Ingawa 7 ni nyingi lakini bado zinatoa point tatu kama anayeshinda 1-0 tu. Arsenal,man city,liverpool,n.k zimeshinda kwao nasi tumeshinda kwetu.
Mtizamo wa kwanza kabisa kwa EtH ilikuwa kufahamu anaenda kucheza away kwa Liverpool ili achukue tahadhali ya kutosha kwa maana ya kupata walau droo tu. Matokeo ya arsenal kwao na City kwao yalitosha kumwambia timu huwa na sura tofauti kwenye uwanja wa nyumbani maana hii ni EPL na sio Eredisie ambapo Ajax anashinda popote anapotaka kwa idadi ya magoli anayotaka.
Rotation ya wachezaji imekua ni shida kubwa sana hasa nafasi za ushambuliaji na kiungo. Mfano mzuri ni Bruno,amekuwa hapumzishwi mechi hadi mechi matokeo yake jana alikuwa anapiga pasi kama amejikwaa vile. Hii wengi wetu tutasema sababu ya kikosi kidogo lakini kuna mechi walau dakika 10-15 za mwisho weka wale madogo wa akademi wakajaribu kutushangaza pia.
Pamoja na kwamba ratiba imechangia sisi kufungwa kwenye hii mechi kwa 50%,ila fomu yetu nzuri ya ushindi imepelekea sisi kupoteza hii game kirahisi na kwa kudhalilika hivi. Tangu mwanzo wa mechi Peter Drury anasema De gea anaonyesha kuanza kupoteza muda ndani ya dakika 10 za mwanzo. Kwamba Man utd walijua watulize presha ya liverpool mwanzoni halafu muda wao wa kushinda mechi utafika wakati wowote. Hii kujiaminia muendelezo mzuri ukafanya tufungwe maana tuliamini bahati bado iko upande wetu siku zote.
Conversion rate ya Rashford inatia huzuni sana. Ana rekodi nzuri siku za hivi karibuni ila bado inategemeana ameamkaje siku ya mechi ili kukupa kiwango stahiki. Tunamhitaji striker wa maana kama msimu ujao tunataka kupambania ndoo kubwa kubwa na wenzetu na wala sio kumtegemea Rashford kwa kazi ya kuzalisha magoli.
Lesson learned and we move forward.
GGMU.