Mandela-Kifo cha furaha nyumbani siyo Ulaya

MchunguZI

JF-Expert Member
Jun 14, 2008
4,006
2,165
Ni furaha kuona kwamba baba wa taifa anafia nyumbani kwake. Nchi zetu hizi viongozi wetu wanafia ulaya, India, S. Africa.

Kwa Mandela hiyo ni ishara ya nchi iliyo timamu. Iliyojengwa Kuwa nchi badala ya kujiandaa kuomba omba. Tusubiri msafara wa mazishi.
 
Kweli ni fahari Sana kwa South Africa sie baba wa taifa la hip hop Tanzania cow Obama kafia south
 
Hapa kwetu ni aibu, nenda national hospital (muhimbili) hatari tupu! Alafu wanakimbilia kujenga daraja kigamboni kwa bl 200 wakati hakuna huduma bora za afya..
 
Ni fahari kubwa sana kufia nyumbani hasa ukiwa unaona umuhimu wa kwenu. Tatizo letu hatujui maana ya uzalendo na vipaumbele. Ni rahisi kuimba uzalenda ila madaraka yanaharibu sana Waafrika sijui wana kitu gani kichwani.

Vipaumbele vya muhimu katika ustawi wa Taifa lolote lile ni Elimu na afya. Na hauwezi kuviendeleza kama fungu kubwa la Taifa linapekekwa nje ama kusomesha ama matibabu. Gharama wizara ya afya, serikali, mashirika ya umma inayotumia kwa mwaka kupeleka watu kutibiwa nje inatosha kuajiri madaktari bingwa kutoka sehemu yeyote ile duniani na kuwa na vifaa vya kisasa kabisa walau kwa Hospitali moja Tanzania na kutoa kabisa rufaa za nje.

Ila tunazalisha viongozi na watawala wachumia matumbo, wanatibiwa malaria India, meno uingereza, macho Germany, Kupumzika Sweeden. Ukiwauliza wanakurupuka na kujiita wazelando.
 
Ni furaha kuona kwamba baba wa taifa anafia nyumbani kwake. Nchi zetu hizi viongozi wetu wanafia ulaya, India, S. Africa.

Kwa Mandela hiyo ni ishara ya nchi iliyo timamu. Iliyojengwa Kuwa nchi badala ya kujiandaa kuomba omba. Tusubiri msafara wa mazishi.

Ni kweli ulichosema, ila hata Nyerere hakwenda kufia Ulaya, aliondoka kwa minajili ya kwenda kufanya check-up. Angelijua kuwa atakufa wala asingeenda, angebaki Butiama kifo kingemkuta akiwa Butiama.
 
Ni kweli ulichosema, ila hata Nyerere hakwenda kufia Ulaya, aliondoka kwa minajili ya kwenda kufanya check-up. Angelijua kuwa atakufa wala asingeenda, angebaki Butiama kifo kingemkuta akiwa Butiama.


Usimlishe maneno, nani kakuambia hayo? Kwa nini asichekiwe nyumbani? Mandela ni shujaa kwa vitu vingi sana! Purely African!
 
Kweli mnazungumza kama wenye hekima? "kifo cha furaha"? ndio kipi... kwa hiyo watu wasiende hospitali wafie majumbani kwao kuonesha wanavyojali familia zao? Absurd.
 
Ni kweli ulichosema, ila hata Nyerere hakwenda kufia Ulaya, aliondoka kwa minajili ya kwenda kufanya check-up. Angelijua kuwa atakufa wala asingeenda, angebaki Butiama kifo kingemkuta akiwa Butiama.

kwani hospital za Tanzania hawafanyi check up?
je raia wengine wa kawaida wakafanye wap check up au wangoje kufa tu?
 
Sidhani kama amesema wasiende hospitali!

that is the implication; kwamba mgonjwa asitafute matibabu anapoweza kupata matibabu; kama watu wanaenda India kutibiwa; wanaenda kwa waganga kutibiwa; wanaenda Kenya, Afrika ya Kusini, UIngereza n.k na wengine wanaweza kwenda Mwananyamala wakati wengine wanaenda Aga Khan; mgonjwa anapotafuta kutibiwa atibiwe kwenye hospitali za serikali tu kuonesha uzalendo?

Wengi wenye kuitoa hoja wanachotaka kusema ni kuwa huduma zetu za afya ni duni sana kwa sababu Nyerere hakuziimarisha vinginevyo na yeye angefia Tanzania kuonesha kuwa ametumia huduma zetu. Watu hawa wenye hoja dhaifu wanasahau kuwa huduma ya Afya ya Afrika Kusini ambayo Mandela amepewa watu wengi hawaipiti huko na siyo Mandela aliyeijenga! Ilijengwa na makaburu! Kama angeenda kufia kwenye hospitali ya Soweto au Kwazul Natal watu wangesema hivyo - kwamba atoke ile hospitali ya kisasa iliyojengwa wakati wa utawala wa Kikaburu na kwenda Soweto kuonesha umoja wake na watu wao!

Ni hoja isiyofikiriwa sana. Lakini wanaotoa hoja hii hawaendi mbali zaidi; kwani huduma gani Tanzani aimekuwa nzuri zaidi tangu Nyerere kaondoka? Elimu analaumiwa yeye; barabara analaumiwa yeye, umeme analaumiwa yeye; sasa kama Nyerere angetatua matatizo yote ya kiuchumi, kijamii na kimaisha ya Tanzania hawa wanaoitwa viongozi wangetafuta uongozi ili wafanye nini (wakati vyote vimeshafanywa na Nyerere)? TUmejenga taifa la watu wanaotaka kudekezwa na kudeka; "Baba hakutuachia nyumba".. alaaah! kawaachia ardhi jengeni!
 
