Vikwazo dhidi ya Zimbabwe vyapaswa kuondolewa mara moja

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,034
VCG111407046289.jpg
Tarehe 25 Oktoba ni “Siku ya Kupinga Vikwazo” iliyoanzishwa na Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC). Katika maadhimisho ya Siku hiyo, viongozi wa nchi nyingi kwa mara nyingine tena wametoa wito wa kuondolewa kwa vikwazo dhidi ya Zimbabwe.

China pia imesisitiza kuwa, Marekani na nchi nyingine za magharibi zinapaswa kuondoa vikwazo haramu dhidi ya Zimbabwe haraka iwezekanavyo, ili kumaliza maafa ya kibinadamu yanayosababishwa na vikwazo hivyo.

Oktoba 25, Makamu wa Rais wa Zimbabwe Constantino Chiwenga alitoa hotuba mjini Harare kwa niaba ya Rais Emmerson Mnangagwa ambaye alikuwa nje ya mji wa Harare, akilaani vikali vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Zimbabwe na nchi chache za Magharibi ikiwa ni pamoja na Marekani, na kutaka vikwazo hivyo viondolewe mara moja na bila masharti.

Chiwenga alibainisha kuwa vikwazo hivyo haramu vimezuia maendeleo endelevu ya Zimbabwe, na kudhuru uhuru na mamlaka ya Zimbabwe.

Tarehe 21 Disemba mwaka 2001, Rais wa wakati huo wa Marekani George W. Bush aliidhinisha “Sheria ya Kufufuka kwa Demokrasia na Uchumi Nchini Zimbabwe”, na kuanza kuiwekea Zimbabwe vikwazo visivyo halali vilivyodumu kwa zaidi ya miaka 20 sasa.

Vikwazo hivyo vimeharibu sana uwezo wa Zimbabwe wa kuendeleza uchumi na kuboresha maisha ya watu, na kuzuia juhudi za kanda ya kusini mwa Afrika kuimarisha ushirikiano na kupata maendeleo ya pamoja. Kwa mujibu wa takwimu zisizo rasmi, hasara za kiuchumi zilizosababishwa na vikwazo hivyo kwa Zimbabwe imezidi dola bilioni 40 za kimarekani.

Mbali na athari mbaya kwa uchumi, vikwazo hivyo pia vimeathiri vibaya haki za binadamu za watu wa Zimbabwe, ikiwa ni pamoja na haki za kuishi, kupata chakula, afya, maendeleo, elimu na haki nyingine za binadamu. Baadhi ya Wazimbabwe waliuliza kwa hasira kama wataendelea kuvumilia kwa miaka 20 zaidi?

Vikwazo vya muda mrefu vilivyowekwa na Marekani na nchi nyingine za Magharibi vimekiuka kwa kiasi kikubwa mamlaka ya Zimbabwe, kuharibu haki ya maendeleo ya watu wa Zimbabwe, na kukiuka kanuni za msingi za uhusiano wa kimataifa.

Kwa muda mrefu, China imesimama pamoja na nchi za Afrika na pande nyingine za haki, kupinga vikali vikwazo hivyo haramu, na kuunga mkono Zimbabwe kupinga uingiliaji wa nje na kutafuta njia ya kujipatia maendeleo.

Wakati wa mjadala mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wa mwaka huu, viongozi wengi wa nchi na mashirika ya kimataifa wametoa sauti hadharani, wakitaka Marekani na nchi nyingine zinazohusika zirekebishe vitendo vyao potovu na kuondoa mara moja vikwazo dhidi ya Zimbabwe.

Katika miaka ya hivi karibuni, Marekani na nchi nyingine za Magharibi zimedai kwamba zinataka kuzisaidia nchi za Kiafrika kujiendeleza, lakini kwa upande mwingine, zinashikilia fimbo ya kuweka vikwazo dhidi ya nchi za Afrika. Marekani na nchi nyingine za Magharibi zinapaswa kuondoa mara moja vikwazo dhidi ya Zimbabwe, ili kurejesha haki kwa Zimbabwe na dunia nzima.
 
US kila sehemu ni mvurugaji ilimradi kila nchi iwe mikononi mwake!
 
Zimbabwe shida ni wizi wa kura na kuwaua wapinzani kwa chama kinachotawala cha ZANU-PF ndilo chimbuko la kuwekewa vikwazo. Ila kuna ubaguzi fulani hivi maana haya ninayaona Uganda na Rwanda lakini sijasikia wakiwekewa vikwazo.
 
Back
Top Bottom