Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Graza kinachowaponza wametoa Uhuru mkubwa watu washike nyadhifa ambazo Ni muhimu Sana ,

Nikweli wanabeba pesa mingi Sana, lakini bado kile kidogo wanachokitumia kwa usajili Ni kikubwa ,hamjawahi kuwa na tatizo la kusajli wachezaji wa €80-100m

Kama Ni hivo tatizo lipo kwa uongozi, Graza hawajui mpira inajulikana , walipotoa mianya waletwe watu wa mpira bado hawakuletwa watu wampira

Leo timu akichukua muarabu bado mtasajili wachezaji wa Bei zile zile ambazo alikuwepo Graza ,

Siku mtakapoleta watu Kama kina Van der sar , Luis ocampos ,na watu wanaofanana mitazamo Kama hai, Katika uongozi wenu , hamtaona ubaya wa Grazzer.

Hivi unajua pale city wachezaji wao ukimtoa jack Ni wa Bei €30-60m tu ,
Glazers msimu huu ndiyo wanatupoteza kabisa maana kama kuuza timu kwa muda uliobaki ni mchache sana.

Sasa hivi ilitakiwa EtH awe ashajua budget yake na kuanza kumalizana na wachezaji mapema.

Liverpool tayari wameshamalizana na Mac Allister, msimu ujao ushindani utakuwa ni mkubwa sana.
 
Kikosi hiki unaweza kuchukua ubingwa wa epl na kuleta ushindani UEFA? sidhani kama itawezekana kwa Man u, unless wanataka kuwa wasindikizaji.
Tatizo ni pesa. Hiki kikosi siyo chini €350m. Kama mashabiki kuna muda inabidi tuwe realistic, United kubeba ubingwa wa EPL msimu ujao ni ngumu sana.

Kile kikosi cha mwanzo kinafaa sana maana kipo balanced ila kama pesa ipo hiki ni cha ubingwa kabisa.
formation_05_06_2023_ 14_53_34.png
 
Tatizo ni pesa. Hiki kikosi siyo chini €350m. Kama mashabiki kuna muda inabidi tuwe realistic, United kubeba ubingwa wa EPL msimu ujao ni ngumu sana.

Kile kikosi cha mwanzo kinafaa sana maana kipo balanced ila kama pesa ipo hiki ni cha ubingwa kabisa.View attachment 2646868
Manjesta shida Ni management ,Chelsea Wanataka wawauzie mount kwa €80m halafu wao hiyo hiyo hela wakamchukue Caicedo kwa £75-80m (€80-85m)

Wakati huo huo manjesta unaona kabisa wanamuhitaji mtu Kama Caicedo ,

Umri mdogo, anacheza #8 ,#6 anacheza inverted RB , Ni press resistant

Kitu kingine Caicedo anatoa priority kwa timu inayocheza UCL ,

Kituko Sasa Manjesta wanakomaa na mount ambaye kwa misimu miwili amekuwa na kiwango duni
 
Liverpool Wana bajeti finyu Sana lakini kwa usmat wao wamempata MacAllister kwa less than £60m .

Timu itakayompata Caicedo itasumbua Sana
 
Manjesta shida Ni management ,Chelsea Wanataka wawauzie mount kwa €80m halafu wao hiyo hiyo hela wakamchukue Caicedo kwa £75-80m (€80-85m)

Wakati huo huo manjesta unaona kabisa wanamuhitaji mtu Kama Caicedo ,

Umri mdogo, anacheza #8 ,#6 anacheza inverted RB , Ni press resistant

Kitu kingine Caicedo anatoa priority kwa timu inayocheza UCL ,

Kituko Sasa Manjesta wanakomaa na mount ambaye kwa misimu miwili amekuwa na kiwango duni
Hatuwezi kulipa €80m kwa Mount, haitatokea. Maximum €55m.

Kwenye eneo la #8 Mount ni hatari zaidi. Caicedo akija atatumika kama IFB. Pia Case akiwa hayupo anaweza ku-cover #6. Jamaa ni kiraka.

