Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Walikuwa na accuracy ya 87.5% kwenye mashuti yao langoni mwetu.

Lakini unaisemea vipi hali ya uchovu wa mechi nyingi mfululizo pamoja na mabadiliko ya kikosi cha kwanza mechi hadi mechi kwenye kile kipigo?
Hata mngepumzika mwaka mzima
Bado tungewapiga nje ndani.

Karibu seven up Mkuu.
 
Sio kwa chuki kwa gunners pamoja na mpira mzuri wanaocheza leo hii binafsi sijashawishika kama ni suala endelevu kuwakuta wakiwa juu misimu 2 mfululizo kama ilivyo kwa city na liverpool. Kwa msimu huu ubora wa city umeshuka na liverpool ndio kama unavyoona tena.
Wameimarika lakini hawajafikia kiwango cha hao wawili,falsafa yao ni umiliki na recruitment yao wanaangalia technical ability ya mchezaji ndio maana wanafanikiwa kupishana na city uwanjani. Ukija upande wetu sasa,baada ya MARTINEZ,ERIKSEN na kidogo Bruno wengine wote wanaogopa mipira kama kiazi cha moto mdomoni.
 
Ungejua ndio kwanza vijana wako na average ndogo ya umri usingeandika huu utopolo
 
Sio kwa chuki kwa gunners pamoja na mpira mzuri wanaocheza leo hii binafsi sijashawishika kama ni suala endelevu kuwakuta wakiwa juu misimu 2 mfululizo kama ilivyo kwa city na liverpool.
Hiyo ndio challenge anayopaswa kupambana nayo mikel arteta, lakini hili linawezekana kama atasimamia kwa nidhamu ya hali ya juu maendeleo ya viwango vya wachezaji wake, suala la recruitments pamoja na sekta ya afya kwa lengo la kupambana na majeruhi

Unawakuta wachezaji mfano wa de bruyne, bernardo silva, walker, mahrez wanaperform kwa kiwango cha juu cha soka kwa zaidi ya miaka 4 na bado wanaendelea kushawishi kuwepo kikosi cha kwanza.

Lakini kuna jamii ya rashford, martial, fred, maguire, lindelof na wengineo wamekosa nidhamu ya consistency.
 
Lakini unaisemea vipi hali ya uchovu wa mechi nyingi mfululizo pamoja na mabadiliko ya kikosi cha kwanza mechi hadi mechi kwenye kile kipigo?
Nakumbuka niliwahi kushare humu ndani..
Kuna comment niliwahi kuiona mtandao wa reddit.

Mshabiki wa ajax alisema ten hag si muumini mkubwa wa kufanya rotation.
Sure tunacheza michuano minne kuliko timu nyengine hivyo lazima kutakuwepo na ladha ya uchovu wa kiakili na kimwili kwa wachezaji.

Ishu inakuja kuna baadhi ya wachezaji ukiwaondoa kikosi cha kwanza ndio umevuruga chemistry nzima.

Unamtukana bruno lakini ukiangalia nje mbadala wake ni kobbie mainoo

Tuwe wavumilivu huenda tutafika
 
City hajashuka Kama wengi wanavyoamini

Kaangalie miaka yote ,Kipind Kama hiki City huwa anakuwa na points ngapi ,utakuta ni hizi hizi alizonazo Sasa

Arsenal average age ni 24 , I think ndio timu yenye umri mdogo EPL wakipishana kidogo na Soton
 
Unachosema ndio hiki nichosema ila mnasema tuna chuki

Bado man u hamuwezi kwenda toe to toe na timu nyingi EPL ,matumaini yaliyopo kwa wengi Ten hag atafanya hivo mbeleni , kitu ambacho binafsi nawakatalia kwa ushahidi wa kimazingira ,Kwanza anaogopa hata kumuondoa Degea zaidi anapambana kumuongezea mkataba ,pili kwa bajeti ya man u alitakiwa awe ameshaleta mabeki wa Kati tayari walio vzr mguuni, tunona alimleta Martinez , coz ya mahusihano na ajax, Sajili zake nje ya ajax na Erevedise Hana ujanja ,so atarudi kwenye sajili za big names ambazo zilishaifelisha man u huko nyuma.

Bado anahitajika kupata perfect replacement ambazo ni long term za casemiro na eriksen.
 
Kama Arsenal tungekua tunacheza 3 4 3 huyu Tavares angekua hatari vile vile. Hakimi hakushine Madrid kwa ajili ya formation, ila Malacia hapati namba siyo kwa vile formation haimsupport ila ni kwavile Shaw anaoffer kinachotakiwa kuliko yeye.

Tomiyasu akiwa left back (ni right footed huyu) akamzuia Salah tukashinda 3. Huyo Shaw akiwa huko anapotakiwa kua wamepigwa 7. Defensively Tomiyasu ni mzuri kuliko Shaw na Dalot.
 


Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Bado tupo vizuri sana ndugu zangu tutembee tu kifua mbele maana tupo kwenye ligi kwenye nafasi nzuri tupo FA tupo ueropa yanini ujipe pressure hapo ulipo kunywa bia wewe.

Tatizo mnakuwa serious mno just relax hata tukikosa makombe yote msimu huu sio mbaya tuna dalili nzuri tulikaa miaka 5 bila kombe lolote japo carabao ni kombe la chai ila tu relax tu.

Timu yetu tuanze kui judge msimu unaofata kwa msimu huu tufunge mabakuli tu.

Just relax ushabiki sio kushinda game tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…