Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Pele akuhit 1000?
Wanaoongoza kwa ufungaji hao hapo according to FIFA ranking, huyo Pele ni wa tano
1647168407403.png
 
Hao hawana akili, naona cr7...kawarudisha kwenye reli na akiendelea katika ubora huu, top 4 guaranteed na kikubwa itahitajika MUMFUNGE ARSE8 ili kulower temper on 4th Spot!!!

View attachment 2148790
We ngj cr7 mnyama anakwenda kuwanyamazisha kwenye UCL zen hawa walalamikaji hawatamuongelea kabisa, kuna watu unaona kabisa hawana moyo mgumu lkn wanajua kwamba ng'ombe hazeeki maini lkn kuna haters hasa ukiangalia historia yao walikuwa Arsenal ndo wakatafuta timu wengine wakaenda Chelsea, wengine City, wachache ndio wakahamia United, na ndiyo hao unaoona wanamkondea Ronaldo maana haiingii akilini unawwzaje kumponda Ronaldo kwa mfano alafu we ni utd fan? Ni kweli kuna game anazingua but hyo ni kawaida lkn eti unakuta utd fan kabisa hampendi cr7 duuhh hata kama kachoka unaanzaje kumchukia mtu aliyetupa heshima kubwa kwenye soka? Jibu ni kwamba hao walikuwa mashabiki wa Arsenal zamani na lazima wamchukie cz aliwatesa sn miaka ile.
 
Kocha mpya asipokuja na mpango wa kutafuta kiungo wa chini mkali kama prime Matic ili ampeleke Fred juu sitamuelewa kabisa.

Fred akicheza juu,huku nyuma yake kukiwa na mtu anafanya mambo basi huwa anacheza kwa class ya juu sana..it's about time tulione hili.kuwachezesha pair na mtu kama McTominay ni upuuzi tu.

Rangnick nadhani ameona hilo..several time amemsogeza mbele na hii imesaidia amepata assists na magoli kadhaa chini ya muda Rangnick aliokaa klabuni.
Ni kweli kabisa tuna shida ya kiungo mkabaji, alafu kingine tunapoteza sn mipira aisee, yn ni ngumu utd players kukaa na mpira hata nusu dakika, kingine sioni sababu ya kubadilisha kocha cz tatizo la utd ni wachezaji.

Hakuna balance kwenye timu yetu yn kuna wachezaji wanakosekana wa kuleta balance ya timu hasa kiungo mkabaji, beki wa kati mwenye akili na mwenye macho, mtumaji na anayeweza kunusa hatari.

Pia beki namba mbili mwenye akili na mwenye kasi ya kupanda na kushuka, hao wakipatikana na kocha akabaki huyu huyu mbn tutabadilika. Tusiwe watu wa kukata tamaa na kocha wkt kikosi bado kina mapungufu, kama Liverpool wangekuwa na imani haba na kocha basi mpk leo ingekuwa mchezo ni kubadili makocha tu hata Klopp asingalikuwepo leo hii.

Tumuamini Ralph tumpe vitendea kazi tuone, kwanza uzuri wa Ralph anasikiliza mashabiki japo naye ana misimamo yake, lkn pia anawajibisha wazembe.

Kuna ombi langu kwa Ralph, msimu ujao aanze kutuondolea wapumbavu na aanze na El Capitano.
 
Kmmke! Dogo!

Leo ndio unaona umuhim wa man u kushinda ? Nikueleze sasa liverpool tutawaachia "utelezi" wajipigie wanavyotaka watukojolee hata 4 kama mlivyotukojolea nyie. Dawa ya moto ni moto.

Wewe upo tandale kwa tumbo unakula upupu ,unajua Nini kuhusu mpira 😅😅😅
 
Ni kweli kabisa tuna shida ya kiungo mkabaji, alafu kingine tunapoteza sn mipira aisee, yn ni ngumu utd players kukaa na mpira hata nusu dakika, kingine sioni sababu ya kubadilisha kocha cz tatizo la utd ni wachezaji.

Hakuna balance kwenye timu yetu yn kuna wachezaji wanakosekana wa kuleta balance ya timu hasa kiungo mkabaji, beki wa kati mwenye akili na mwenye macho, mtumaji na anayeweza kunusa hatari.

Pia beki namba mbili mwenye akili na mwenye kasi ya kupanda na kushuka, hao wakipatikana na kocha akabaki huyu huyu mbn tutabadilika. Tusiwe watu wa kukata tamaa na kocha wkt kikosi bado kina mapungufu, kama Liverpool wangekuwa na imani haba na kocha basi mpk leo ingekuwa mchezo ni kubadili makocha tu hata Klopp asingalikuwepo leo hii.

Tumuamini Ralph tumpe vitendea kazi tuone, kwanza uzuri wa Ralph anasikiliza mashabiki japo naye ana misimamo yake, lkn pia anawajibisha wazembe.

Kuna ombi langu kwa Ralph, msimu ujao aanze kutuondolea wapumbavu na aanze na El Capitano.
Ralf anaonekana hapendi ujinga kabisa..lakini ndo kama hivyo tumesikia bodi imeshaanza kutafuta kocha.
 
Ralf anaonekana hapendi ujinga kabisa..lakini ndo kama hivyo tumesikia bodi imeshaanza kutafuta kocha.
Hii bodi ndiyo inayotuharibia kila iitwapo leo, badala watafute wachezaji classic wa kuziba mapengo wao wanajishughulisha na makocha, wanatakiwa wamuamini kocha kwanza, hii timu kwa ss hata Ferguson mwenyewe angerudi angechezea za uso mpk angefia uwanjani.
 
robin van persie dhidi ya aston villa ndio naikumbuka hatrick yake.
Zimeshafungwa hat-trick 4 baada ya hiyo. Ya kwanza alifunga Martial baada ya miaka 7 tangu van Persie afanye hivyo ilikuwa against Sheffield United, ya pili alifunga Rashford against RB Leipzig, ya tatu akafunga Bruno msimu huu against Leeds United na ya nne ndiyo imefungwa na Ronaldo.
 
Back
Top Bottom