Ardhi ya nyumbani, ama kifo maneno kutoka kwa rais wa Burkina Faso

political monger senior

JF-Expert Member
Nov 26, 2020
1,801
5,788
“ARDHI YA NYUMBANI, AMA KIFO!”

Hotuba iliyotolewa na Rais wa Burkinafaso aliyeingia madarakani kwa kufanya mapinduzi, bwana Ibrahim Traore katika mkutano wa viongozi wa Afrika na Urusi huko St Petersburg, nchini Urusi imevuta hisia zangu kwa karibu.

Ibrahim Traore, anaanza hotuba yake kwa kushukuru kupewa nafasi ya kuhudhuria na kuhutubia mkutano huo, sambamba na kuwaomba samahani wazee (kama Rais Museveni wa Uganda na Paul Biya wa Cameroon) waliokuwepo kwenye mkutano huo kwa swali atakaloliuliza kwa niaba ya vijana wa rika yake.

Ibrahim Traore ndio rais kijana zaidi aliye madarakani Afrika na duniani kwa ujumla, akiwa na miaka 35. Hivyo alichukua jukumu la kutusemea vijana wa Afrika katika mkutano huo, nanukuu...

“I cannot understand why Africa, with its huge mineral resources, water and sun, is the poorest continent where hunger abounds, and why we have to ask for help. We ask these questions, but we are not getting any answers.”

Pamoja na suali hilo lenye mshangao na kukata tamaa ndani yake, nimependa ujasiri wake wa kuonesha njia pia, kwamba Afrika inaweza kuanza upya kwa kuanzisha uhusiano mpya wa usawa na washirika wake wa kimataifa.

Ibrahim Traore anaeleza kuwa,

“ kwa Burkinafaso, kwa miaka 8 mfululizo tumekuwa tukipambana na ushenzi na ukatili kutoka kwa ukoloni na ubepari ambao umelazimisha utumwa mamboleo kwetu."

Traore anaendelea kusema kwamba,

“Sisi, tumejifunza vizuri kitu kimoja, mtumwa asiyepingana na udhalimu anaofanyiwa, hastahiki chochote zaidi ya huruma na maisha yake ya mbeleni yapo mashakani"

Sentensi hizo za Traore zina kusudia kuengeza muamko kwa mataifa ya Afrika kupambana na ukoloni mamboleo na kujikwamua kiuchumi.

Ibrahim Traore anawanyooshea vidole vya shutuma juu ya kuwa vibaraka na uzandiki wa viongozi wa Afrika wa kutowaunga mkono wenzao wanaopambana na ubepari na badala yake, wanawadunisha. Nanukuu...

“The problem is not when people decide to take up arms. The problem is that the leaders of African countries do not bring anything to people fighting imperialism, calling us armed groups or criminals. We do not agree with this approach. We, the heads of African states, must stop acting as puppets ready to act whenever the imperialists pull the strings.”

Ibrahim Traore anawapasha viongozi wa Afrika kuwa,

“Siku ya jana, Rais Vladimir Putin alitangaza msaada wa nafaka kwa Afrika. Viongozi wa Afrika tumeonesha kufurahia sana na kushukuru. Hatua hio inatuma ujumbe pia kwa viongozi wa Afrika ni lazima tuhakikishe katika mkutano ujao, nchi zetu zinajitosheleza kwa chakula.”

Huku akitoa ushauri
“We must rely on the experience of African countries who have been able to achieve this objective and reinforce our cooperation in this field by strengthening our relations with the Russian Federation in order to meet the needs of our people.”

Mwisho, Ibrahim Traore anamalizia hotuba yake,

“Ushindi kwa mataifa yetu! Hadhi na heshima kwa mataifa yetu!...Ardhi ya nyumbani ama kifo!”

Naam, maneno hayo yanasadiki kiu ya waAfrika kupata hadhi na heshima wanayostahiki katika jamii ya kimataifa, pamoja na ukombozi na uhuru wa kiuchumi.

#political monger
 
Kukubali kuwa vibaraka ni sisi wenyewe ila siku tutashiba continent lote na kusaidiana wenyewe kwa wenyewe basi ndio siku tutajikomboa

Kuna viongozi wanafurahia kufa njaa kwa majirani badala ya kushikamana na kuwasaidia, wanawauzia mahindi

Kweli ni biashara lakini serikali haiwezi kutoa Tani kadhaa na kuwapa wenye uhitaji?
Mzungu anakupa mkopo au chakula huku ukifurahia je Bara letu ni vilema?
 
Mkuu Mtoa Post, maneno yaliyosemwa na huyo "Rais Kijana" sio mageni humu Afrika. Nafikiri Mzee Musebeni (Luganda Pronunciation) na Mzee Paul Biya hawakushangazwa na kauli zake hizo kwasababu hata wao walipoingia madarakani enzi zao walizisema.

Kwao hiyo sio 'a moving speech'. Ila kwa vijana kama wewe na ambao hamsomi Historia ya Afrika vizuri, endeleeni kuifurahia.
 
"Africa's time of slavery to western regimes is over and the battle for full independence has begun either homeland or death"

Reincarnation of Thomas Sankara.
FB_IMG_1691948453552.jpg


Sent from my Infinix X657B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom