Katika hali isiyo ya kawaida, Rais Barack Obama ambaye nchi yake bado imeng'ang'ania kuiwekea Cuba vikwazo kibao, leo wamesalimiana tena kwa kukumbatiana mbele ya hadhara ya dunia (kupitia luninga)! Nina hakika hili lisingewezekana wakati wa utawala wa George Bush! Hii ni dalili kwamba yawezekana kabisa iko siku, tena si nyingi, Marekani itaondoa vikwazo vyake dhidi ya Cuba vilivyodumu kwa miaka mingi tangu enzi za Fidel Castro (kakake Castro-Rais wa sasa).