Dogo ana potential sana. Kama unakumbuka last season wakati De gea ameenda Spain, kipindi mtoto wake anazaliwa(na ndio kipindi hicho De gea alikuwa na makosa mengi). Henderson alianza kucheza, na hata De gea aliporudi England dogo aliendelea kucheza. Hata final ya Europa nadhani alitakiwa kucheza, Ole akashindwa kumuamini. Dogo ana footwork nzuri na pia ni sweeper, hata shot-stopping ability ni nzuri(Rejea kiwango alichoonyesha akiwa Sheffield kwa mkopo). Nadhani ilitakiwa msimu huu ndo awe Goalkeeper wa kwanza, shida ni Ole kukosa uthubutu.. Timu zingine huwa haziogopi kufanya maamuzi magumu,, kama mnakumbuka kipindi kile Chelsea walivoamua kuachana na Cech halafu Courtois ndo akawa chaguo la kwanza