TANZIA Harry Belafonte, mwimbaji, mwigizaji na mwanaharakati, afariki akiwa na umri wa miaka 96

balibabambonahi

JF-Expert Member
Apr 5, 2015
14,456
12,581
Nakumbuka nilipata kufahamu habari za mtu huyu kupitia JF hasa kwa kazi adhimu ya Mzee Mohamed Said.Mwanazuoni MS aliandika mengi kumhusu Belafonte, Leo nimesoma mahala kadhaa kwamba nguli huyu kaumaliza mwendo wa safari yake hapa chini ya jua. Nimuombe Mzee MS, amwandike japo kwa uchache.

Natanguliza shukrani zangu kwa Mzee Mohamed Said.

Kumradhi.

==========

Harry Belafonte, singer, actor and tireless activist, dies aged 96​


GettyImages-621734964-1920x1080-12706493.jpg

Harry Belafonte, the singer, actor and civil rights activist who broke down racial barriers, has died aged 96.
As well as performing global hits such as Day-O (The Banana Boat Song), winning a Tony award for acting and appearing in numerous feature films, Belafonte spent his life fighting for a variety of causes. He bankrolled numerous 1960s initiatives to bring civil rights to Black Americans; campaigned against poverty, apartheid and Aids in Africa; and supported leftwing political figures such as Cuba’s Fidel Castro and Venezuela’s Hugo Chavez.

The cause of death was congestive heart failure, his spokesman told the New York Times. Figures including Joe Biden, the rapper Ice Cube and Mia Farrow paid tribute to Belafonte. The US president said Belafonte was a “groundbreaking American who used his talent and voice to help redeem the soul of our nation”.

“Harry Belafonte’s accomplishments are legendary and his legacy of outspoken advocacy, compassion, and respect for dignity will endure forever,” Biden said on Twitter.

The US news anchor Christiane Amanpour tweeted that he “inspired generations around the whole world in the struggle for non-violent resistance justice and change. We need his example now more than ever.”

Bernice King, daughter of Dr Martin Luther King, shared a picture of Belafonte at her father’s funeral and said that he “showed up for my family in very compassionate ways. In fact, he paid for the babysitter for me and my siblings.” The Beninese-French musician Angélique Kidjo called Belafonte “the brightest star in every sense of that word. Your passion, love, knowledge and respect for Africa was unlimited.”

Belafonte was born in 1927 in working-class Harlem, New York, and spent eight years of his childhood in his impoverished parents’ native Jamaica. He returned to New York for high school but struggled with dyslexia and dropped out in his early teens. He took odd jobs working in markets and the city’s garment district, and then signed up to the US navy aged 17 in March 1944, working as a munitions loader at a base in New Jersey.

After the war ended, he worked as a janitor’s assistant, but aspired to become an actor after watching plays at New York’s American Negro Theatre (along with fellow aspiring actor Sidney Poitier). He took acting classes – where his classmates included Marlon Brando and Walter Matthau – paid for by singing folk, pop and jazz numbers at New York club gigs, where he was backed by groups whose members included Miles Davis and Charlie Parker.

He released his debut album in 1954, a collection of traditional folk songs. His second album, Belafonte, was the first No 1 in the new US Billboard album chart in March 1956, but its success was outdone by his third album the following year, Calypso, featuring songs from his Jamaican heritage. It brought the feelgood calypso style to many Americans for the first time, and became the first album to sell more than a million copies in the US.

The lead track was Day-O (The Banana Boat Song), a signature song for Belafonte – it spent 18 weeks in the UK singles chart, including three weeks at No 2. His version of Mary’s Boy Child was a UK chart-topper later that year, while Island in the Sun reached No 3. He released 30 studio albums, plus collaborative albums with Nana Mouskouri, Lena Horne and Miriam Makeba. The latter release won him one of his two Grammy awards; he was later awarded a lifetime achievement Grammy and the Academy’s president’s merit award.

Bob Dylan’s first recording – playing harmonica – was on Belafonte’s 1962 album, Midnight Special. The previous year, Belafonte had been hired by Frank Sinatra to perform at John F Kennedy’s presidential inauguration.

A lifetime of activism … Belafonte with Martin Luther King Jr.

A lifetime of activism … Belafonte with Martin Luther King Jr. Photograph: Hulton Archive/Getty Images
Belafonte maintained an acting career alongside music, winning a Tony award in 1954 for his appearance in the musical revue show, John Murray Anderson’s Almanac, and appearing in several films, most notably as one of the leads in Island in the Sun, along with James Mason, Joan Fontaine and Joan Collins, with whom he had an affair. He was twice paired with Dorothy Dandridge, in Carmen Jones and Bright Road, but he turned down a third film, an adaptation of Porgy and Bess, which he found “racially demeaning”.

He later said the decision “helped fuel the rebel spirit” that was brewing in him, a spirit he parlayed into a lifetime of activism, using his newfound wealth to fund various initiatives. He was mentored by Martin Luther King Jr and Paul Robeson, and bailed King out of a Birmingham, Alabama, jail in 1963 as well as co-organising the march on Washington that culminated in King’s “I have a dream” speech. He also funded the Freedom Riders and SNCC, activists fighting unlawful segregation in the American south, and worked on voter registration drives.

