fuentte
JF-Expert Member
- Jul 30, 2015
- 3,210
- 9,206
Wachezaji wetu wengi ni average sana na ukiongezea work rate yao kuwa chini ndipo wanaanza kuumbuka mwishowe wanataka kulalamikia mwalimu kila siku.hata Ole gunnar na benchi lake la ufundi likiongozwa na Kieran McKenna walivurumishiwa mvua ya maneno kama hayo matokeo yake na sisi mashabiki pamoja na wapenzi tukaingia choo cha kike kwa kuwaamini kwa haraka wachezaji na madai yao ya udhaifu wa benchi la ufundi.
amekuja ralf na falsafa zake za kibabe ameanza kuletewa hadithi kama zile za Ole.
kama bodi itawasikiliza wachezaji na madai yao tujiandae na anguko la milele kwa sababu hatokuja kocha mwengine yeyote atakayeweza kuwacontrol hao wachezaji na upumbavu wao.
Watu kama Park Ji Sung,Quintone Fortune,Sylvester,Oshea,Brown,Fletcher,n.k walikuwa sio world class ila walikuwa wanajituma sana kuficha udhaifu wao kiufundi.
Klabu ya Manchester united imeripotiwa kumpa mkataba wenye ofa ya mshahara wa £500k kwa wiki kiungo paul pogba,ambapo pogba akisaini mkataba huo atakuwa ni mchezaji anayelipwa zaidi katika historia ya ligi kuu uingereza.[@MailSport ]


