D A E M U S H I N
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 22,633
- 121,022
Ningelikuwa nipo ndani ya bodi ya klabu ningelipendekeza ralf rangnick apewe kandarasi ya miaka miwili akiwa kama kocha mkuu na si mshauri wa klabu kama mkataba wa sasa unavyozungumza, na hii ni kwa sababu bado siamini ya kwamba nafasi yake ya ushauri itampa nguvu sawa ya kumsimamia na kuhoji maamuzi ya kocha mkuu ajaye kiundani na uwazi zaidi.
mungu wa mpira ametuletea nabii wa mpira ndani ya timu atakayeweza kutuongoza kuelekea njia sahihi baada ya kupotea kwa muda mrefu bila ya kujua ni ipi njia sahihi tunayopaswa kuifuata hivyo tusije kuipoteza fursa hii na kuendelea kuichagua njia ile ile iliokwisha tukwamisha.
pia mashabiki, legends na viongozi waandamizi wa klabu wanapaswa wavisafishe vichwa vyao ambavyo bado vimebeba fikra za kizamani zinazowafanya wajione bado tuna timu bora, bado tuna timu yenye uwezo wa kuleta ushindani dhidi ya wengine na vile vile bado tuna timu yenye wachezaji bora kama wengineo (kama vile man city, liverpool, bayern munich, real madrid na chelsea) na kuziendeleza fikra hizo zinazobebwa zaidi na historia yetu ni kuendelea kujidanganya na kuifuata njia ya motoni ambayo tumeshaanza kuifuata.
Hatua walioamua kuianza Arsenal na hata Barcelona ndio tunapaswa na sisi tuifuate bila ya kujali ni kipi kinazungumzwa au kufanywa na majirani zetu (man city, liverpool, chelsea) kwa sababu wao tayari wameshatutangulia na kutuacha kwa hatua kubwa. Laiti kama ingelikuwa kanuni ya time travelling inafanya kazi halafu ukawauliza viongozi wa arsenal baada ya kusafiri na muda kwa kurudi nyuma hadi 2018.
" hivi tumsajili pepe kwa paundi millioni 80 au tumsubirie bukayo saka huyu mwenye miaka 17, bila ya shaka jawabu litakalotoka vinywani mwao ni la kumsubiria bukayo saka kwa sababu tayari wameshamuona anachokifanya mwaka 2021 ni bora zaidi kuliko kitakachofanywa na pepe"
ralf rangnick aliwahi kusema : ni bora usisajili kabisa kuliko kusajili mchezaji ambaye si sahihi.
liverpool wamekuwa wakiitumia kanuni hii licha ya kwamba klopp baadhi ya nyakati anabanwa na kikwazo cha bajeti ya kutimiza mahitaji yake hatimaye hujifichia hapo.
Arsenal nao wameanza kuitumia kanunii hii na wanakwenda vizuri huku wakisafisha takataka zinazobeba mishahara mizuri huku work rate ikiwa ni ndogo na hata Barcelona nao wanaelekea kuitumia njia hii.
Rangnick ndiye mwanadamu pekee aliyebaki kwenye ulimwengu wa soka mwenye uwezo wa kutusafishia hawa wahuni na washenzi waliotamalaki ndani ya kikosi cha manchester united na kuleta wachezaji watakaoendana na falsafa zake, si guardiola, klopp wala arteta anayepatikana sokoni kama tutaweza kumchukua msimu ujao.
Nimemtaja Arteta si kwa sababu ya ubora wake bali ni ule ukakamavu wake wa kusimama kama bosi ndani ya klabu na ni suala la muda tu kabla hajamuonyesha mlango wa kutokea pierre aubameyang ili kuwaonyesha wachezaji wengineo ukuu wake kwa mara nyengine (alishafanya hivyo kwa mesut ozil, amemweka benchi kipa namba 1 kwa nusu msimu).
Rangnick ni mjeuri na muelewa wa mpira wa kileo kuliko mourinho, ni suala la muda tu kabla hatujashuhudia vita vya mwanaume na vijanadume vinavyokula mshahara wa paundi laki 2 huku wakiingia uwanjani wanapoteza possession mara 120 kwa dakika 90.
mara hii itakuwa ni kazi ya bodi ya klabu kuchagua upande