikali kama kitu cha kujivunia.
Focus yake ingetakiwa iwe kwenye hukumu ya Lissu na kuwahamasisha wananchi kwa wingi wao kuhudhuria kesi. Mjadala sasa umehamia kwake Lema na sio kuhusu kesi ya Lissu wiki hii muhimu kuelekea hukumu na kupunguza pressure kwa serikali /mahakama.