Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Mpaka sasa tumesajili mchezaji mmoja na wachezaji wa hakiba wawili.

Natamani niwe sipo sahihi ila sidhani.
 
Man Utd’s last 30 games at Old Trafford:

WDWWWWWWWWWWWWWDWWWWDWWWDWWWWW

New season, same United, but things could have been very different today... 👀

They faced 23 shots vs a hugely impressive Wolves side, having only faced more on one occasion in 2022/23, (25 – away to Arsenal). 😳

And they may consider themselves quite lucky after VAR decided NOT to award Wolves a penalty in the 95th minute, after new man André Onana clattered into Craig Dawson in the 95th minute.

One things for sure, the Red Devils will need to step up their game if they're to challenge for the top 4 this year... 😅
 
Nasubiri mumuombe AWB msamaha..
Yeye lini atatuomba msamaha mashabiki kwa kupigwa 7-0 na Loserpool, kuruhusu man city kubeba treble wakati alikua na uwezo wa kulizuia hili kwenye fainali ya FA,

Atuombe kwanza yeye msamaha kwa udhalilishaji tuliofanyiwa na Sevilla kwenye europa au mashabiki hawana haki ya ku demand apologies toka kwa wachezaji wasio tekeleza majukumu yao ipasavyo?
 
If I speak.....
Alishanipa wasiwasi tokea mechi za kirafiki, ndio maana naimba wimbo wa AMRABAT
Weka 6 yoyote duniani kwa mfumo wa Jana angechemka, i hope hii ni wake up call kwa ETH no 8.5 wawili inaweza kutucost tukikutana na Timu inayojielewa 7 zinaweza rudi tena. Hawa Wolves ndio wanatabiriwa kushuka daraja ila Cunha alikua anapita tu katikati, kweupe kabisa.
 
Hii nilivyoiona tu kwenye mechi nilitegemea kukutana nayo mtandaoni. 😂

Jana wachezaji wetu wamenyanyaswa sana. Hii mechi ilikuwa kama Boys vs Men na Men ni hao Wolves. Bruno jana kapigwa push za kutosha, Garnacho, Pellistri wameonyeshwa bado ni watoto wadogo sana kwenye hizi kazi za kiume.

Premier League inahitaji wachezaji wenye nguvu na akili ya mpira sasa ukiwa na mchezaji ambaye hana vyote ndiyo yale yaliyotokea jana. Ni kazi ya bench la ufundi kusimamia mazoezi ya gym kwa hawa vijana, push kidogo tu mtu yupo chini.
 
Jana nimeingalia man utd yangu mpaka naona huruma, wachezaji very weak, hamna kujituma, no chemistry cjui uwanja wa mazoezi wanafundishwa nini aisee, fitnes zero, Wolves ilikua timu bora ktk nyanja zote uwanjani,

Yaani endapo tungeanza na man city ile jana zilikua 8 ashukuriwe mwenyenzi Mungu tu

Casamiro ndio nin unatufanyia!

Timu inapoteza mipira ovyo, kutengeneza shambulizi la kieleweka ni shida, yaani tunacheza kama ndondo cup la kina shafidauda

Yule Mount ETH kaona nini kwake???? Maana nikae kimya tu, mim sio muumini wa watoto wa kingereza kabsa, wanakuzwa na media zao tu

Msimu wa stress kama kawaida yetu

Msimu huu Simba Sc ndio imebeba furaha yangu, mwenyenzi Mungu ibariki Simba lunyasi
 
Casemiro kachoka sana nadhani muda wa kula pensheni umefika.

Rashford punda sana anacheza kifaza sana ,washambuliaji wetu hovyo sijui tutafikaje September bila namba 9 katili,hapa wakachukue cheap options kama Mehdi Taremi tu.

Kupigwa msako kawaida ila huwa tunafanyiwa hivi tukiwa tunaongoza kwa tofauti ya goli 1 inatakiwa washambuliaji wabadilike tukiwa tunaongoza hata 3 hatuwezi kukutana na hizi shuruba za stoppage time kwa sababu tunakuwa hatuna presha.

Sajili 3 hazitoshi hapa naona usajili ni wa kipa tu hizo nyingine pata potea
Timu letu linacheza hovyo kuanzia kwenye midfield huko.mbele ndiyo hivyo zaidi
 
Back
Top Bottom