Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,220
- 44,194
Mkuu chukulia mfano wa kilayman kabisa.Boss, logic yangu ilijengwa katika hili ulilolisema "Lazima kuna deal la chini ya kapeti wameingia ili Bank ifaidike..."
Nakataa kuwa kuna dili chini ya kapeti. Hizo hela hazikuchotwa kinyume na taratibu, bali ni jinsi deal lilivyoingiwa toka mwanzo.
Wewe unataka kuinunua Mtibwa, thamani ya Mtibwa ni Bilioni 10, huna Bilioni 10 ukaenda kwa Bakhresa akukopeshe, Bakhresa akakupa Bilioni 10 ila kwa Riba ya Bilioni 1 kila mwaka, na wewe ukaamua usilipe deni la Bakhresa ukalihamisha kwenye Club, ila kila mwaka unampa Bakhresa Bilioni 1,
Baada ya miaka 15 umemlipa Bakhresa riba ya Bilioni 15, na deni lipo pale pale anakudai, na wewe mwenyewe faida uliopata hafiki hata Bilioni 10, je mtu akitumia figure of speech na kusema Mtibwa inamilikiwa na Bakhresa si sawa?
Hii figure ya Swissramble ni ya 2019 ila utapata general idea
Ukiangalia Box la kwanza kuna Interest na Debt repayments around £900m na Dividends ni £166m,
So kinachoenda bank ni kikubwa sana, compare na Faida wanayopata Glazzer, even ukijumuisha mauzo ya hisa £465M still kinachoenda Bank ni kikubwa.
Hizo ni data za 2019, mwaka huu hio figure imeshazidi £1B. Plus deni lao inakaribia £2B ambayo wanachota toka kwetu.
Ukumbuke Utd haikuwa na deni kwa miaka takriban 100, inajiendesha yenyewe bila tabu.