Kibarua cha Kuirejesha Manchester United juu kimekuwa kigumu sana..
naweka akiba ya maneno ila..Only Pep Can Do That..
Our Ten Hag tutamuonea tu..
huwezi beba ubingwa wa EPL na wachezaji dizaini ya Sancho, Rashford, Antony, and co..
Manchester United inahitaji 5 Worldie kubeba EPL..as of now ni Only Casimiro..ndie World Class Player..
yule bwana hamis77 huwa tunamuona snitch ila kiuhalisia yupo sahihi..
Imagine Manchester United wame spend karibu £250M.. ila mpira bado hauna uelekeo..
Mchukue Rashford mpeleke Real Madrid, Bayern Munich, Manchester City, PSG, tuone atamweka nani benchi?
Safari bado ni ndefu..tuwe na subira..ingawa bila watu sahihi wa usajili safari ni ndefu zaidi..
Pep msimu wake wa kwanza alifanya nini City?
Wala huhitaji World class players kubeba EPL, unahitaji wachezaji sahihi tu. Wengi mnashindwa kuelewa United ina matatizo kwenye kila eneo: kuanzia GK, CB, RB, CM, ST.
Hata wakisajili hayo maeneo yote bado nafasi ya kubeba EPL msimu ujao ni ndogo sana, zaidi tutakuwa title contenders. Maana ndiyo kwanza kila usajili tunafanya kwa ajili ya first eleven na siyo squad depth.
Tumetumia £250m kuboresha maeneo kadhaa. Timu ni kiungo na hilo ni eneo United hatuna watu sahihi, hatuna striker, hatuna top quality CBs: ameumia Martinez na Varane tuna-drop points. Hatuna RB wa kuweza ku-link up na RW: ikumbukwe Sancho pale Dortmund alikuwa anacheza na Hakimi.
Ten Hag ni kocha anayeonyesha mwanga, kwanza kaleta ball-passing CB "Martinez" baada ya kipindi kirefu United tumepata DM "Casemiro" kamleta Antony na sasa anamtaka Frimpong ambaye sasa anacheza RW ila yeye anataka amtumie kama RB ku-influence RWs zake.
Huwezi kucheza total football ukimtegemea De Gea "stopper" ambaye anashindwa kuanzisha mashambulizi na hawezi kumiliki eneo lake vizuri. De Gea ndiyo chanzo cha United kupoteza mipira kila muda anapopata anabutua, kipa wa Brighton (2nd GK) jana katoa somo.
Rashford, Sancho, Antony ni wachezaji wazuri sana tu, tukiboresha eneo la kiuongo kwa kumpata ball carrier "De Jong", ST, CB, RB, GK tutabadilika kiuchezaji.
Suala la ku-spend na kufanya vizuri havina uhusiano. Chelsea £600m imetumika na bado timu haina muunganiko.