Moja ya hasara ya kulipa mishahara mikubwa ni hii [emoji3516]
[emoji3502]Mchezaji akilipwa mshahara mkubwa alafu ana uwezo wa kawaida inakuwa ngumu sana kumuuza kwa sababu zifuatazo:
1) Timu zingine zinazotaka kumnunua wanashindwa kufikia makubaliano ya mshahara wake; wachezaji wengi hawakubali kwenda timu kwa mshahara mdogo kuliko anaolipwa.
2) Mchezaji mwingine yuko radhi akae benchi maadamu kibunda kinaingia. Hajali.
3) Ili kumuuza inabidi klabu iwe ruthless—yaani kama mkataba wake amebakiza miaka miwili wamlipe ela yote ya miaka hiyo iliyobaki, wamfukuze/wavunje mkataba. Hiki kitu kwa Glazers ngumu sana kufanya.
[emoji3502]Tunaposema kulipa mishahara mikubwa sana kuna madhara hasa kama mchezaji kiwango chake hakistahili malipo hayo, hasara zake ndio kama hizo.
[emoji3502]Machester United ndio timu inayolipa mishahara mikubwa zaidi EPL. Lakini huenda ndio timu yenye wachezaji wavivu zaidi EPL.
Matatizo yote tumejisababishia sisi, tusingeshindwa kuuza wachezaji ili tupate hela ya kusajili wengine.
Watu kama Maguire na Martial ni mizigo ila kuuzwa hawataki,acha tuendelee kuwaangalia Gunners soon wanamfikia City