Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

1702630441487.jpg
 
Nadhani kuna mpango mkubwa sana wa kupandisha vijana kutoka kwenye academy. Ukifuatilia utagundua kwa siku za karibuni wanachezeshwa sana vijana wageni. Nadhani mpango wa kuingia sokoni hautakuwepo.
Kwa hiyo na ninyi mmeingia mtego kama blues , kuchezesha vitoto na kutengeneza long term project au sio ?
Mtaiweza inconsistency ya kuchechemea na vipondo mfululizo kama Chelsea tunavyopitia ?
Mna roho ngumu ?
 
Leo kipenga kingechelewa kupulizwa hao Luton wangekubandua na wewe
Hali mbaya mzee mwenzangu , watoto washenzi hawana adabu hawa Luton
Na epl inazidi kuwa ngumu kila siku ,yaani sasa hivi mule epl Hamna kibonde , ukizubaa unabondwa
Tunajikongoja
Ninyi nyumbu Fc na sisi Kenge fc hamna tofauti , tukubali tu kuwa kwa sasa ni vilema , hamna namna
Tukubali kujitafuta kama asenyetoz walivyojitafuta kwa miaka mingi sasa hivi ndio wameanza kujipata
 
Substitute ya Mainoo mpaka sasa sijaielewa.Sijui Mwl alikuwa anataka nini ?.

Wazee wa uchambuzi ebu mteteeni huyu mdachi.
 
Man Utd is an amazing club. We just need to work on our short and long passes, ball control, crossing, ball domination, dribbling, defending, sprinting, tackling,goalkeeping, crosses, man marking,positioning,set pieces, through passes, attacking, and scoring goals.
Very few things, au mnaonaje wenzangu.
One thing i am certain,man u tuna wachezaji avarage mno, wanaostahili kuanza ni watatu tu walio baki uza wengine wabaki kutengeneza depth.
Amad,maino, licha staters
Garnacho, bruno, bissaka subs
The rest uza
 
.

Timu bora imeshinda mechi , simple like that hata hilo goli moja ambalo wamefunga Man United ni basi Turner kafanya msaada .

Walichofanya Notts Forest ndio timu nyingi huwa wanafanya dhidi ya Man United hata usitumie sana nguvu

1: Wasubiri waje wakufanyie pressing ( ambayo mbovu ) maana mawinga wao wanaenda kuzuia mabeki wa kati wa timu pinzani maana yake ?

2: Fullbacks wa Forest wanakuwa huru sana weka mpira pembeni then unatoka nyuma kirahisi sana ( Aina na Montiel ) walikuwa wanatoka tu ... shida ilikuwa mara kadhaa distribution ya kipa wao haikuwa nzuri .

3: Ukifika pembeni basi ingia ndani haraka maana namba 6 wao anaachwa peke yake , kwahiyo space ya kushambulia kubwa mno .

Leo Man United hujui hata walikuwa wanafanya nini ... wakiwa na mpira hujui lengo na mpango ni nini na hata bila mpira hujui pia changanya hapo na wachezaji hata kupiga pasi tatu kamilifu inakuwa shida . performance duni kabisa ambayo ilistahili kupoteza mechi .

Nuno Santo alifanya kazi chini ya Mourinho alichofanya dhidi ya Newcastle ndio kafanya dhidi ya Man United baada ya kufunga goli la pili , toa wachezaji wa ushambuliaji halafu ingiza wachezaji wa ulinzi , zuia kwa maisha yako yote kumaliza mechi . BINGO .!

NOTE

1: Niakhite kitasa kimepiga mechi nzuri sana , kila Garnacho akipata kuleta zake , kitasa kinachukia mali halafu kinapiga pasi

2: Danilo amewapika viungo wote wa Man United

3: Antony ? hata sijui kama kuna jipya lakini ukweli ni kwamba sio peke yake leo , bali 99.99 % ya wachezaji wamecheza hovyo sana

4: Forest wamefunga magoli ya kimsingi kabisa yenye ufundi wake

5: Elanga mpaka sasa EPL , magoli 4 na assists 6 halafu angalia wingers wa United

6: Nuno Santo mechi 3 kavuna alama 6

7: ETH bhana , unatoa Mainoo ambaye anaweza kukaa na mali then anaingia Scott ambaye hata hanusi hatari na angalia magoli yote mawili ya Forest

8: TRIP SHAMBA , TRIP GEREJI . Tabia yao ile ile , WAFUNGE au WAKUFUNGE .

9: Kuna timu zina damu mikononi mwao , wameruhusu vipi United kuwa nafasi ya 7 ?

FT: Forest 2-1 Man United

AMBANGILE
 
Back
Top Bottom