Manchester United (Red Devils) | Special Thread

Ngoja tuendelee kuwakera sasa, naona msha maliza kujadili uozo wa timu yenu.
 
Kwa Ole formation ilifanya wasiwe average? Hivi mpo serious kumlaumu huyu mzee wa watu na udwanzi wa Rashford na Mctominay?
Kwanini kipindi Cha Sosha Scott na Rashiford walionekana wachezaji wazuri tofauti na kipindi hiki Cha RR, wewe haujiulizi?au kazi kumtetea Mzee wa maneno mengi mazuri RR kuliko Mourinho lakini kazi haionekani uwanjani?
 
Matumaini gani alikupa Sosha kaka
Hakunipa Mimi matumaini,Bali bodi ya timu na mashabiki pia Na ndo maana akawa anaongezewa muda mpaka kufika miaka mitatu Kwa matumaini ya kuwa Kuna siku atafanya vizurii na Yote ni kutokana na matokeo aliyo kuwa akiyapata nyuma,Kwa kufika nusu fainal euroapa Ligi,fa cup,na Kombe la Ligi,kufika fainal licha ya kupoteza mbele ya Villarreal,kumaliza nafasi ya tatu,msimu uliopita nafasi ya pili.

Lakini huyu Mzee asipobadilika na KUENDELEA na gengen dressing Kwa wachezaji wa united ataishia nafasi ya 8 au ya 9 na mashindano mengine hatofika mbali.
 
@Moderator na timu yake imelala.

Watu wazima wenye akili zao wameachana na hili jukwaa. Wamebaki wapumbavu wenye matusi na hawana hoja zenye mashiko.

Siku hizi zile hoja zenye mashiko hazipo tena.

Binafsi nafikiria kuondoka humu for good.
 
Kwa hali tuliyofikia Man united tunahitaji a pragmatic Manager than a football philosopher.

Manchester United kwa sasa ina wachezaji wengi ambao ama hawawezi tena kuchezea Man United au hawataki tena kuitumikia timu.

Kwenye rebuild ya Solkjaer kila tulipojenga kona moja kona nyingine ilibomoka.

Hii orodha inapaswa kupewa mlango wa kutokea.
1. Nemanja matic
2.Juan Mata
3. Phil Jones
4. Harry Maguire
5. Anthony Martial
6.Jesse Lingard
7. Paul Pogba

Hawa watu wanazuia timu yetu kufanya usajili wa wachezaji watakoleta ushindani.
 
Mkuu usimsahau na Rashford tafadhali
 
Rashford anachezeshwa ametoka kwenye injury ya bega lakini bado ni mchezaji mzuri
Mkuu Rashford ana matatizo makuu matatu
1. mara nyingi amekuwa na ubinafsi wa pass kwa wenzake
2. end product yake hainivutii kulingana na ukubwa wa jina lake.
3. Mechi moja anakuwa vizuri inayofuata anacheza kama kapoteza akili yake.

Hata hivyo sidhani kama board itamtoa kirahisi pale united.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…