He later focused on a series of African initiatives. He organised the all-star charity record We Are the World, raising more than $63m for famine relief, and his 1988 album, Paradise in Gazankulu, protested against apartheid in South Africa. He was appointed a Unicef goodwill ambassador in 1987, and later campaigned to eradicate Aids from Africa.

After recovering from prostate cancer in 1996, he advocated for awareness of the disease.

He was a fierce proponent of leftwing politics, criticising hawkish US foreign policy, campaigning against nuclear armament, and meeting with both Castro and Chavez. At the meeting with Chavez, in 2006, he described US president George W Bush as “the greatest terrorist in the world”. He also characterised Bush’s Black secretaries of state Colin Powell and Condoleezza Rice as being like slaves who worked in their master’s house rather than in the fields, criticisms that Powell and Rice rejected.

He was a frequent critic of Democrats, particularly Barack Obama, over issues including Guantanamo Bay detentions and the fight against rightwing extremism. He criticised Jay-Z and Beyoncé in 2012 for having “turned their back on social responsibility … Give me Bruce Springsteen, and now you’re talking. I really think he is Black.” Jay-Z responded: “You’re this civil rights activist and you just bigged up the white guy against me in the white media … that was just the wrong way to go about it.”

Harry Belafonte explains how his mother inspired him into activism – video
He continued to take occasional acting roles. In 2018, he appeared in the Spike Lee movie BlacKkKlansman. In 2014, 12 Years a Slave director Steve McQueen announced he was working with Belafonte on a film about Paul Robeson, though it wasn’t developed.

Belafonte was married three times, first to Marguerite Byrd, from 1948 to 1957, with whom he had two daughters, activist Adrienne and actor Shari. He had two further children with his second wife, Julie Robinson: actor Gina and music producer David. He and Robinson divorced after 47 years, and in 2008 he married Pamela Frank, who survives him.

Source: theguardian.com
 
Nakumbuka nilipata kufahamu habari za mtu huyu kupitia JF hasa kwa kazi adhimu ya Mzee Mohamed Said.Mwanazuoni MS aliandika mengi kumhusu Belafonte,Leo nimesoma mahala kadhaa kwamba nguli huyu kaumaliza mwendo wa safari yake hapa chini ya jua.Nimuombe Mzee MS ,amwandike japo kwa uchache.Natanguliza shukrani zangu kwa Mzee Mohamed Said.Kumradhi.
HARRY BELAFONTE
(1927 - 2023)
(1)
Nimeandika makala kadhaa ambazo ndani yake nimemtaja Harry Belafonte ambae mimi nimesikiza muziki wake nikiwa na umri wa miaka mitano.

Makuzi yangu na vijana wengi tuliozaliwa miaka ya 1950 tulipitia maisha ya ''wazimu'' ambayo wengi wetu tukiangalia nyuma tunabakia kutingisha kichwa.
Harry Belafonte amefariki jana tarehe 24 April nyumbani kwake Manhattan, New York.

Nakumbuka siku moja niko katika kihoteli kidogo Manhattan pembeni ya Hudson River, mwenyeji wangu akaniambia kuwa tukivuka huo mto tutafika nyumbani kwa Harry Belafonte.

Bahati mbaya hawakuwa wanafahamiana kwa hiyo hakuweza kunipeleka kwake.

Naweka hapo chini baadhi ya makala ambazo nimeandika kuhusu Harry Belafonte:

HARRY BELAFONTE NA SIDNEY POITIER NYUMBANI KWA HAMZA AZIZ
Hamza Aziz kazaliwa Mtaa wa Kipata mtaa ambao mimi nimezaliwa.

Babu yangu Salum Abdalah alikuwa na nyumba Mtaa wa Mbaruku jirani na nyumba ya Aziz Ali baba yake Hamza na Dossa Aziz.

Kwa ajili hii Hamza Aziz wamejuana na baba yangu toka udogoni kwao.

Hamza Aziz kwangu alikuwa baba na rafiki na tukizungumza mengi sana hadi alipotangulia mbele ya haki tulikuwa hivi.

Jana niliweka picha ya Harry Belafonte na Sidney Poitier na nikasema kuwa watu hawa maarufu walikuwa nyumbani kwa Ally Sykes.

Rose Aziz bint ya Hamza Aziz jana usiku kaniletea ujumbe baada ya kuona picha ile na kunifahamisha kuwa pale ni nyumbani kwao Msasani na baba yake ndiye siku hiyo aliyewaalika Harry Belafonte na Sidney Poitier nyumbani kwao pamoja na Ally Sykes na John Malecela.

Kwenye picha ya kwanza John Malecela amekaa pembeni ya Sidney Poitier.

Naweka hapa picha za siku hiyo adhimu wakati Harry Belafonte na Sidney Poitier walipokuwa wageni wa Hamza Aziz nyumbani kwake Msasani.

