Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Psg walikua wana mtaka rashford aka sugue benchi au watupe icard
 
Mkuu rebuild sio lazima uweke makinda pekee,hata aged players wanaweza kuwa na msaada huku ukiongeza mmoja mmoja.

Leo hii milner bado anaonekana muhimu liver japo aliondoka man city akiwa mzee.
Kuwa na wachezaji wenye umri mkubwa siyo tatizo kabisa tena ni muhimu ila shida kubwa huu usajili ni kama unafanyika kwasababu tu United imeanza msimu vibaya wame-panic halafu bado hatuvutii wachezaji zaidi ya mishahara minono kitu ambacho kinaharibu structure ya timu, tuna wachezaji wengi wa kawaida lakini wanapokea pesa ndefu.
 
Hii mimi ndiyo thinking Yangu
 
Yawezekana ni kweli ni panic buy chief, ila kwenda hizi match mpaka dirisha lijalo bila dm labda hututakii mema tu, tutapigwa hadi tushangae. Aje tu huku tunaendelea ku explore long term DM ajaye taratibu kuliko hii patner ya Mctominay na Fred
 
Timu bora Dunian mmepoa wanangu wa Manchester United [emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
Wamevurugwa wamepanic huko sokon wanakurupuka kununua kina casemiro waje Kula pesa za bure ....

Casemiro ana uefa zaidi ya 2 +makombe kibao ...

Ronaldo uefa zaidi ya 3+makombe kibao ....

Varane uefa za kutosha ....

Sasa unawasajili ili waje kukupa Nini kiu ya mafanikio kimpira haipo ,ila saizi wanajitakia pesa ,wazeeke na mishahara minono Kwan huko Madrid Perez anaakili kichizi hawezi ongeza mshahara kwa wachezaji wenye 30+ years ,hata wawe vzuri na mna gani kwani ni maji ya jioni ndio maana kawaacha kina Marcelo ,varane , Ronaldo,Sasa casemiro ,anaingiza damu changa kuzidi kuimalisha real Madrid Leo na kesho ......


ila Hawa wazee wa kukurupuka wanataka kunenepesha ng'ombe siku ya mnada subili uone watakavyo pigwa [emoji23][emoji23][emoji23]mtu Kama casemiro unaona kabisa yupo after money ,Hakuna taji ambalo unaweza mtishia ...
 
Mkuu,kwani hizo pesa ni zako? Mbona zinakuuma sana?😂
 
Mkuu rebuild sio lazima uweke makinda pekee,hata aged players wanaweza kuwa na msaada huku ukiongeza mmoja mmoja.

Leo hii milner bado anaonekana muhimu liver japo aliondoka man city akiwa mzee.

Hapa ndio Perez anawazidi viongozi wengine na its clear United hakuna rebuild yeyote ,matatizo yetu yanajulikana kwa miaka kadhaa mpaka muda wa usajili unaisha ndio tunaanza kukurupuka. Casemiro deal is very expensive kulingana na age yake kulikuwa na wachezaji wengi vijana wa kusajiliwa wa bei chee
 
Halafu casemiro wa Sasa Ni injury prone, Madrid game za UCL kashinda ,ila kiungo Chao kilikuwa kinazidiwa , angalia hata Zile game na Chelsea,

Casemiro wa Sasa anafata man u pesa , nasikia ana dabo salary

Man u wanarudia kosa Lile Lile walilofanya kwa Varane

Injury prone

Uwezo umepungua

Kocha wa man u hajui anataka nn, kwasasa anajifichia kwenye kichaka Cha wamiliki,

Hivi jiulize project ya man u Ni ipi ,analeta WAZEE , Tena Wala pesa ndefu

Kamsajiri Martinez beki mfupi amchezeshe Kati ,epl itakusulubu TU

Kamsajiri Malacia anakula benchi ,

Kamsajiri Eriksen maji ya jioni

Now anamleta casemiro

Hadi hapo unaona huyu Kocha ameshafeli , ila kwasasa anajifichia chini ya Kwamba Grazzer family ndio wenye shida.

Anadhani epl Ni ereveside

Kwa nionavyo Mimi soon mashabiki baada ya dirisha kutungwa watamkaanga yeye
 
Jamaa katoa maon TU, Kuna muda tuacheni ujinga, tujadili football

Football sio uhasama, jamaa hajatukana Wala kukashfu ,why usimjibu kwa kumchallange hoja yake
Mkuu,uhasama uko wapi hapo? Wapi nimemtukana hapo? Halafu ni muda sasa umefika Watanzania mjifunze kusoma maandishi katika sauti ya mwandishi.

Halafu hizi ni kauli za kawaida sana kwenye majadiliano ya mpira,hata sioni kama kuna kitu cha kubeba kwenye kifua hapo.
 
ni haki yako kuwaza, lakini sina uhakika kuwa uwezo wa kocha upo kama unavyotaka kutuaminisha, muda ni mwalimu mzuri sana uwe na akiba ya maneno kidogo [emoji276]
 
Baada ya man u kumpiga Liverpool magoli manne pre season, walitamani msimu uanze sasa msimu umeanza wanatamani uishe, ndo kwanza kipigo kikubwa ni kutoka kwa Brentford tu na hajakutana na pep, jurgen k, conte na tomas T.
 
Ktk usajili kuna targets 3 kuu kwa ajili ya
  1. Plan za muda mfupi (30+ yrs) - hawa ni wale wenye experience na ni wa muhimu kwa immediate impact kwenye timu
  2. Plan za muda wa kati (23-29yrs) - hawa ni wa muhimu kuiwezesha timu iwe na continuity nzuri kutoka kwa academy hadi kwa wazoefu
  3. Plan za muda mrefu (<23 yrs)- Hawa ni kwa ajili ya plan za 10+ years to come
Timu ikifanya usajili bila kuweka hiyo mix, itakwama tu kwenye mashindano
Ndio maana sisi Chelsea kupitia uongozi mpya tumewekeza kwenye hayo malengo matatu niliyotaja
Hii mix Man U hamkuwa nayo kwa muda mrefu na ndio maana leo hii Man U imekuwa hovyo hovyo tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…