Yule kilaza Ole alishusha hali ya kujiamini ya wachezaji. Jaribu kuvuta picha Arsenal, West Ham walituzidi zaidi ya alama 7 kabla ya mchezo wa Chelsea.
Heshima yangu kwake kama mchezaji wetu mahiri itabaki pale pale ila kama kocha alikuwa kituko sana.
Kumbe huyu kocha wa young boyz naye ni zao la professor rangnick, kupitia interview yake hapo jana alisema yeye ndiye aliyempa nafasi timu ya vijana ya hoffenheim, jinsi alivyokuwa anaizungumzia young boys na mwenendo wao kwenye ligi yao imeonyesha jinsi gani rangnick alivyo na utajiri wa taarifa za soka. Rangnick anatisha na wasiwasi wangu hata hii ligi ya diamond na ali kiba pia anaifahamu kiundani. Teh teh teh