Manchester United (Red Devils) | Special Thread

huyu jamaa hapa ndo kamaliza kabisa
 
We are the famous fucking red devils. Leo mbinu ni ileile hakuna mabadiliko, tunakaa nyuma tunaziba space vizuri, tukipata mali inapigwa kwa Bruno, Bruno anapiga ndefu kwa Rashford... Kamba. Au tunapiga ndefu Moja Kwa Moja kumtafuta Hojlund ... Kamba
Wacha we mko vizuri
 

Ili kuweza kushindana unahitajika uwekezaji mkubwa, nafasi moja inapaswa kuwa na wachezaji wazuri zaidi ya wawili. Leo hii DM anategemewa Casemiro pekee na ndio huyo ameshakuwa babu, akiwa nje ni msala.

Timu yetu baado saana!!
Amrabat je
 
Hii timu hata akija De Zerb nae ataonekana mbovu tu, mtu ukitaka kuharibu career yako ni uende kufundisha au kuchezea United.
Nje ya Mourinho hakuna kocha mwingine yoyote alieifundisha United alihitajika na timu yoyote inayojielewa, wachezaji pia ni hivyohvyo hata sokoni hawauziki.
Nahisi msimu huu wachezaji wa United ndio wanaoongoza kwa kutembea uwanjani kuliko wachezaji wa timu nyingine yoyote kwenye Epl.
Wachezaji hata molari hawana, tena wakibahatika kufunga kagoli kamoja ndio wanaona maisha wameyapatia kwelikweli muda wote wanapiga back passes tu, wakifungwa hata ile juhudi ya kurudisha goli huioni maana wanauhakika baada ya wiki £250,000 inaingia kwenye A/c
Hii timu ili ije kubadilika kitu cha kwanza na muhimu ni kukamata familia yote ya Gilaza unatia kwenye sandarusi unaweka na mawe halafu unaenda kuwatupa kwenye kina cha bahari.
Kama boss mwenye mali hana uchungu wowote na timu zaidi ya kuangalia faida tu anayoipata usitegemee wachezaji ndio wawe na uchungu na timu hapo kila mmoja anaangalia maslahi yake tu.
Marehemu mzee Glazzer angekua yupo hai sidhani kama angevumilia kuona huu upuuzi unaoendelea kwenye timu yake, mitoto ya marehemu haina uchungu wowote na mali ya urithi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…