Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ralf will turn things around.
Kitu cha msingi ni kumpa mamlaka kamili juu ya sajili za wachezaji pale united kama alivyofanya Pep pindi anakuja city.
sehemu sahihi ya ralf ni ushauri, tumekuwa na rekodi mbovu sana ya kufanya maamuzi ya ovyo hivyo tunamuhitaji zaidi kwa kazi hiyo. murtough na fletcher kuwategemea peke yao ni kujidanganya.
 
kibaya zaidi huna uhakika wa kutimiziwa mahitaji yako kwa dirisha moja. pochettino yupo desperate na soka la uingereza hivyo ni rahisi kuja. wale midfields wa aston villa pamoja na beki zao za pembeni zina uhakika wa kucheza ndani ya timu yetu. tumetumia paundi billion 1 lakini bado timu haionyeshi ahueni
Na ndio hapa nawashangaa Gunners wenzangu wanaosema ili timu yetu iwe Bora haswa tajiri amwage tu mapesa
 
ukimuongezea wan bissaka tuliyemsajili kwa paundi million 50. kituko zaidi usajili wa wan bissaka unaambiwa takriban wachezaji 800 walifanyiwa utafiti halafu yeye akaibuka kinara, inaumiza na kustaajabisha. now tunavumishiwa kumhitaji tariq lamptey kwa paundi milion 30
Mkuu umeikumbuka namba 804 ya watahiniwa wa Ole ili kumpata Wanbisaka
 
Na ndio hapa nawashangaa Gunners wenzangu wanaosema ili timu yetu iwe Bora haswa tajiri amwage tu mapesa
pesa ikalenge wachezaji sahihi wanaoendana na falsafa za mwalimu husika au timu.kwa mfano chini ya guardiola hutoshuhudia mchezaji aina ya yanga mbiwa kwa sababu haendani na fikra za mwalimu. sijaangalia mechi za academy na zile za wanawake ila naamini man city wameshaingiza falsafa inayofanana ya kiuchezaji kwa timu zote
 
tulimuacha fabinho tukamkimbilia matic mwenye miaka 29.
Hii timu imepoteza watu wenye macho ya kuona vipaji vinavyochipukia matokeo yake wanakimbilia proven players ambao kimsingi kuja kwao united ni kutunisha mifuko yao tu.
Ni kama vile hii kazi ya scouting inafanywa na ndugu hivyo hawataki kuumiza vichwa zaidi ya kumtaja mchezaji ambaye hata mimi namuona.
 
Back
Top Bottom