Mbona mkali unakuwaga na Michango mizuri sana ya Soka ila kwa ETH unakuwa kama unaendeshwa na Hisia zaidi! Kuna wakati huwa unasema De Zerbi asipewe timu kubwa sababu atatisha sana na Maneno mengine ya aina Hiyo. Ni Mwalimu Mzuri ila Unadhani kwa nini Timu kubwa Nyingi Italy wakati anaondoka Sassuolo hazikuwa na muda naye na nyingi kati yao hazikuwa na walimu wa uhakika?
Kila Mwalimu ni Bora kwa Style yake akipata Players anahitaji kuweka falsafa yake {Hakuna Mfumo Universal kwamba ndio Bora} Hata Sean Dyche angepewa World Class Players kwa Style yake kucheza na Ilokuwaga Burnley yake ingekuwa kazi jaribu kuwaza yeye anaamini katika Def Set-Up na Long Balls, awe na kina Pepe, LLoriente, Aduriz, Zlatan, Matic, Drogba, etc kwenye kila nafasi hamna ambae angetamani Game na timu yake.
Unazungumzia sana TALENT ID, Juzi umekwepa Swali langu na leo kauli yako inaonyesha uliliona ukakwepa, Wewe ni Arsenal Fan, ARTETA ameshasajili wachezaji 29 na kombe analo 1, ETH alisajili 4 akaweka Kombe 1 mezani CR7 kocha kamkataa, Auba, Ozil, Lacazette kesi hiyo hiyo. Unasema hana namna ya kuwaamini Academy Players, tuna Garnacho na kama sio Injury ungekuwa unamwona Mainoo akipata dakika.
Swali langu Narudia, NITAJIE ACADEMY PLAYER/S YEYOTE ALIYEAMINIWA ARTETA MNAE KWENYE KIKOSI NA KAPATA DEBUT TOKA KWA ARTETA? Nakukumbusha Arteta ana msimu wa 5 Arsenal.