Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Wachezaji pesa nyingi ila hawaoneshi thamani ya pesa
 
Nakubaliana, na inafanya tukose magoli mengi na kufanya Goal difference ya 9+
 
Kweli 10Hag ana kibarua kigumu sana pale united. Leo hii akitokea mwendawazimu mmoja akasema tumuuze Rashford ili nafasi yake achukue Mitoma watu watamshangaa kama walivyokuwa wanakasirika pindi Son akikuzwa dhidi ya Rashford. Kwa sasa tunadanganywa na rekodi ya magoli yake ila jamaa anaiharibu striking force yetu sana tu kwa ajili ya kufukuzia rekodi binafsi. Takwimu ni kitu kingine ila muunganiko wa timu ni suala la msingi zaidi.

United inaharibiwa na media za uingereza pia ila hii damage ingepungua kama tungepunguza hawa kenge wa malkia kwa kiasi cha kutosha. Kwa miaka ya sasa Wingereza wanafaa kucheza nafasi za mabeki wa pembeni kuliko nafasi nyingine zozote ndani ya uwanja.

Kosa la 10Hag liko wapi kama anafundisha timu kutengeneza nafasi za kufunga na timu inafika langoni mwa adui mara kadhaa ila wanashindwa kuweka mpira kambani? Pale mbele ni mashindano ya one man show kati ya Rashford,Martial,Anthony,Garnacho,e.t.c
 
Oyaa nyie nyumbu achieni hiyo top 4 waingie liverkuku. Hamstahili kucheza champions league na sie.
 
Halafu Hamis Yuko wapi wazee. Kule kwetu simuoni nikasema nije nimcheki huku ambapo ndiyo kijiweni kwake baada ya maskani ila huku Nako simuoni...
 
Ni ukweli mchungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…