Tatizo letu ni pesa tu.
 
hatujawahi kuwa na shida ya matumizi ya fedha, yapo mengi ya ujinga anayoandika huyo hamis77 na pia yamo mengi ya msingi anayoandika huyo bwana.

anachokosea yeye ni njia sahihi ya kuwasilisha.
timu inayotumia paundi millioni 150 hadi 200 kila mwaka huwezi kusema ina ukata wa fedha.
 
tatizo kuu linalotukabili hatujui muda sahihi wa kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa klabu.
mfano:

chini ya ralf rangnick tulishuhudia kupewa muda mwingi wa kucheza anthony elanga, kwa klabu ilio makini ingelihakikisha inamuweka sokoni dirisha lililopita na tungelipata fedha nzuri.

mimi ninayeishi huku unguja upembani nilishamuona anthony elanga hana future njema hapo klabuni, ina maana uongozi wa manchester united wao hawakuliona hilo?

leo hii tunamweka elanga kwa thamani ya paundi millioni 10

liverpool wamemuuza neco williams kwa paundi millioni 17 kwenda nottingham forest.
liverpool wamemuuza harry wilson kwa paundi millioni 14 kwenda Fulham.
liverpool wamemuuza solanke kwa paundi millioni 19 kwenda bournermouth
hawakusita kuwaweka sokoni kwa sababu walishaona hawana mpango nao wa muda mrefu licha uchanga wa umri wao.

walichokifanya wao ni kuwabrand wachezaji wao.
full stop

manchester city walimuuza bazunu kwenda southampton, yaani city wamepata paundi millioni 13 kwa golikipa anayecheza Kikosi B.

MAN CITY hao hao wamemuuza lavia kwenda southampton kwa paundi millioni 15 huku wakiweka kipengele cha kumnunua tena kwa paundi millioni 40, huyu lavia naye alicheza team B.

sisi mpaka leo tunaumiza kichwa juu ya dean henderson, yaani kimasihara masihara tunazikalia paundi millioni 25 hadi 35 kwenye makalio ya carrington.

Team ilio serious haiwezi kumfikiria scott mctominay kwa zaidi ya mara mbili, newcastle united walishaonyesha nia ya kumhitaji lakini klabu inasita kupokea paundi millioni 25 hadi 35 kwa mpuuzi kama yule.

unajiuliza hii klabu ya manchester united inakhofia kitu gani kwa kumpoteza mctominay?

uza mctominay baadae mnunue mathew nunez wa wolves,
umepoteza nini?

tuna safari ndefu sana
 
nasubiria muujiza wa ten hag.
nataka kuona jinsi atakavyoitawala hiyo dunia kwa kutumia namba 8 wawili kama tunavyoambiwa.

bruno + mount .
na wakati huo huo DM wako ni casemiro na si RODRI.
tutaendelea kucheza mpira wa kufukuzana na wapinzani mpaka kiama.
ninachokiona mimi ujio wa mount si mwisho wa kusajiliwa kiungo mwengine wa kati

we need controller hususani phase 1 ndipo tumfikirie huyo mount.
chelsea wamefanya sajili nyingi za kipumbavu lakini Mungu kawajaalia huduma ya ENZO.

mwili wa enzo ulipaswa kuwepo manchester united, ila sishangai tulikataa kulipa euro millioni 20 kwa ajili yake.
tukakataa kulipa euro millioni 6 kwa caicedo.
 
  1. 2023 - tunataka beki wa kati wa kulia (mkorea, timber)
  2. 2022 - tumesajili beki wa kati wa kushoto (martinez)
  3. 2021 - tumesajili beki wa kati wa kulia (varane)
  4. 2019 - tumesajili beki wa kati wa kulia (maguire)
  5. 2018 - tumesajili beki wa kati wa kulia (lindelof)
  6. 2016 - tumesajili beki wa kati wa kulia (bailly)
inawezekana miaka nimekosea ila content sijakosea.

This is Manchester united
 
hatujawahi kuwa na shida ya matumizi ya fedha, yapo mengi ya ujinga anayoandika huyo hamis77 na pia yamo mengi ya msingi anayoandika huyo bwana.

anachokosea yeye ni njia sahihi ya kuwasilisha.
timu inayotumia paundi millioni 150 hadi 200 kila mwaka huwezi kusema ina ukata wa fedha.
Tatizo la United siyo pesa ni matumizi sahihi ya pesa zake.

Kufanya maamuzi sahihi juu ya kikosi chake.

Kama united wangekuwa serious nusu ya kikosi alichotumia Ten Hag msimu huu kisingekuwepo.

Wachezaji wengi wa Man United kwenye vilabu vingine vikubwa wangekuwa chaguo la tatu.

Kwenye kikosi chetu hakuna mchezaji hata mmoja angeweza kuwa chaguo la kwanza kwenye kikosi cha Man City na Liverpool labda Casemiro na Bruno tu wengine wote hata benchi wasingekaa.
 
tatizo kuu linalotukabili hatujui muda sahihi wa kufanya maamuzi yenye maslahi mapana kwa klabu.
mfano:

chini ya ralf rangnick tulishuhudia kupewa muda mwingi wa kucheza anthony elanga, kwa klabu ilio makini ingelihakikisha inamuweka sokoni dirisha lililopita na tungelipata fedha nzuri.

mimi ninayeishi huku unguja upembani nilishamuona anthony elanga hana future njema hapo klabuni, ina maana uongozi wa manchester united wao hawakuliona hilo?

leo hii tunamweka elanga kwa thamani ya paundi millioni 10

liverpool wamemuuza neco williams kwa paundi millioni 17 kwenda nottingham forest.
liverpool wamemuuza harry wilson kwa paundi millioni 14 kwenda Fulham.
liverpool wamemuuza solanke kwa paundi millioni 19 kwenda bournermouth
hawakusita kuwaweka sokoni kwa sababu walishaona hawana mpango nao wa muda mrefu licha uchanga wa umri wao.

walichokifanya wao ni kuwabrand wachezaji wao.
full stop

manchester city walimuuza bazunu kwenda southampton, yaani city wamepata paundi millioni 13 kwa golikipa anayecheza Kikosi B.

MAN CITY hao hao wamemuuza lavia kwenda southampton kwa paundi millioni 15 huku wakiweka kipengele cha kumnunua tena kwa paundi millioni 40, huyu lavia naye alicheza team B.

sisi mpaka leo tunaumiza kichwa juu ya dean henderson, yaani kimasihara masihara tunazikalia paundi millioni 25 hadi 35 kwenye makalio ya carrington.

Team ilio serious haiwezi kumfikiria scott mctominay kwa zaidi ya mara mbili, newcastle united walishaonyesha nia ya kumhitaji lakini klabu inasita kupokea paundi millioni 25 hadi 35 kwa mpuuzi kama yule.

unajiuliza hii klabu ya manchester united inakhofia kitu gani kwa kumpoteza mctominay?

uza mctominay baadae mnunue mathew nunez wa wolves,
umepoteza nini?

tuna safari ndefu sana
Pamoja na ubovu wa management Man United ndiyo timu ambayo inawachezaji legelege kuliko timu zote za EPL, ukiondoa defenders na Casemiro wachezaji wengine wote hawakuwa na uwezo wa kushinda duel yoyote.labda Chief Mkwawa ana takwimu sahihi.
 
Ndugu zngu allypipi Flano poleen kwa kichapo tulichowapa najua mnatuombea njaa game ya Jmos lkn hakuna namna Record yenu ya treble mliyokua mnalingia ss inaenda kua mwsh.

The Noise Neighbors are going places now .. #TheCityzens
 
Kane gani kwanza huyo mnaye msemea humu.maana kane wa Tottenham ana enda zake madrid.nyumbu labda mpewe kane wa WWE.mk8 jitahidi sana mta pata mitrovic wa Fulham ndo size zenu
 
Costa De Gea

#𝙏𝙧𝙪𝙨𝙩𝙏𝙝𝙚𝙋𝙧𝙤𝙘𝙚𝙨𝙨𝙀𝙏𝙃
#𝙐𝙣𝙞𝙩𝙚𝙙𝙛𝙤𝙧𝙩𝙝𝙚𝙁𝙖𝙣𝙨
#𝙂𝙡𝙖𝙯𝙚𝙧𝙊𝙐𝙏
#𝙂𝙂𝙈𝙐

man utd |
IMG_20230605_191814_191.jpg
 
Back
Top Bottom