Rose amenieleza kuwa Hamza Aziz alikutana tena na Harry Belafonte Canada na Sidney Poitier Marekani na wakabakia kuwa marafiki wa karibu.

Mzee Hamza Aziz mimi na yeye tukimpenda Nat King Cole na akanieleza kuwa katika ujana wake akiziimba nyimbo zake.

Siku moja aliniimbia nyimbo ya Nat King Cole, ''I Love You For Sentimental Reasons.''

Abbas Sykes na Hamza walikuwa marafiki wakubwa sana.

Balozi Sykes alikuwa akimtania Hamza Aziz kwa kumwita jina lake la utani ''Nat King Cole'' akilifupisha kwa kumwita ''Nat.''

Hamza Aziz na yeye akimwita Balozi Sykes ''Spencer Tracey'' jina la muigizaji maarufu katika miaka ya 1950 hadi 1960.

Mwenyezi Mungu awarehemu wazee wetu hawa.

Picha tatu za chini kulia ni Hamza Aziz, Sidney Poitier na Harry Belafonte.

343120564_590232099748917_490777644715919044_n.jpg
343295991_619206050080405_8972071852745468175_n.jpg

343422558_228986753111216_1218512226689167750_n.jpg

343295574_1405669953502355_2555643305488555626_n.jpg

343296047_128866110171629_5259426512539183182_n.jpg
 
Nimekusoma Maalim,nimefarijika sana.
HARRY BELEFONTE MIAKA 96 (2)
Miaka ya mwanzoni 1970s nilikuwa napita nje ya ofisi ya British Airways wakati huo Independence Avenue sasa Samora Avenue.

Mbele yangu nikawaona Harry Belafonte na Sidney Poitier wanatoka katika ofisi hiyo.

Nikawasogelea karibu nikawasalimia na kuomba autograph zao.

Nilikuwa sina karatasi nikatoa kitambulisho changu cha East African Cargo Handling Services wakaweka saini zao nyuma ya kitambulisho changu.

Nakumbuka nyimbo yangu ya kwanza kuisikia ya Harry Belafonte ilikuwa, "Round the Bay of Mexico," ikipigwa katika radio.

Ilikuwa mwaka wa 1957 nakaa Mtaa wa Kiungani Gerezani kwa mama yangu mkubwa Bi. Mwanaisha bint Mohamed.

Jirani yetu kwenye kona ya Mtaa wa Kiungani na Mtaa wa Sikukuu ilikuwa nyumba ya Mashado Plantan.

Hii ilikuwa ndiyo nyumba nzuri kupita zote pale mtaani ikiwa na kila kitu maji, umeme nk.

Namkumbuka mwanae Rita mama yake Mjerumani.

Rita alikuwa mkubwa kwangu kwa umri.

Mashado Plantan alikuwa na mke wa Kijerumani.

Lakini Harry Belafonte alikuwa akipendwa na Bibi yangu Zena bint Farijala.

Bibi kila ilipotokea nafasi ya kuhadithia senema ataeleza movie ya Harry Belafonte "Island in the Sun," aliyoiona na babu yangu Salum Abdallah miaka mingi iliyopita katika ujana wao.

Kipande alichopenda kuhadithia ni Harry Belafonte kupendwa na bint wa Kizungu.

Basi nami nikawa namjua Harry Belafonte na kupenda muziki wake toka utoto wangu.

Katika nyimbo nilizozipenda ilikuwa, "Coconut Woman."

Baadae Harry Belafonte alipokutana na Miriam Makeba wakawa wanaimba pamoja nikapenda sana nyimbo yao, "Train Song."

Hii nyimbo wameimba kwa Kizulu na waliimba nyimbo nyingi kwa Kizulu na Ki-Khosa na kwa hakika utazipenda.

Mwanangu aliniletea biography ya Harry Belafonte "My Song."

Ananambia kwenye duka la vitabu muuzaji alimuuliza kama hicho kitabu atasoma yeye.

"Hiki nampelekea baba yangu yeye anampenda Harry Belafonte."

Belafonte kuna sehemu katika kitabu ilinihuzunisha kidogo kwani hakumsema vizuri Miriam Makeba juu ya hisani kubwa iliyopitika kati yao wakati wa ujana wao wakishirikiana katika muziki.

Makeba anasema hakuna jambo lililokuwa likimpa raha na starehe kama kuwafundisha Wamarekani kuimba nyimbo za Kizulu.

Miaka ikapita nikajikuta niko New York najibanza Manhattan pembeni ya Hudson River.

Wenyeji katika mazungumzo wakanifahamisha kuwa nikivuka mto tu nitafika nyumbani kwa Belafonte.

Bahati mbaya hakuna aliyekuwa anafahamiananae anipeleke kwake.
Picha ya pili kushoto Hamza Aziz akimtambulisha Ally Sykes kwa Harry Belafonte na Sidney Poitier alipowaalika chakula cha usiku nyumbani kwake.
 
Back
Top Bottom