Kweli mnazungumza kama wenye hekima? "kifo cha furaha"? ndio kipi... kwa hiyo watu wasiende hospitali wafie majumbani kwao kuonesha wanavyojali familia zao? Absurd.

Limekugusa mzee mzima!Come back home njoo utafute riziki nyumbani.Mzalendo halisi ni nyumbani sio ugenini.
 
Kweli mnazungumza kama wenye hekima? "kifo cha furaha"? ndio kipi... kwa hiyo watu wasiende hospitali wafie majumbani kwao kuonesha wanavyojali familia zao? Absurd.
Nzee Mwanakijiji, I salute you Sir! Nadhani umemwelewa vibaya aliyesema hivyo. Anaposema kifo cha furaha ukifia nyumbani bila shaka hakumaanisha kutoenda hospitali. Anamaanisha kwamba Mandela ametibiwa tangu mwanzo kwa kutumia resources za nyumbani kwake South Africa yaani 6M and one S vikiwamo manpower, money, medicine, machinery, materials, moment, na skills akajiaminisha kwamba vyote vimefanya kazi stahiki yenye quality kama ya kokote kwingineko duniani. Iliposhindikana, kila mtu leo anaamini kifo hiki kimeruhusiwa na Mungu mwenyewe kwa kuwa kama jitihada za madaktari walioandaliwa nchini South Africa zilikuwa kubwa sana. Ndio maana hatusikii watu wakilaumu juhudi hafifu ya madaktari kunusuru maisha ya Madiba kipenzi cha duniani pote.

Sitaki kumsemea mleta hoja, lakini a simple psychology if properly applied hata yeye anaguswa na msiba huo sana tu, ila kakuzidi kete kwa kwenda hatua kumi mbele yako, akiangalia sio kifo cha Madiba tu, bali kwamba Madiba kafa kwa kuiheshimu kada ya madaktari walioandaliwa nchini kwake. Hiyo ni furaha kwa Msouth Afrika yeyote na inapaswa kuwa furaha ya kila Mwafrika na iigwe. Kwa nini Bush haji Muhimbili kutibiwa au Gordon kwenda KCMC kutibiwa wakati Sisi viongozi wetu wanakwenda Apollo na London au Massachussets kutibwa magonjwa ambayo hata hukom waendako wanawashangaa kupelekewa minor medial problems which could otherwise be managed here in Chitemo rural Dispensary?

Acha utani bwana hakuna anayefurahia kifo hata kama ni cha adui yako, kwani kuwapo kwa adui katika maisha yako ni kichocheo cha kupevuka kwa akili yako na hata misahafu inatuambia tumwombee adui aendelee kuishi ili ajifunze kwamba Mungu wako anakutetea unapofanikiwa mambo yako. Not absurd lakini huo ndo ukweli, kwamba kuna magonja mengine ni njia halali ambayo Mungu anamuandalia binadamu kama njia ya kuondokea kutoka duniani mtake msitake. Kwani kama Madiba angeendelea kuteswa na ugonjwa wake ndo ingekuwa furaha? Mbona kuna wengine kulekule South Afrika wanakiri kwamba "Acha apumzike baba yetu ameteseka sana, ingawa katuachia majonzi....."? Tuseme sisi wnaJF ndo tujifanye tulimjali zaidi Madiba kuliko walio wa Afrika Kusini?

Kama umewahi kuugza, lazima utaingia kwenye akili ya mleta hoja ukajua uchungu aliokuwa nao akafikiri sana na kufikia alichokiandika. RIP Madiba, lakini Miaka ya binadamu ni 80, zidi ya hapo ni neema tu ya Mungu lakini yaweza kuwa neema yenye machungu kwa mwenye kuishi huko. Kama angekuwa mlalahoi Madiba huenda hata 95 hiyo ingekuwa paukwa pakawa. Tumshukuru Mungu kwa kuushikilia uha wa Madiba hadi 95 ambaye nadhani mazoezi magumu ya kufanyishwa kazi za hovyo kule Robben Island yalimsaidia kuimarisha afya yake. Ndo maana JF ni ya great thinkers ambako ukitumia akili ya juu juu unaweza kutoelewa wachangiaji makini. Mzee Mwanakijiji najua ni kwa sababu ya huzuni uliyo nayo juu ya Madiba ukashindwa kudaka haraka nini mchangiaji anamaanisha, kwani hicho kichwa chako siku zote kimekuwa model kwangu kwa namna unavyofikiri kabla hujaandika, ndo maana nikiona umechangia kitu huwa navuta kiti nakaa vizuri na kusoma kwa makini mawazo yako. Pole kaka, hii ndiyo yenyewe JF unayoifahamu, wote tuko msibani, tuhurumiane tu. Mungu akutie nguvu.
 
Kweli mnazungumza kama wenye hekima? "kifo cha furaha"? ndio kipi... kwa hiyo watu wasiende hospitali wafie majumbani kwao kuonesha wanavyojali familia zao? Absurd.

Anaeleweka mzee isipokuwa wewe umemchukulia literally badala ya literary
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom