Hatari sana, vuguvugu limeanza kwa "kukataa kusikiliza sauti ya mwenyekiti wa chama" na sasa kadi za chama kikongwe kuchomwa moto!
Nilitazama kikao cha Halmashauri Kuu juzi juzi Ikulu nikaona body language ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya chama cha kijani wakiwa hawana tabasamu, raha hata imani na hotuba ya Mwenyekiti wao. Wakati Mwenyekiti alikuwa ''makini kusoma hotuba" kuvutia lakini wajumbe wale wazee walionesha kukataa, kutoridhika, kukosa tumaini, maumivu na kutoafiki uongozi wake kwa body language.