Kaimu Waziri wa Afya- Saada: Sio Ubaguzi. Tatizo kuna watu wanaweka vichwa vya habari wanavyotaka wao

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
1,943
Reaction score
2,982
Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyojitokeza hivi karibuni kuhusu kauli yake juu ya matumizi ya Mfumo wa Matibabu Kadi, huku akisisitiza kuwa mfumo huo umekuwa ukitumiwa vibaya na kuingiza mzigo mkubwa wa gharama kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Akizungumza leo Juni 12, 2026, katika mahojiano maalum na Salim Kikeke wa Crown Media, Waziri Saada Mkuya amefafanua kauli yake iliyotafsiriwa na baadhi ya watu kama ya 'kibaguzi' dhidi ya wakazi wa Tanzania Bara

Waziri Saada amebainisha kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu ambapo watu wasio na sifa (non-entitled) wamekuwa wakipata kadi hizo na kupata huduma za matibabu.

"Matibabu Kadi imekuwa 'abused'. Watu ambao hata hawako 'entitled' wanajikuta wamo kwenye mfumo. Mtu ana uwezo wake, pengine si mkazi wa eneo husika, na hata Sheha hamtambui, lakini anapata Matibabu Kadi na anaenda kupata huduma," amesema Waziri Saada.

Kauli ya Kibaguzi wa Watanzania Bara
Akitolea ufafanuzi madai kuwa kauli yake ililenga kuwabagua watu wa Tanzania Bara wanaotumia vitambulisho vya Taifa (NIDA) visivyotambuliwa rasmi kwenye mfumo huo wa kadi, Waziri Saada amesema maneno yake yalichukuliwa vibaya kutokana na vipande vya video vilivyosambazwa mitandaoni.

Amefafanua kuwa Kitambulisho cha NIDA kinaruhusiwa na kinatumika kujisajili kwenye Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHFS). Hata hivyo, utaratibu wa Matibabu Kadi uliwekwa kama mpito wa muda tu kuelekea mfumo kamili wa ZHFS.

"Unajua unapozungumza, kama hatujakaa mimi na wewe hivi na hivi, maybe wewe utakapondoka hapa utakuwa umenifahamu mimi nini nazungumza. Lakini kwa mtu ambaye kwa clips zile ambazo zilikuwa zikitolewa na kila mtu anakata, kila mtu anakata, kila mtu anatengeneza title yake, kwa mimi it was really fine." amesema Waziri Saada

Amekiri kuwa gharama za uendeshaji wa huduma za afya ni kubwa mno, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasongwa na mzigo mkubwa wa kifedha kutokana na kutoa huduma bila vizuizi au udhibiti thabiti (restrictions).

"Tunawahimiza kila ambapo mtu unakwenda kupeleka matibabu kadi maana yake uwe registered, tuchukue details zako, next time unapokuja tuhakikishe kwamba tayari una ZHFS. Kwa hiyo ule ulikuwa ni temporary, temporary transition mpaka kufikia ile Zanzibar Health Services Fund. Kwa hiyo hiyo imekuwa, lakini sasa gharama za matibabu ni kubwa mno. Sisi kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tunashindwa ku-afford kwamba kila anayekuja ukimpa matibabu kadi alafu anakwenda kupata matibabu alafu hakuna restriction"

Maana ya wazawa na sio wazawa wanafanya kazi ulikuwa una maanisha nini
 
Mpuuzi huyo ......
Na hii kauli haijatoka kwa makusudi , kuna namna ! Wacha tuone !

Ni sawa na yule mmbunge aliyesema kuwa serikalini kuna Yuda "msaliti".... hizi kauli haziji kwa bahati mbaya !

Alafu wote wazenji
 
Kaimu Waziri wa Afya Zanzibar, Saada Mkuya Salum, amefunguka kuhusu sintofahamu iliyojitokeza hivi karibuni kuhusu kauli yake juu ya matumizi ya Mfumo wa Matibabu Kadi, huku akisisitiza kuwa mfumo huo umekuwa ukitumiwa vibaya na kuingiza mzigo mkubwa wa gharama kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Akizungumza leo Juni 12, 2026, katika mahojiano maalum na Salim Kikeke wa Crown Media, Waziri Saada Mkuya amefafanua kauli yake iliyotafsiriwa na baadhi ya watu kama ya 'kibaguzi' dhidi ya wakazi wa Tanzania Bara

Waziri Saada amebainisha kuwa kumekuwa na ukiukwaji mkubwa wa taratibu ambapo watu wasio na sifa (non-entitled) wamekuwa wakipata kadi hizo na kupata huduma za matibabu.

"Matibabu Kadi imekuwa 'abused'. Watu ambao hata hawako 'entitled' wanajikuta wamo kwenye mfumo. Mtu ana uwezo wake, pengine si mkazi wa eneo husika, na hata Sheha hamtambui, lakini anapata Matibabu Kadi na anaenda kupata huduma," amesema Waziri Saada.

Kauli ya Kibaguzi wa Watanzania Bara
Akitolea ufafanuzi madai kuwa kauli yake ililenga kuwabagua watu wa Tanzania Bara wanaotumia vitambulisho vya Taifa (NIDA) visivyotambuliwa rasmi kwenye mfumo huo wa kadi, Waziri Saada amesema maneno yake yalichukuliwa vibaya kutokana na vipande vya video vilivyosambazwa mitandaoni.

Amefafanua kuwa Kitambulisho cha NIDA kinaruhusiwa na kinatumika kujisajili kwenye Mfuko wa Huduma za Afya Zanzibar (ZHFS). Hata hivyo, utaratibu wa Matibabu Kadi uliwekwa kama mpito wa muda tu kuelekea mfumo kamili wa ZHFS.

"Unajua unapozungumza, kama hatujakaa mimi na wewe hivi na hivi, maybe wewe utakapondoka hapa utakuwa umenifahamu mimi nini nazungumza. Lakini kwa mtu ambaye kwa clips zile ambazo zilikuwa zikitolewa na kila mtu anakata, kila mtu anakata, kila mtu anatengeneza title yake, kwa mimi it was really fine." amesema Waziri Saada

Amekiri kuwa gharama za uendeshaji wa huduma za afya ni kubwa mno, na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inasongwa na mzigo mkubwa wa kifedha kutokana na kutoa huduma bila vizuizi au udhibiti thabiti (restrictions).

"Tunawahimiza kila ambapo mtu unakwenda kupeleka matibabu kadi maana yake uwe registered, tuchukue details zako, next time unapokuja tuhakikishe kwamba tayari una ZHFS. Kwa hiyo ule ulikuwa ni temporary, temporary transition mpaka kufikia ile Zanzibar Health Services Fund. Kwa hiyo hiyo imekuwa, lakini sasa gharama za matibabu ni kubwa mno. Sisi kama Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tunashindwa ku-afford kwamba kila anayekuja ukimpa matibabu kadi alafu anakwenda kupata matibabu alafu hakuna restriction"

Huyu ni kiazi mbatata tu, hakuna kitu kichwani. Halafu bidada wakati wa JK amewahi kuwa Naibu Waziri wa Fedha, nilitegemea uzoefu wake kufanya kazi Serikali ya Muungano basi awe mwalimu kwa wengine.

Kuna mahali alisema utatibuje watu milioni 60? Hamna namna anaweza kuji disassociate na "ubaguzi".
 
Mpaka jasho la vidole likutoke mkuya umeyatimbanga. Muungano uvunjike wabaguzi wakubwa nyie.
 
Back
Top Bottom