Manchester United (Red Devils) | Special Thread

 
daaah! Hii timu hata kuangalia mpira wake ni kazi mpira unachezwa hauna radha hata kidogo, wachezaji wetu control hawana we cheki mechi inaisha short on target 0_mmmh! Me nasema tena kuchange makocha bila kufukuza michezaji mizembe pale tutakua kama evatoni, wachezaji hawajitumi hadi hasira
 
Mashabiki wa Manchester United wanaweza wakapata mental disease usiku huu wa leo kwa sababu ya kichapo walichopokea usiku wa leo.

Mungu awatangulie kwa kweli wakuu. Japo najua mtapata usingizi wa shida ila hakuna namna. Ndiyo ukubwa huo.
Shida sio kichapo, shida kubwa inyoumiza ni huo mpira tunaocheza yaani hata Majimaji ya Songea wana afadhali, yaani utafkiri timu kwa mara ya kwanza ndio imepanda daraja msimu huu.
 
Juzi baada ya kuifunga Burnley (BURNLEY) Sista mmoja akatuma screenshot akazungushia na kaduara kumaanisha wana mechi mkononi na wakishinda mechi ijayo (Hii ya Wolves) anakua nyuma ya mshika namba 4 na akishinda ijayo anakua namba nne.

Sasa mimi nasema mwambieni SISI TULIO NAMBA NNE tumekubali kumpa points tatu za kiporo chake kisha alete screenshot ya msimamo tujue kama atakua kaifikia namba nne.

Next game ni dhidi ya Villa, mnaanza nao kwenye Carabao kisha ligi, mtatia aibu mkipotezwa kote kuwili.

Also clean sheet bado ni msamiati. Hawa ni wale walikua wakishangaa bei ya White wakawa wanasema Varane ameshinda makombe mengi yeye na Maguire watatengeneza ukuta umetulia.
Varane anapokea 340K back four ya Arsenal inapokea 310K lakini tunajua ni ukuta wa dunia ndiyo unasumbuka kupata clean sheet against Newcastle, Wolves, Burnley and the like
 
Kwa kipindi hiki kocha ni bora angetumia formation ya 4-5-1 kuliko kung'ang'ania hio Ngengemkeni yake.
 
Hii timu yangu pendwa kuliko yeyote duniani niliyoanza kuishabikia nikiwa kinda wa miaka 12 imenifanya nikomenti tena kwa huu uzi kwa mara ya pili tangia uanzishwe, kiukweli nashindwa kuelewa tatizo la timu yetu liko wapi, tangia mzee Fergie atuache hatujaweza kusimama tena kwenye soka la ushindani.

Tangu mwaka 2012 mpaka leo tumespend kununua top and complete world classic player's kuliko timu yeyote uingereza, amekuja Di maria, Falcao, ibrahimovic, pogba, n.k na sasa Sancho wote hao walishindwa kudeliver kabisa, tumewaleta makocha wakubwa duniani morinho, van gal , Moyes aliyekuwa wa moto kipindi hicho lakini wote wameshindwa, hata huyu Ralf simuoni akifanya maajabu ndani ya united.

Je tatizo la timu yetu nini haswa?, tuendelee kusubiri muujiza wa uponyaji labda, kwa sababu hata tungekuwa na klopp, Tuchel au Pep sizani kama wangetoboa kwa hali hii tunayokwenda nayo , nadhani hata ao tungewakataa tu.
Sasa je shida ya timu yetu ni nini, ni wapi tulikwama hadi kufikia hapa? Sioni cha kutusaidia kwa sasa zaidi ya kusubiri miujiza kwa miaka 30 kama ilivyokuwa kwa Liverpool.
 
Mashabiki na kipa watoe kwenye orodha ya wehu.
Yaani kwa hii timu ni bora hata majimaji ya songea wanacheza mpira unaoeleweka, yaani hata hip nafasi ya 6 sijui tumefikafikaje, ilitakiwa tuwe kule kwa kina New castle.
Huko chini maporomokoni ndiko mnakoenda sasaπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
hua tunajipa moyo tu kabla mechi, ila kiuhalisia tunajijua kabisa hamna timu hapo, tunawadindikiza tu wenye timu zao.
Lakini mkuu nilikwambia mapema ukanibeza.
Wolves siyo wepesi kama mlivyofikiria...Wolves bila kujikaza hutoboi wale jamaa.


Sasa nyie mlidhani mtawafunga kweli??
Nadhani leo mmeshuhudia mubashara ule ukuta na defence yao ilivyo.


Hamna timu hapo,
Mwanaume kushabikia manchester utd ambayo hata wadada hatuitaki aisee ni uzembeπŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…