Maana yake viongozi jengeni na imarisheni huduma za afya kwenu
Hapo umenena Mkuu !!
Maana yake viongozi jengeni na imarisheni huduma za afya kwenu
Sawa lakini huduma ya hospitali za Afrika Kusini alizijenga Mandela? Je Waafrika wote wa Afrika ya Kusini wanapata huduma hizo bora na hivyo hawaendi nje ya Afrika ya Kusini kupata tiba? Na wakiamua kwenda kupata tiba nje ina maana hawana uzalendo.
Mandela kazi yake kubwa na aliikamilisha ilikuwa ni kumaliza au kukomesha ubaguzi wa rangi ingawa hata Wasouth Africa weusi ni wabaguzi sasa hivi kuliko wazungu.
Sawa lakini huduma ya hospitali za Afrika Kusini alizijenga Mandela? Je Waafrika wote wa Afrika ya Kusini wanapata huduma hizo bora na hivyo hawaendi nje ya Afrika ya Kusini kupata tiba? Na wakiamua kwenda kupata tiba nje ina maana hawana uzalendo.
mkuu unamaanisha hata kama Mandela amefia nyumbani hana tofauti na viongozi wengine wanaofia Ulaya.?
sababu ni kwamba huduma alizohudumiwa nyumbani sio yeye alieziboresha.!
Ni furaha kuona kwamba baba wa taifa anafia nyumbani kwake. Nchi zetu hizi viongozi wetu wanafia ulaya, India, S. Africa.
Kwa Mandela hiyo ni ishara ya nchi iliyo timamu. Iliyojengwa Kuwa nchi badala ya kujiandaa kuomba omba. Tusubiri msafara wa mazishi.
Nelson Mandela ana kila sababu za kutofia India au Uingereza kwa sababu nchi aliyoijenga haina tofauti kabisa na nchi yoyote ya dunia yakwanza, south Afrika ni kama ulaya tu.
Maskini kama Tz ndio hatutibiwi kwetu tunakimbilia nnje kwa kuwa tunajua kuwa Muhimbili ni hospitali kanjanja,
.
Mungu bariki Mandela
Nilichotaka ni kumwambia ukweli ambao ndio nilioelekeza mpaka mstari wa mwisho, sikuwa na nia ya kumkandia bali kumpa changamoto.Umemwambia vizuri mwisho unaanza kumrembaremba.
Ndio maana nasema tumejenga taifa la watu wasiojua kufikiri vizuri; wanafikiri wanajenga hoja kumbe wanatengeneza absurdities zisizo za lazima kabisa. Unamsifia Mandela kwa kufia nyumbani kwake - well kwa juu juu watu wanaweza kuona umesema kitu lakini kwa kweli ni an irrational argument. Kwani huduma za afya za Afrika ya Kusini zilijengwa na Mandela?
Hoja ya kusema kuweka posho na marupurupu kwenda nje hiyo nakubaliana na wewe kabisa. Lakini si watu hawa hawa wamechaguliwa na sisi na tunajua kuwa tunapowachagua tumewapa na hilo vile vile? Kama suala ni taifa kulipia viongozi kwenda kutibiwa nje hiyo ni hoja nyingine kabisa; lakini kama kiongozi ana fedha zake na kwa uwezo wake kwanini asiende kutibiwa nje? Kama mauti yakamkuta huko nje kwanini anaonekane si mzalendo? Kwani anayekufa ulaya na anayekufa Maneromango yupi anakuwa amekufa sana?
It is silly argument. Ukitaka kuzungumzia suala la kugharimia matibabu ya viongozi nje lete hiyo hoja.
..............................................
Inaonesha ndugu zetu hata historia yetu ya nchi hawaijui au wameisahau. Baada ya miaka zaidi ya 40 ya ukoloni wakati wa Uhuru Nyerere aliiachiwa madaktari wazalendo 2; na wahandisi wazalendo 12. Hospitali kubwa zote zilikuwa za misheni, sehemu nyingi hakukuwa na kliniki wala vituo vya maana vya afya. Hatujazungumzia manesi n.k. Hapa pia hatujazungumzia hali ya elimu ilivyokuwa; hatujazungumzia barabara, nishati, n.k .