Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Namuona Rashford akiongezewa mkataba, kama akiondoka Heaton, Jones, Shaw, Bissaka, Tuanzebe na kuna uwezekano tukamuuza Williams tutabakiwa na homegrown players watano na katika sheria za FA lazima tuwe nao angalau 8.

Rashford kigezo cha Uingereza kinaweza kumbeba kupata mkataba mpya, ukizingatia sioni EtH akivutiwa na wachezaji wa Kiingereza. Kuliko kununua mchezaji mpya wa England au ku-promote academy graduates kukidhi vigezo ni heri kumbakisha kama squad player.

Hapo mwengine labda De Gea tu ndiyo nina uhakika anaweza kupewa mkataba mpya. Wengine itategemea zaidi na maamuzi ya kocha.
 
So far kuna improvement kwenye defence ya United,partneship ya Martinez & Varane wamekuwa wanaelewana sana na wanajipanga vizuri na defence yote (back four) wamekuwa unit ,mmoja akifanya kosa wenzake wanawahi ku-clear .Only weakness kwenye defence ni Dalot na amekuwa ana-improve na wenzake wanamsaidia .Casemiro akishasettlle huenda katikati patatulia Erikson akisogea mbele tuweze ku-dictate midfield na ku-create more chance
 
Defence kuna umoja..hata mmoja akilala wengine wanacover fasta..Ndo spirit tunayotaka.


Jana Dalot alinifurahisha sana baada ya ile goalkick alivyoenda kupeana tano kibabe na Martinez plus Varane.
 
Kwa jana sikuangalia game ya united kwa utulivu wa kutosha lakini kwa kiasi fulani Mctominay amecheza vyema ukilinganisha na zama za Ole. Na sio hapo tu,tangu game ya Liverpool na Soton dogo ameongeza kujiamini kwenye umiliki wa mpira,anaachia mara moja na anacheza rafu zenye akili kidogo.

Naomba siku ambayo Case atatulia kwenye timu,tuone combo yake na Fred the Red (yaani kuihamishia anchor ya Brazil United). Kwangu mimi hii itawezekana endapo mwenendo wa Bruno utaendelea kuwa wa kubahatisha kama wadau wengi wanavyopiga kelele dhidi yake kwa sasa,hivyo itakuwa mid 3 ya fred,case na eriksen.

Mbali na Maguire,wadau tumemsahau mapema sana the ice man Lindelof. Nilipenda kuona pacha yake na martinez in case varane pancha zikianza kumrudia ili kuwa na uhakika kuwa maguire hatarudi uwanjani hivi karibuni.
Katika defense,martinez ndio kabadilisha kila kitu hivyo nategemea kuona ubora wa lindelof anaouonyesha akiwa na timu yake ya taifa,sweden pindi watakapocheza pamoja.

Kwa game ya jana,sikujua kwanini Eriksen kawa man of the match. Mwenye uelewa anisaidie tafadhali.
 
Man chester kwa sasa mpo vizuri. Naamini mtaendeleza ushindi kadri kocha atavyoendelea kuzoea Ligi. Kama mnakumbuka Gadiola alivyokuja Epl alipigwa kipigo heavy na Lescister City mpaka suruali ilitaka kudondoka akachapwa tena Everton kipigo kweli kweli.

So hata ten hang amekaribishwa ipasavyo Epl. Lakini sasa ameanza kuimili Ligi[emoji122][emoji122]
 
Hukuangalia mechi halafu unashangaa ericksen kuwa man of the match unashangaa Sana

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Kaka endelea kutuombea Mungu atuinue tena.....siku nabeba epl aseee lzm nitoe sadaka ya shukurani kwa baba muumba
 
Manjestaa kesho mukishindwa kula uroda wa ma gaygooners fc aka arse8 aise nitawashusha vyeo. Nategemea kesho muwakate utepe wale watoto.
#CFC💙💙💙
 

Umewaza kama mimi mkuu. Hii mechi inatakiwa Fred na Casemiro waanze pamoja, mbele yao acheze Eriksen au Bruno.
Tuwe na ulinzi shirikishi. Arsenal wapo fast wakati wa kushambulia, so aggressiveness ya Casemiro, Martinez na Fred inahitajika kwenye hii mechi.
Sitashangaa akianza Mc Tomminay tena, maana inaonekana kocha anamuelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…