Habari za leo ndugu zangu. Hii tumeipenda wenyewe acha ituue tu.
BInafsi napenda tunavyo pata haya matokeo pengine Glazzer wanaweza kufikiria kuondoka. Na hapo tunaweza kuanza upya kujitengeneza bila kujali kocha atakuwa nani, japo natamani sana Eric abakie, naamini ana kitu cha ku prove.
Najua saizi mashabiki tumesha gawanyika. Kuna watakaonona tatizo ni Uongozi, wengine Kocha wengine watasema wachezaji. Ukweli ni kwamba kila mmoja anaweza kuwa sahihi kutokana na hoja zake.
Nitajaribu kuzungumziaa mitazamo tofauti.
Nianze na kocha, kitu pekee ambacho binafsi namlaum Eric ni kuiacha falsafa yake,( mpira ulio mtambulisha hasa akiwa Ajax) lakini katika hili napata pia ugumu kumlaumu tena kwa sababu kuu mbili.
1) Alijaribu kuimplement ikafeli, je angekomaa nayo wakati sisi mashabiki na uongozi una hitaji zaidi matokeo?? Tukumbuke kuwa yupo kazini na anakuwa judged kwa matokeo zaidi.
Lakini pia nikamkumbuka Van gaal ambaye katika makocha walio pita kwetu ni yeye alijitaidi kuweka identity yake kilicho mgharimu ni kwamba hakupata sapoti ya kutosha lakini pia Uongozi ulitaka matokeo/mafanikio ya haraka akaonekana hana maana. Kwa reference hii ndogo naweza kumuekewa Erick kwa nini ali opt kutafuta matokeo kwanza.
2 ) Wachezaji alio wakuta wangeweza kuendana na mfumo huo. Kumbuka kikosi alicho kikuta kwa asilimia kubwa ni mazao ya Mou na Ole, hawa ni watu wa wili wenye mifumo tofauti, kwa hiyo Ten hag angekuwa na kazi mbili, ku shape wachezaji wa mifumo tofauti wafiti kwenye mfumo wake auu wachezaji wengi waondoke ili alete watu wanao mfaa, hivi viwili vyote vimekuwa vigumu kufanyika. Kwa hiyo amejikuta hana namna nyingine.. Kwa akili yangu fupi msimu jsna baada ya kumkosa De jong ambaye alikuwa ni first target ya kocha, basi nilitegemea mbadala wake angekuja mchezaji mwemye profile inayo endana na De jong. ila akaja Casemiro( Sio mchezaji mbaya na ametusaidia sana) Hapo unategemea kocha ataweza ku endelea na Plan yake auu inabid abadil plan kulingana na aina ya wachezaji alio nao
Kwa upande wa wachezaji nawalaumu kwamba wengi hawaonyeshi juhudi za wazi katika kuipigania timu. hakuna timu ambayo ina World class watupu. Ila timu nyingi zinazo fanikiwa ni kwa sababu wachezaji wanakuwa na spirit ya hali ya juu katika kuipambania timu. Hiki ni kitu tuna kikosa kwa wachezaji wetu. Hapa ndio unakumbuka ile kauli ya Ralph kuwa timu ilihitaji mabadiliko makubwa sababu kubwa ni hii.
Upande wa uongozi. Kwa mtazamo wangu hapa ndio kwenye shina la tatizo. Uongozi haunyeshi kama una maono ya uwanjani. Anzia kwenye aina ya makocha ambao wanakuja utagundua kuwa hata uongozi haujui unataka nini na identity ya timu ni ipi.
Moyes>Van gaal>Mou>Ole>Ralp>Eric. Utaona hapo hakuna muendelezo wa falsafa. Kwa hiyo lazima kila kocha aanze upya. Na kwa hali ilivyo mimi huku Nanjilinji naona kuna umuhimu wa kuwa na DOF (mtu anaye weza kusimamia mambo ya uwanjani) lakini uongozi wangu hawajaona huo umuhimu bado, hili ni tatizo.
Kuna wanao sema Uongozi wetu umetumia hela nyingi lakini hawaoni matunda labda ndio maana wamekuwa wachungu.
Lakini fuatilia sajili ambazo tumetumia gharama kubw recently sababu ilikuwa ni either biashara auu delay zetu za kijinga mpaka kujikuta unalazimika kutoa hela nyingi. Refer ishu ya Anthony,Casemiro nk. Lakini pia wanapo pewa option ya kusajili kwa bei ndogo bado hawakubali refer Enzo,Haland nk. Lakini pia sina hakika kama Scouts wetu wana fanya kazi ipasavyo auu ndio hawasikilizwi. Kuna stor kuwa Eric anasajili watu ambao ana connection nao. Tangu Moyes tumekuwa na kasumba hii, ni kama timu haina ushawishi. Wachezaji wengi tumepata ni either wana connection na kocha auu lah basi ni kwa hela nyingi. Moyes na Fellain. Kwa Van gaal na Waholanzi+ Bastian, Mou na Ibra+ Matic. Kuna jinsi tuna struggle sana kupata wachezaji wazuri kwa bei za kawaida kama hakuna conbection, hii sijui shida ni nini
Pia turudi nyuma kidogo. Uongozi huu huu ambao uliruhusu mtu kama Herrera aondoke bure sababu alitaka kuongezewa mshahara( inawezekana alihitaji mkubwa kuliko impact yake) lakini wakaidhinisha mkataba mpya wa Phil Jones alikuwa wodini tu. Ni nani anaelewa kwa nini msimu ulio pita tulimkosa Gapko??
Na kuna mlolongo wa maamuzi ya ajabu ambayo yamekuwa yakifanyika kwenye timu yetu unabaki kujiuliza hivi hawa Glazzer na wasaidizi wao ni wazungu auu.
Nitakuwa wa mwisho kuamini makocha wote walio pita kwetu ni wabovu,