Kweli mnazungumza kama wenye hekima? "kifo cha furaha"? ndio kipi... kwa hiyo watu wasiende hospitali wafie majumbani kwao kuonesha wanavyojali familia zao? Absurd.
Nzee Mwanakijiji, I salute you Sir! Nadhani umemwelewa vibaya aliyesema hivyo. Anaposema kifo cha furaha ukifia nyumbani bila shaka hakumaanisha kutoenda hospitali. Anamaanisha kwamba Mandela ametibiwa tangu mwanzo kwa kutumia resources za nyumbani kwake South Africa yaani 6M and one S vikiwamo manpower, money, medicine, machinery, materials, moment, na skills akajiaminisha kwamba vyote vimefanya kazi stahiki yenye quality kama ya kokote kwingineko duniani. Iliposhindikana, kila mtu leo anaamini kifo hiki kimeruhusiwa na Mungu mwenyewe kwa kuwa kama jitihada za madaktari walioandaliwa nchini South Africa zilikuwa kubwa sana. Ndio maana hatusikii watu wakilaumu juhudi hafifu ya madaktari kunusuru maisha ya Madiba kipenzi cha duniani pote.
Sitaki kumsemea mleta hoja, lakini a simple psychology if properly applied hata yeye anaguswa na msiba huo sana tu, ila kakuzidi kete kwa kwenda hatua kumi mbele yako, akiangalia sio kifo cha Madiba tu, bali kwamba Madiba kafa kwa kuiheshimu kada ya madaktari walioandaliwa nchini kwake. Hiyo ni furaha kwa Msouth Afrika yeyote na inapaswa kuwa furaha ya kila Mwafrika na iigwe. Kwa nini Bush haji Muhimbili kutibiwa au Gordon kwenda KCMC kutibiwa wakati Sisi viongozi wetu wanakwenda Apollo na London au Massachussets kutibwa magonjwa ambayo hata hukom waendako wanawashangaa kupelekewa minor medial problems which could otherwise be managed here in Chitemo rural Dispensary?
Acha utani bwana hakuna anayefurahia kifo hata kama ni cha adui yako, kwani kuwapo kwa adui katika maisha yako ni kichocheo cha kupevuka kwa akili yako na hata misahafu inatuambia tumwombee adui aendelee kuishi ili ajifunze kwamba Mungu wako anakutetea unapofanikiwa mambo yako. Not absurd lakini huo ndo ukweli, kwamba kuna magonja mengine ni njia halali ambayo Mungu anamuandalia binadamu kama njia ya kuondokea kutoka duniani mtake msitake. Kwani kama Madiba angeendelea kuteswa na ugonjwa wake ndo ingekuwa furaha? Mbona kuna wengine kulekule South Afrika wanakiri kwamba "Acha apumzike baba yetu ameteseka sana, ingawa katuachia majonzi....."? Tuseme sisi wnaJF ndo tujifanye tulimjali zaidi Madiba kuliko walio wa Afrika Kusini?
Kama umewahi kuugza, lazima utaingia kwenye akili ya mleta hoja ukajua uchungu aliokuwa nao akafikiri sana na kufikia alichokiandika. RIP Madiba, lakini Miaka ya binadamu ni 80, zidi ya hapo ni neema tu ya Mungu lakini yaweza kuwa neema yenye machungu kwa mwenye kuishi huko. Kama angekuwa mlalahoi Madiba huenda hata 95 hiyo ingekuwa paukwa pakawa. Tumshukuru Mungu kwa kuushikilia uha wa Madiba hadi 95 ambaye nadhani mazoezi magumu ya kufanyishwa kazi za hovyo kule Robben Island yalimsaidia kuimarisha afya yake. Ndo maana JF ni ya great thinkers ambako ukitumia akili ya juu juu unaweza kutoelewa wachangiaji makini. Mzee Mwanakijiji najua ni kwa sababu ya huzuni uliyo nayo juu ya Madiba ukashindwa kudaka haraka nini mchangiaji anamaanisha, kwani hicho kichwa chako siku zote kimekuwa model kwangu kwa namna unavyofikiri kabla hujaandika, ndo maana nikiona umechangia kitu huwa navuta kiti nakaa vizuri na kusoma kwa makini mawazo yako. Pole kaka, hii ndiyo yenyewe JF unayoifahamu, wote tuko msibani, tuhurumiane tu. Mungu akutie nguvu.